read

Aya 180-182: Urithi Wa Mbingu Na Ardhi Ni Wa Mwenyezi Mungu

Maana

Na wasidhanie kabisa wale ambao wanafanyia ubakhili vile alivyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kuwa ni bora kwao, bali ni shari kwao.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuhimiza kujitolea mhanga kwa nafsi, amefuatishia kuhimiza kujitolea kwa mali. Makusudio ya Aya hii ni wale wanaojizuia kutoa Zaka na Khumsi ambazo ni wajibu, na wala sio kutoa sadaka ya sunna. Kwa sababu kiaga kikali ambacho kinaelezwa na Aya kinaonyesha kuacha wajibu, sio kuacha sunna.

Imesemekana pia kuwa makusudio ni mwenye kuficha jina la Muhammad (s.aw.) na sifa zake zilizokuja katika Taurat na Injil. Vilevile imesemekana ni kufanya ubakhili wa elimu kwa anayeihitajia. Lakini linalokuja haraka kwenye fahamu, ni kufanya ubakhili kwenye mali. Hilo linaonyeshwa na kauli yake Mwenyezi Mungu. Watatiwa mandakozi ya hivyo walivyovifanya ubakhili siku ya kiyama. Hii ni tafsiri ya; 'na ni shari kwao.'

Kutiwa mandakozi, hapa ni fumbo la adhabu kali, kama vile Mwenyezi Mungu alivyosema. Siku (mali) itakapotiwa moto katika moto wa Jahannam na vichomwe vipaji vyao vya nyuso na mbavu zao na migongo.yao kwa mali hiyo.” (9:35)

Matajiri Ni Mawakala Sio Wenyewe

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amehimiza kutoa mali katika Aya kadhaa, nyingi katika hizo ameonyesha kuwa mali zote sio miliki ya aliyenazo, isipokuwa ni miliki ya Mwenyezi Mungu peke Yake na kwamba mtu amewekewa amana tu kuruhusiwa kuitumia kwa mipaka maalum bila ya kuikiuka kama alivyo wakala, hufuata matakwa ya mwenye mali katika matumizi yote.

Miongoni mwa Aya nyingine zilizotaja hayo ni: "Na tafuta - kwa yale aliyokupa Mwenyezi Mungu - makazi mazuri ya akhera." (28:77). "Toeni katika yale aliyowapa Mwenyezi Mungu." (36:47) Aya iliyo wazi zaidi ni ile isemayo. "Na toeni katika yale ambayo (Mwenyezi Mungu) amewafanya kuwa makhalifa kwenye hayo" (57:7) maana ya kuwa khalifa ni kuwa kaimu.

Katika Hadith Qudsi anasema: "Mali (zote) ni zangu, na matajiri ni mawakala wangu, mafukara ni watu wangu (wanaonitegemea) basi mwenye kuwafanyia ubakhili watu wangu, nitamwingiza motoni bila ya kujali."

Kwa hivyo, Aya na Hadith zinafahamisha kuwa Uislamu haukubali miliki ya mtu kwa aina yoyote ile, ni sawa iwe ni miliki ya mtu binafsi kabisa, kama ulivyo mfumo wa kibepari, au milki ya kiwango maalum, kama ulivyo mfumo wa kijamaa, au hata miliki ya umma, kama ulivyo mfumo wa kikomunist.

Aina zote hizi zinakanushwa na uislamu na kubakia milki ya kihakika ya Mwenyezi Mungu peke Yake, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amehalalishia mtu kutumia mali kwa ajii yake na watu wake kwa uzuri, na pia kuitumia katika njia ya kheri kwa sharti ya kuipata kwa njia ya halili siyo ya haramu; kama vile kughushi, kuhadaa, kunyang'anya, rushwa, riba, ulanguzi na kufanya biashara ya ulevi. Kwa hivyo ruhusa ya kuitawala mali na kutumia ni kwa kiwango maalum.

Unaweza kuuliza, baadhi ya Aya zinafahamisha kuwa mali ni milki ya mtu,kama "Piganeni jihadi kwa mali yenu" "Wapeni mayatima mali zao." Katika Hadith imeelezwa. "Damu zenu na mali zenu ni haramu (kwa mwengine)." Na "watu ni wenye mamlaka juu ya mali zao." Na bei na urithi ni katika mambo ya lazima ya dini na sheria ya kiislamu. Kwa hivyo basi, si haifai kusema kuwa uislamu hau- tambui milki ya mtu kwa aina zote?

Jibu: kutegemeza mtu kitu kunafaa kwa mnasaba ulio karibu. Kwa mfano kumwambia mgeni sahani yako au kumwambia mpotea njia, "hii ndiyo njia yako." Hapa inajulikana wazi kwamba mgeni hana sahani, isipokuwa makusudio ni mgeni ale kwa kutumia sahani hiyo `na mpotea njia, hana njia isipokuwa ni kufuata hiyo njia. Kwa hiyo mali inaegemezwa kwa mtu kwa kutumia kwa njia ya halali na kwa ruhusa sio kwa njia ya milki; kama kauli yake Mwenyezi Mungu. "Na Mwenyezi Mungu amewafanyia wake katika jinsi yenu." (16:72)

Na kauli ya Mtume (s.a.w.) "Wewe na mali yako ni ya babako." Kwa dhahiri ni kwamba mke siye milki ya mume kabisa wala mtoto si milki ya kihakika ya mzazi.

Ama mauzo na mirathi ni utambulisho wa haki; yaani uislamu umemjaalia mwenye mali kuitambulisha itumiwe na mwengine, wakati huo huo umehalalisha haki maalumu kwenda kwa mrithi na mnunuzi. Na tofauti kati ya milki ya utambulisho na milki ya hakika ni kubwa.

Kwa ufupi ni kwamba uislamu umehalalishia mtu kuhodhi mali kwa sharti maalu- mu na kuitoa kwa sharti mahsusi, ukasisitiza sana juu ya masharti haya na kuharamisha kuyakiuka. Hii peke yake inatosha na ni dalili wazi kwamba mwanadamu ni wakala wa mali na si mwenye mali, kama si hivyo, basi ingelijuzu kwake kutumia bila ya masharti yoyote.

Ni vizuri tumalizie mlango huu kwa kauli ya Imam Jafar as-Sadiq (a.s.): "Mali ni ya Mwenyezi Mungu, nayo ni amana kwa waja wake. Amewaruhusu kula bila ya kuifuja, kuvaa bila ya kuifuja, kuoa bila ya kuifuja na kupanda (k.v. farasi) bila ya kuifuja. Itakayozidi hapo itarudi kwa mafukara waumini kurekebisha hali yao. Atakayefanya hivyo, basi anachokila ni halali, anachokinywa ni halali, anachokipanda ni halali na aliyemuoa ni halali, zaidi ya hivyo ni haram."

Hakika Mwenyezi Mungu amekwisha sikia kauli ya wale waliosema: Hakika Mwenyezi Mungu ni fukara na sisi ni matajiri.

Aya haikutaja majina ya waliotamka kufuru hii, lakini wafasiri wamenakili kuwa Mtume alipoteremshiwa Aya hii. "Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri." (2:245). Wayahudi wa Madina waliwokuwako wakati wa Mtume, walisema "Fukara tu, ndiye anayetaka mkopo kwa tajiri.

Kwa hivyo Mwenyezi Mungu ni fukara na sisi ni matajiri." Hili sio la kushangaza kwa Mayahudi hasa wale matajiri. Kwa sababu misingi yao na kazi zao zinafahamisha wazi uovu huu na kutojali misimamo ya kibinadamu. Na mwenye kufuatilia historia ataona kuwa hakuna sehemu yoyote duniani isipokuwa imeathiriwa na ufisadi wao na malengo yao maovu.

Hakuna ufasaha unaofahamisha taswira ya hakika ya ukweli wa Uyahudi kuliko kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Na utawaona wengi wao wanakimbilia kwenye dhambi na uadui na ulaji wao haramu. Hakika ni mabaya kabisa wayafanyayo. Mbona watawa wao na wanavyuoni wao hawakatazi maneno yao ya dhambi na ulaji wao haramu. Hakika ni mabaya kabisa wayafanyao. Na Mayahudi walisema: mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndiyo iliyofumba, na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema." (5: 62-64)

Sina shaka kabisa kwamba kila mwenye kuingilia hekima ya Mwenyezi Mungu na akasema kwa ulimi wake maneno, kwa mfano, 'Ilikuwa haifai kwa Mwenyezi Mungu kufanya hivi, isipokuwa angefanya hivi' sina shaka kuwa anayesema hivyo atakuwa pamoja na waliosema. Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba; atake asitake.

Tutaandika yale waliyoyasema.

Hili ni kemeo la kiaga cha wale waliosema. "Hakika Mwenyezi Mungu ni fukara na sisi ni matajiri." Kwa sababu kuandika dhambi kunapelekea adhabu.

Na kuuwa kwao Mitume. Pia tutaandika wa kale wao walivyowaua Mitume. Kumenasibishwa kuua kwao, ingawaje walioua ni wa kale wao. Hayo yamekwishaelezwa katika tafsir ya Aya 21 ya Sura hii.

Hayo ni kwa sababu ya yaliyotangulizwa na mikono yenu; na kwamba Mwenyezi Mungu si dhalimu sana kwa waja.

Vipi atadhulumu na Yeye amekataza dhulma na kuifanya kuwa ni kubwa ya madhambi makubwa na katika Aya nyingi akiita kuwa ni kufuru?

Zaidi ya hayo dhalimu anadhulumu kwa sababu tu anahitajia hicho anachokifanyia dhulma. Na Mwenyezi Mungu amejitosheleza na kila kitu. Kwa msingi huu wa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kujitosha na hahitajii kitu, kunathibitisha uadilifu wake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) vilevile kunathibitisha kwamba yeye hana mwili, kwa sababu mwili unahitaji vitu.

Kwa hivyo, inatubainika kubatilikia kwa madhehebu ya wanaosema kuwa shari inatokana na Mwenyezi Mungu, na kwamba yeye anamtengenezea maasi mja, kisha amwadhibu.
Pengine watafute njia ya kuhepa kauli hii ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hakika Mwenyezi Mungu si dhalimu wa waja. Kwa vile ametumia neno Dhallam lenye maana kudhulumu sana iwe anaweza kudhulumu kidogo, lakini sio sana! Mwenyezi Mungu ametakasika kabisa na wayasemayo madhalimu.

الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّهَ عَهِدَ إِلَيْنَا أَلَّا نُؤْمِنَ لِرَسُولٍ حَتَّىٰ يَأْتِيَنَا بِقُرْبَانٍ تَأْكُلُهُ النَّارُ ۗ قُلْ قَدْ جَاءَكُمْ رُسُلٌ مِنْ قَبْلِي بِالْبَيِّنَاتِ وَبِالَّذِي قُلْتُمْ فَلِمَ قَتَلْتُمُوهُمْ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ {183}

Wale ambao wamesema: Hakika Mwenyezi Mungu ametuahidi kuwa tusimwamini Mtume yeyote, mpaka atuletee kafara itakayoliwa na moto. Sema: Hakika waliwajia Mitume kabla yangu kwa hoja zilizo waziwazi na kwa hayo mliyosema basi mbona mliwaua kama mu wa kweli?

فَإِنْ كَذَّبُوكَ فَقَدْ كُذِّبَ رُسُلٌ مِنْ قَبْلِكَ جَاءُوا بِالْبَيِّنَاتِ وَالزُّبُرِ وَالْكِتَابِ الْمُنِيرِ {184}

Kama wakikukadhibisha, basi hakika wamekadhibishwa Mitume kabla yako waliokuja na hoja waziwazi na vitabu vya waadhi na kitabu chenye mwanga.