read

Aya 75: Je Mna Matumaini Wataamini?

Maelezo

Kilamwenyeujumbefulanihuwaanapupiawatuwauaminiujumbehuo.Kwa hivyo anaueneza kwa matumaini ya kupata wafuasi wengi, na anahimili taabu na mashaka katika hilo, kama alivyofanya Mtume (s.a.w.) na sahaba zake, waliueneza mwito wa Uislamu katika pembe zote kwa kutaraji kupata wafuasi.

Kulikuwa na mfungamano wa kijirani, kibiashara na hata kunyonyeshana watoto kati ya Ansar na Mayahudi. Hivyo wakawalingania kwenye Uislamu kwa amri ya Mtume. Wakawatolea dalili kwa hoja zinazoingia akilini na kwa mantiki mazuri, wakatumai kwamba nyoyo zao zitashtuka, hasa kwa kuzingatia kwamba wao ni watu wa Kitabu na kwamba sifa za Muhammad (s.a.w.) zimetajwa kwa uwazi katika Tawrat yao.

Walipoendelea Wayahudi kukaidi mwito wa Uislamu na kuendelea kukufuru na kuipinga haki, ndipo Mwenyezi Mungu alipomwambia Mtume wake kwa kusema: Je mnatumaini nyinyi Waislamu ya kwamba watawaamini hao Mayahudi, na hali wazee wao hawa Mayahudi walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa Nabii Musa (a.s.) pamoja na miujiza, lakini wakiyabadilisha na kuyageuza vile matamanio yao yanavyotaka pamoja na kujua kuwa hayo maneno ni ya haki?

Kwa hivyo, hali ya Wayahudi wa Madina ni kama hali ya wazee wao waliopita, ambao walibadilisha halali ikawa haramu na haramu kuwa halali kwa kufuata matamanio yao na wakabadilisha sifa za Muhammad (s.a.w.) zilizopokewa katika Tawrat, ili isiweko hoja juu yao.

Mwenye Majmaul-Bayan anasema: “Katika Aya hii kuna dalili juu ya ukubwa wa dhambi ya kuibadilisha sheria. Na dhambi hiyo inapatikana katika kuleta Bid’a katika fatwa au hukumu na mambo yote ya kidini.”

Kuongezea juu ya maneno hayo ya mwenye Majmau ni kuwa Aya hii ni dalili juu ya kuwa mwenye kufuata upotevu kwamba sio kuwa anajifanyia uovuyeyemwenyewetu,baliathariyakeinaeneakwavizazi,kama ilivyoelezwa katika Hadith.

وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ قَالُوا أَتُحَدِّثُونَهُمْ بِمَا فَتَحَ اللَّهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَاجُّوكُمْ بِهِ عِنْدَ رَبِّكُمْ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ {76}

Na wanapokutana na wale walioamini husema: Tumeamini. Na wanapokuwa peke yao, wao husema: Mnawaambia yale aliyowahukumia Mwenyezi Mungu ili wapate kuhojiana nanyi mbele ya Mola wenu? Je, hamna akili?

أَوَلَا يَعْلَمُونَ أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ {77}

Hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyafanya siri na wanayoyadhihirisha?