read

Aya 51 – 53: Na Tulipomwahidi

Lugha

Neno Musa kwa lugha ya Kiarabu lina maana ya kifaa cha kunyolea nywele kilichotengezwa kutokana na chuma; lakini maana yanayokusuduwa kwa Musa bin Imran siyo ya Kiarabu, bali ni ya Kikibti ambayo ni matamko mawili:
Mu lenye maana ya maji na Sa lenye maana ya mti. Kwa hiyo maana ya Musa ni maji ya mti, Ama maana ya kuitwa Maji ya mti, kama ilivyoelezwa katika Majmaul- Bayan, ni kwamba wajakazi wa Asiya(mke wa Firaun), walitoka kwenda kuoga wakakuta sanduku lililokuwa na Musa ndani yake baina ya maji na mti; wakawa naye.

Maelezo

Baada ya Firaun kuangamizwa na Mwenyezi Mungu na waliokuwa pamoja naye, Waisrail Walipumua, wakarudi Misri wakiwa salama; kama livyoelezwa katika Majmau. Wakati huo, Tawrat ilikuwa bado haijateremshwa, wakamtaka Musa awaletee kitabu kutoka kwa mola wao. Basi Mwenyezi Mungu akamwahidi kumteremshia Tawrat na akamwekea wakati. Musa akawaambia:

“Hakika Mola wangu ameniahidi kitabu ambacho ndani yake mna ubainifu wa ambayo ni wajibu kwenu kuyafanya na kuyaacha.”

Akawambia wakati wake ambao ni masiku arobaini, na masiku hayo-kama ilivyosemwa - ni mwezi wa Dhul-Qaada, na siku kumi za mwezi wa Dhul-Hijja.

Musa akenda kwa Mola wake ili awachukulie watu wake kitabu; ndugu yake Harun akawa naibu wake. Kabla ya kwisha muda wa kuja Musa, walianza kuabudu ndama badala ya Mwenyezi Mungu, wakajidhulimu wao wenyewe.

Hayo ndiyo maana ya dhahiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na tulipomwahidi Musa masiku arobaini mkafanya ndama (kuwa Mungu) badala ya Mwenyezi Mungu mkawa madhalimu ( wa nafsi zenu).”

Baada ya Musa kurejea kwa watu wake, walitubia na wakarudi kwa Mola wao; Mwenyezi Mungu akawakubali toba yao na hii ni neema ya tatu ambayo imeelezewa katika Aya: Kisha tukawasamehe baada ya hayo.

Amaneemayannenikitabucha MwenyeziMungu:NatulipompaMusa kitabu na upambanuzi ili mpate kuonoka.” Kisha chenyewew ni Tawrat; yenye kukusanya kila kitu kwa ajili ya kubainisha haki na batili, na halali na haramu.

Kunganisha kati ya neno, kitabu na kupambanua, ni kuunganisha sifa kwenye kile kinashosifiwa. Kwa muhtasari ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewakumbusha Waisrail katika Aya zilizotangulia, neema nne. Kuwaokoa kuchinjiwa watoto wao wa kiume na kuachwa wa kike wawe watumwa, kuangamia kwa Firaun, kusamehewa na kuletewa Tawrat.

Maelezo mazuri zaidi niliyoyasoma kuhusu maudhui haya ni kauli ya Abu Hayan Al-AndulusikatikaTafsirAl-BahrulMuhit;namnukuu:

Tazama uzuri wa safu hizi ambazo zimepangika kwa mpango wa mtungo wa lulu na wa sayari katika falaki zake, kila safu katika hizo, yaani neema, imeishia kwa mnasaba wake na ikafikia daraja ya juu ya ufasaha ukitoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia mdomoni mwa Muhammad mwaminifu wake, bila ya kusoma kitabu chochote kabla yake, wala kuandika kwa mkono wake.”

Abu Hayan anaonyesha kuwa mpangilio huo wenye kupangika vizuri ni katika miujiza ya Muhammad; kwamba yeye anauelezea bila ya kujifundisha.

Mwenyezi Mungu awarehemu wahenga, awasamehe na awape neema nyingi. Kwani hakika wao hawakuona chochote chenye harufu ya kuitilia mkazo dini hii na Mtume wake mtukufu isipokuwa walikinyooshea shingo kwa pupa na shauku; wakafanya haraka kukisherehesha, kukifafanua na kukitolea dalili.

Lakini tuko wapi sisi wanavyuoni wa sasa ambao twapupia zaidi dunia; hatuoni umuhimu wowote isipokuwa umuhimu wetu tu; wala matatizo isipokuwa matatizo ya watoto wetu tu! Tuko wapi sisi na hao watukufu waliojitolea kila kitu kwa ajili ya kuutukuza Uislamu na Mtume wa Uislamu? Mwenyezi Mungu awasamehe na awainue, na kila mwenye kuitumikia dini, kwenye daraja ya juu.

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنْفُسَكُمْ بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَاقْتُلُوا أَنْفُسَكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ

عِنْدَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ {54}

Na Musa alipowaambia watu wake; Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmejidhulumu kwa kufanya kwenu ndama (kuwa ni Mungu). Basi tubini kwa Muumba wenu na jiueni; hilo ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu. Basi akapokea toba yenu. Hakika Yeye ndiye apokeaye toba Mwenye kurehemu.

وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَنْ نُؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى اللَّهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْكُمُ الصَّاعِقَةُ وَأَنْتُمْ تَنْظُرُونَ {55}

Na mliposema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mungu waziwazi. Ukawanyakua ukelele na hali mwatizama.

ثُمَّ بَعَثْنَاكُمْ مِنْ بَعْدِ مَوْتِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ {56}

Kisha tukawafufua baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru.

وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْغَمَامَ وَأَنْزَلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۖ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَٰكِنْ كَانُوا أَنْفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ {57}

Tukawatilia kivuli kwa mawingu na tukawateremshia Manna na Salwa: Kuleni katika vitu vizuri tulivyowaruzuku. Na hatukuwadhulumu, lakini wamejidhulumu wenyewe.