Aya 5-6: Msiwape Wapumbavu Mali Zenu
Lugha
Makusudio ya wapumbavu hapa ni wale wabadhirifu wanaotumia ovyo mali.
Maana.
Wala msiwape wapumbavu mali zenu .
Imesemekana kwamba msemo unaelekezwa kwa kila mwenye mali na kwamba anaamrishwa kutompa ambaye ataitumia pasipo mahali pake; ni sawa mbadhirifu awe ni mtoto au mke wa mwenye mali. Vilevile wasii wake au mtu wa kando.
Pia imesemekana kuwa msemo unaelekezwa kwa mababa tu, kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewakataza kuwakabidhi watoto wao waasi mali waliyofadhiliwa na Mwenyezi Mungu na wanapozeeka wanaijutia.
Ilivyo hasa ni kwamba msemo unaelekezwa kwa wasimamizi, kwa maana ya kuwa enyi wasimamizi msiwape wabadhirifu mnaowasimamia mali zao.
Hilo linafahamika kutokana na Mwenyezi Mungu anavyoendelea kusema, 'Na muwakimu na muwavishe katika mali hiyo.' Kwa sababu huu ni msemo unaelekezwa kwa wasi- mamizi. Zaidi ya hayo Aya zilizotangulia zinawahusu wasimamizi kwa hiyo inakuwa vizuri kufungamana na hizo.
Mbadhirifu, ni yule anayetumia ovyo mali yake; huyu hawezi kutumia mali yake isipokuwa kwa idhini ya msimamizi (walii) wake. Lakini anaweza kutumia vitu visivyoambatana na mali. Tumezungumzia kwa urefu kuhusu hukumu za mbadhirifu katika kitab Fiqhul-Imam Jafer As-sadiq, mlango wa Hajr.
Unaweza kuuliza: Kama msemo ungekuwa unawahusu wasimamizi wa mali za wabadhirifu, ingelazimika kusema, 'mali zao' na wala sio 'mali zenu', Sasa imekuaje?
Jibu; Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametegemeza mali za wabadhirifu kwa wasimamizi wao kwa kuangalia kuwa ziko chini ya usimamizi wao. Na inajulikana kwamba kutegemezea kitu kunafaa hata kwa sababu ndogo tu.
Kumwamini Mwenyezi Mungu Na Tatizo La Maisha
Mali zenu ambazo amewajaalia kuwaendeshea maisha.
Razi anasema: "Maana yake ni kuwa maisha hayapatikani ila kwa mali. Ilipokuwa mali ndiyo sababu ya kuendesha maisha, ndipo Mwenyezi Mungu akaiita kuwa ni ya kuendeshea maisha kwa kutumia jina la chenye kusababishwa kwa sababu. Sababu anayomaanisha ni mali, na chenye kusababishiwa ni maisha."
Mwenye kufuatilia Aya za Qur'an na Hadith za Mtume, ataona kuwa uislam umeipa kipaumbele mali katika maisha, mpaka kufikia hatua ya kulinganisha sawa na nafsi katika Aya kadhaa; kama vile Aya hii: "Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kutoka kwa waumin nafsi zao na mali zao ili wapate pepo… (9:111)
Hapo Mwenyezi Mungu ameuza pepo yake kwa mali itolewayo kwa ajili yake; sawa na mfanyi biashara anavyouza bidhaa yake kwa ajili ya mali inayotolewa kwa ajili ya maslahi yake. Aya nyingine ni ile isemayo; "Amewafadhilisha Mwenyezi Mungu wanaopigana jihadi kwa mali zao na nafsi zao." (4:95)
Kwa sababu hiyo ndipo mafakih wakasema: "Asili katika kila kitu ni halali mpaka uthibitike uharamu isipokuwa damu tupu na mali, hizo asili yake ni haramu (mpaka uthibitike uhalali)."
Qur'an imetumia neno 'kheri' kwa maana ya mali katika Aya nyingi mfano: "Na hakika yeye kwa sababu ya kupenda mali ni bakhili." (100:8) Hapo mali imetafsiriwa kutoka neon kheri.
Hata baadhi ya wafasiri wamesema kuwa neno kheri limetumika kwa maana ya mali tu katika Qur'an, lakini sisi hatuafikiani na rai hii, ingawaje twajua kuwa Aya nyingi zimeamrisha amali njema, kusaidiana kwa kheri na kujiandaa kwa kujikinga na maadui wa dini na wa nchi , na kwamba haiwezekani kutekelezeka yote isipokuwa kwa mali.
Mwenyezi Mungu amekataza kurundika mali na amewakemea wanaozirundika kwa adhabu kali; kama ambavyo amekataza kufanya israfu na ubadhirifu, na kuwachukulia wabadhirifu kuwa ni ndugu za mashetani, kwa sababu ubakhili na ubadhirifu unakwamisha maendeleo na uzaliishaji unaowafaa watu. Mtume (s.a.w.) amesema: "Mwenyezi Mungu akiitakia nyumba kheri, basi huwaruzuku watu wake wepesi katika maisha na tabia nzuri."
Na Imam Ali (a.s.) amesema: "Mtu hawezi kuonja hakika ya imani, mpaka awe na mambo matatu; Fiqh katika dini, subira katika masaibu na ukadiriaji mzuri katika maisha." Imam ameunganisha imani na utatuzi wa maisha katika dunia hii, kwa sababu ukadiriaji mzuri wa maisha, maana yake ni kufanya kazi vizuri na kutumia mazao ya kazi katika njia yake inayonufaisha.
Hii ni dalili wazi kuwa dini haitengani na maisha; na kwamba imewekwa kwa ajili ya maisha bila ya shaka. Yeyote atakayetenganisha dini na maisha na kuona kuwa ni kiasi cha kuwa ni nembo, ibada na kujinyima starehe tu, basi ama atakuwa ni mjinga aliyechukua dini kutoka kwa wanaoifanyia istihzai, au atakuwa ni mpin- zani wa haki.
Tulipofasiri Aya ya 182 ya sura iliyotangulia (Al-Imran) katika kifungu cha 'matajiri ni mawakala' tulitaja kuwa mali yote ni ya Mwenyezi Mungu na kwamba mtu anaruhusiwa kuitumia mali kwa mipaka maalum, ambayo kama ataikiuka, basi atakuwa amenyang'anya. Hebu rudia kidogo sehemu hiyo, kwani inaambatana na maudhui haya.
Tunaweza kuyarudia kama ikija Aya itakayofungamana nayo na tutafafanua tuliy- oyataja huko na hapa. Kwa sababu fikra haiwezi kukienea kitu kwa pande zake zote isipokuwa inaelekea yote kwenye upande ule unaogusiwa na Aya, mapokezi au tukio lolote.
Na muwakimu katika mali hiyo na muwavishe.
Msemo unaelekezwa kwa wasimamizi wa wabadhirifu. Makusudio ni kuwa wasi- mamizi wawatimizie mahitaji yao ya chakula, nguo, makazi masomo, kuoa n.k. Unaweza kuuliza: Kwa nini amesema 'katika mali hiyo' na wala hakusema kutoka katika mali hiyo?
Jibu: Lau angesema kutoka katika mali hiyo, basi ingelikuwa maana yake ni kuwa atumie asili ya hiyo mali (mtaji). Kwa hiyo ingelipungua au ingelikwisha yote.
Ama kusema: 'Katika mali hiyo' ni kuwa mali iwe ni mtaji wa kutafutia riziki, kwamba msimamzi aizalishe mali hiyo na matumizi ya mbadhirifu yatokane na faida sio mtaji wenyewe.
Swali la pili: Kwa nini amehusisha kivazi; na inajulikana kuwa kivazi ni katika jumla ya kukimu?
Jibu: Amehusisha kivazi kwa kukipa umuhimu. Kwani huenda msimamizi akakipa umuhimu chakula na kughafilika na mavazi. Ndipo Mwenyezi Mungu akaikinga dhana hii kwa kutaja kivazi waziwazi.
Msimamizi wa mbadhirifu ambaye ubadhirifu wake umeanzia utotoni mpaka akakua nao, ni baba, na babu. Ama ikiwa ubadhirifu aliuanzia ukubwani (baada ya kubaleghe), basi msimamizi atakuwa ni kadhi.
Na muwaambie maneno mazuri
Baadhi ya wasimamizi huenda wakaona kuwa ni lazima wale wanaowasimamia wawasikilize na kuwatii, kama mzazi na mtoto wake. Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akazindusha kwa kauli yake hii, ili kila msimamizi amchukulie upole anayemsimamia na kumfanyia mambo yamridhishayo na yanayomtuliza roho yake.
Na wajaribuni mayatima mpaka wafikilie umri wa kuoa. Mkiwaona wana uwekevu, basi wapeni mali zao.
Aya hii inafahamisha kuwa mtoto hapewi mali mpaka awe na sifa mbili: Kubaleghe na kuwa mwekevu. Yamekongamana madhehebu yote ya Kiislam kuwa kutoa manii kunafahamisha kubaleghe; kwa mwanamume na mwanamke, katika umri wowote na hali yoyote; iwe ni usingizini au akiwa macho. Wametoa dalili kwa Aya hii na Aya nyingine isemayo:
"Na watoto miongoni mwenu watakapobaleghe, basi na wapige hodi." (24:59), ambapo limetumika neno 'hulum' lenye maana ya kukomaa mwili kijinsia.
Na imethibiti Hadith kutoka kwa Mtume (s.a.w.) kuwa yeye amesema; "Imeondolewa kalamu (ya kuandika amali) kwa watu watatu: Mtoto mdogo mpaka atoke manii, mwenda wazimu mpaka apone na aliyelala mpaka aamke."
Ama uwekevu unathibiti kwa kupewa yatima mali yake kidogo aitumie. Ikiwa ataitumia vizuri, basi atakuwa ni mwekevu na atapewa mali yake, vyenginevyo atazuiliwa, hata kama atafikisha miaka mia. Abu Hanifa anasema: "Mbadhirifu atapewa mali yake akiwa na miaka 25 (hata kama si mwekevu), "Hashia ibni Abidin J. 5 mlango wa Hajr.
Wala msizile kwa kuzifuja.
Yaani enyi wasimamizi! Msipetuke mipaka mnayoruhusiwa katika kula mali mna- zozisimamia. Kwa sababu msimamizi anaweza kula mali ya anayemsimamia kwa sharti ya kuwa awe fukara; kama itakavyoelezwa.
Na kwa haraka kwa kuwa watakuwa wakubwa.
Msimamizi anaweza kufanya haraka kuitumia mali ya yatima kwa kuhofia asiwe mkubwa akachukua mali yake. Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akakataza matu- mizi hayo ambayo faida yake inamwendea msimamizi, na akazindua kuhusu hatari ya uharamu wake.
Na aliyetajiri, basi na ajizuie; na atakayekuwa fukara, basi ale kwa kiasi cha kawaida.
Msimamizi ama atakuwa mwenye kujitosheleza au fukara. Kwa hiyo mwenye kuji- tosheleza ni lazima ajiepushe kula mali ya yatima na kukinai na riziki ya kutosha aliyopewa na Mwenyezi Mungu. Lakini kama ni fukara, basi inafaa kwake kutumia kiasi cha haja yake ya dharura bila ya kuzidisha.
Kuna Hadith isemayo kuwa Mtume (s.a.w.) aliulizwa na bwana mmoja kuhusu yati- ma akiwa hawezi kutumia mali yake kuwa atakula mali yake?
Akamwambia: "Kula kwa njia ya kawaida," Na imesemekana atakula kwa njia ya mkopo. Lakini dhahiri ya Hadith inaibatilisha kauli hii.
Na mtakapowapa mali zao basi washuhudizeni: na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa mhasibu.
Shia na Hanafi wanasema kuwa si wajibu kwa msimamizi kushuhudiza utoaji wa mali ya anayemsimamia akiwa mwekevu au baleghe. Na amri ya kushuhudiza katika Aya hii, wameichukulia kuwa ni sunna kwa ajili ya kuondosha tuhuma na kujiepusha na uhasama.
Shafii na Malik wamesema kuwa ni wajibu na wala sio sunna kwa kuchukulia dhahiri ya Aya hii.
لِلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنْهُ أَوْ كَثُرَ ۚ نَصِيبًا مَفْرُوضًا {7}
وَإِذَا حَضَرَ الْقِسْمَةَ أُولُو الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينُ فَارْزُقُوهُمْ مِنْهُ وَقُولُوا لَهُمْ قَوْلًا مَعْرُوفًا {8}
وَلْيَخْشَ الَّذِينَ لَوْ تَرَكُوا مِنْ خَلْفِهِمْ ذُرِّيَّةً ضِعَافًا خَافُوا عَلَيْهِمْ فَلْيَتَّقُوا اللَّهَ وَلْيَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا {9}
إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا {10}