Aya 110: Na Simamisheni Swala
Maana
Aya hii imekusanya mambo matatu:
1. Kuamrisha kusimamisha swala
2. Kuamrisha kutoa zaka
3. Kuhimiza herikwa ujumla
Katika Tafsir ya Al-Manar imeelezwa kwamba Aya ina madhumuni ya hukumu mahsusi ambayo ni kuamrisha swala na zaka. Kisha imetaja hukumu kwa ujumla ambayo iko peke yake, lakini ujumla wake unakusanya pia hukumu mahsusi iliyotangulia. Na huu ni katika mfumo wa Qur’an ambao ni wa aina yake.
Mtaikuta mbele ya Mwenyezi Mungu
Makusudioyakenikukutamalipo yake na thawabu zake sio kukuta amali yenyewe, kama ilivyosemwa kwa sababu amali hazibaki.
Unaweza kuuliza:Tumeona Qur’anmara kwa mara inakutanishaamriya swala na ya zaka; Je, kuna siri gani?
Limejibiwa swali hili kwamba swala ni ibada ya kiroho na zaka ni ibada ya kimali, mwenye kuitekeleza kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu inamuwia wepesi kujitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Swala Na Vijana Wa Kisasa
Vijana wengi wa kisasa wanapuuza dini na wanaoshikamana nayo; wengine wanasema wazi kuwa chochote zaidi ya hivi vitu vilivyoko.” Wengine wanasema kuwa yuko mwenye kupanga mambo vizuri na mwenye hekima, lakini hakuwajibisha saumu wala swala. Aina zote hizo mbili za watu mbele ya Mwenyezi Mungu ziko sawa katika ukafiri. Kwa sababu mwenye kuacha swala kwa kuamini kuwa sio wajibu, huyo ni sawa na anayemkanusha Mwenyezi Mungu.
Na sisi wanavyuoni tunawaangalia vijana wa kisasa wakiendelea kupuuza dini na kuikataa haki, bila ya kufanya kazi yoyote au kuwakinaisha kwa namna yoyote ile.
Nikisema kazi, nakusudia kazi za ushirikano zenye kuleta matunda ambazo zinataka maadili na vikao vya kujadili namna ya utekelezaji kisha kufunguliwe shule na vyuo vya elimu ya Qur’an, Hadith, Falsafa ya Itikadi ya Kiislamu, Historia ya Kiislamu na elimu ya nafsi (Saikolojia).
Vilevilekuwenamazoeayakutoamawaidhanayakulinganiakwenye dini kwa njia nzuri na ya kisasa. Ndio, wengine wamefanya juhudi zao zilizoleta natija ambazo zinafaa kutolewa shukurani. Lakini linalotakikana hasa ni kuzishirikisha pamoja juhudi hizo na kuwa na Ikhlasi katika nia na kujitolea mhanga katika yote. Lakini vipi zitashirikishwa pamoja juhudi na hali wenye kutaka kuchuma kwa jina la dini ni wengi ambao hawaoni umuhimu na haliwashughulishi lolote zaidi ya lile litakalowapatia jina na mali tu?
Kwa hiyo jukumu la kuwalea vijana ni letu sisi wanavyuoni wa dini, na tutaul-izwa hilo mbele ya Mwenyezi Mungu; sawa na vile ambavyo wao nao wataulizwa kutokana na kupuuza na kuacha kutafuta kujua dini ya haki na kutumia hukumu zake.
وَقَالُوا لَنْ يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَنْ كَانَ هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ ۗ تِلْكَ أَمَانِيُّهُمْ ۗ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ {111}
بَلَىٰ مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُ أَجْرُهُ عِنْدَ رَبِّهِ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ {112}
وَقَالَتِ الْيَهُودُ لَيْسَتِ النَّصَارَىٰ عَلَىٰ شَيْءٍ وَقَالَتِ النَّصَارَىٰ لَيْسَتِ الْيَهُودُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُمْ يَتْلُونَ الْكِتَابَ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ مِثْلَ قَوْلِهِمْ ۚ فَاللَّهُ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ {113}