read

Aya 19 – 21: Tangamaneni Nao Kwa Wema

Maana

Enyi ambao mmeamini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu.

Dhahiri ya Aya inaonyesha kukataza kuwachukulia wanawake kama wanyama na kuwarithi, kama walivyokuwa wakifanya wakati wa ujahiliya. Walikuwa wakimuhis- abu mwanamke kuwa ni katika jumla ya mali ya mirathi aliyoacha marehemu.

Mtu akifa msimamzi wa mali zake huja kumtupia nguo mjane, na kumchukua kwa hiyo nguo kama anavyochukua mateka au nyara. Akipenda anamuoa au amwoze mume mwengine na yeye (msimamizi) achukue mahari; kama anayeuza bidhaa na kuchukua pesa. Au akipenda anaweze kumfunga nyumbani mpaka ajikomboe kwa kitu atakacho kikubali.

Imesemekana kuwa makusudio sio kama ilivyo dhahiri ya Aya na kwamba kuna maneno yaliyokadiriwa kuwa ni msirithi mali za wanawake kwa nguvu. Na mfano wa kurithi kwa nguvu ni kuwa mwanamke na msimamizi wake wa karibu kama kaka; mwanamke akawa na mali na kaka yake akamzuwia kuolewa kwa kuwa na tamaa ya kumrithi.

Kwa sababu akiolewa atarithiwa na mumewe na wanawe. Ndipo uislam ukaamrisha kumpa mwanamke uhuru wa kuolewa na kukataza kumzuia kwa tamko la kumrithi kwa nguvu. Kwa sababu kurithi ndio makusuido na lengo; na kuzuwia kuolewa ni sababu tu.

Sisi hatuoni tatizo kwa atakayechagua tafisiri ya kwanza au ya pili, au zote pamo- ja, maadamu uislam unakataza kumchukulia mwanamke kama bidhaa, na unam- pa uhuru katika kuolewa na kuchagua mume.

Wala msiwataabishe kwa kutaka kuwanyang'anya baadhi ya mlivyowapa.

Kama ambavyo si halali kwa mwanamume kummiliki mwanamke kama mnyama au kumzuilia kuolewa, vile vile si halali kwa mume kumfanyia uovu mkewe kwa kukusudia kuwa atoe mali ili ajikomboe. Ikiwa mke atatoa katika hali hii na mume akachukua mali, basi atakuwa ni mwenye dhambi. Kwa sababu mali ya mtu hai- wezi kuwa halali (kwa mwengine) isipokuwa kwa kuridhika mwenyewe.

Hata hivyo ikibainika kuwa amefanya zina itajuzu katika hali hii kumpa dhiki mpaka atoe kitakachomridhisha, kutokana na kauli yake: "Ila watakapofanya uchafu ulio wazi."

Makusudio ya uchafu hapa ni zina. Kundi dogo la wanavyuoni limesema kuwa uchafu unakusanya pia unashiza1Mwenye Bahrul-muhita amenakili kutoka kwa Malik kwamba inafaa kwa mume kumdhikisha mkewe aliye nashiza na kumchukulia kila anachomiliki, Sheikh Muhammad Abduh anasema:.Uchafu ni pamoja na zina, unashiza, wizi na mengineyo katika mambo yaliyoharamishwa.

Tuonavyo sisi ni kuwa si halali kumdhikisha mke kwa ajili ya mali ila akiwa amezi- ni. Na ni haramu kumfanyia hivyo katika isiyokuwa zina, vyovyote itakavyokuwa dhambi; kwa kuangalia maana ya yakini yaliyokusudiwa na Aya.

Zaidi ya hayo kufanyika dhambi hakuhalalishi kula mali za wanayofanya dhambi. Kama si hivyo utaratibu ungeharibika na mambo yangekuwa sambe jambe. Ni nani atakayekuwa na uhalali wa kula mali ya mwenye dhambi? Je, ni mwenye dhambi kama yeye au asiyefanya (mwenye kuhifadhiwa na) dhambi? Ikiwa ni mwenye dhambi kama yeye basi vipi atahalalisha mali ya mwengine; na kama atakayechukua ni maasum basi yuko wapi?

Kwa hakika ni kwamba haijuzu kwa Kadhi kuhukumu kufuta mahari ya mke aliyethibitikiwa na zina kwa sababu ruhusa ya kumdhikisha na kuchukua kitu ina- muhusu mume tu., ni kati yake yeye na Mola wake. Na kwa ibara ya mafakihi, Inajuzu kuchukua mahari katika mfano wa hali kwa ridhaa hii sio kwa kulipa.

Mtaka Yote, Hukosa Yote

Na kama mkiwachukia, basi huenda mkachukia kitu na Mwenyezi Mungu amejaalia heri nyingi ndani yake.

Huenda mtu akachukia baadhi ya mambo ya mkewe, asivumilie, akamwacha na kuoa mke mwengine. Mara huyu mke mwengine anakuwa mbaya zaidi na mwenye vitendo viovu kuliko yule wa kwanza. Hapo hujuta tena, ambapo hakufai chochote. Kwenye kitabu Aghani anasema: Farazdaq alimwacha Nawal, kisha akaoa mwanamke mwengine aliyeachwa, akajuta. Ikawa anamsikia akipiga kite na kumlilia mumewe wa kwanza. Basi akatunga shairi hili;

Mumewe wa kwanza amlilia, nami wangu wa kwanza namlilia.

Nimewaona wengi ambao huwa hawana chochote, mtu hamiliki hata chakula chake anaishi kwa kuombaomba tu, Mara anapata kazi inayomsaidia maisha yake na kutekeleza haja zake kiasi cha kutomtegemea mwengine, kisha huikataa kazi hiyo kwa kutaka zaidi. Basi Mwenyezi Mungu humtia adabu kwa kupata hali mbaya zaidi. Hapo hujuta tena ambako hakumfai chochote. Kuna methali maarufu isemayo; 'Mtaka yote hukosa yote.'

Vile vile tumeona wengi wenye shahada za juu lakini wakakubali kazi ile wanay- opata wakawa makarani tu au chini ya karani; wakangoja fursa wakimtegemea Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Si baadae sana mara hupanda kidogo kidogo mpaka kufikia cheo cha juu. Kuna Hadith isemayo: 'Kukinai ni miliki isiyotoweka na ni hazina isiyokwisha …'

Maana yake ni kuwa mwenye kutosheka na apatacho na wala asidharau alichonacho au kutaka asicho nacho, basi yeye daima ni sawa na aliyenacho (mwenye hazina isiyoisha daima).

Na mtakapotaka kubadilisha mke mahali pa mke, na mkawa mumempa mmoja wao rundo la mali, basi msichukue katika mlichowapa.

Maana yako wazi na yanafupilizwa na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Muwaache muacho mzuri." (33:49) Kuachana kuzuri ni kutoa talaka pamoja na kutekeleza haki zake zote.

Baadhi ya wafasiri wanasema, kuwa wanavyuoni wametofautiana kufikia kauli kumi katika kuweka kiwango maalum cha mrundo wa mali kwa usahihi ni kuwa hilo ni fumbo la wingi. Na kisa cha mwanamke aliyempinga Umar bin Al-khattab - wakati alipotaka kumwekea kiwango cha mahari - kwa Aya hii, ni mashuhuri haki- na haja ya kukitaja.

Je, mnakichukua kwa dhulma na kwa makosa yaliyo wazi?

Yaani mnanyang'anya kwa batili na dhuluma. Unaweza kuuliza: Kwa nini Mwenyezi Mungu amehusisha kukataza kunyang'anya mali ya mke katika hali ya kutaka kubadilisha ambapo tunajua kuwa kunyang'anya ni haram, ni sawa kuwe ni kwa kutaka kubadilisha au la.
Jibu: Hakuna mwenye shaka kuwa kunyang'anya kokote ni haramu huenda ikawa hekima ya kuhusisha kutaja kubadilisha ni kuwa mume anaweza akadhani kuwa anaruhusiwa kuchukua mahari ya mke ikiwa anataka kubadilisha mke mwengine, kwa vile mke mwengine anachukua nafasi ya yule wa kwanza na kuwa itakuwa uzito kwake kutoa mahari mara mbili, Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akaondoa dhana hii, kwa kutaja kutaka kubadilisha.

Mtakichukuaje na hali mmeingiliana.

Baadhi ya wafasiri wamesema makusudio ya kuingiliana hapa ni kujamiiana tu. Wengine wamesema pia na faragha.

Kundi jingine la tatu limesema kwa kuya- pamba meneno: "Makusudio ya kuingiliana ni mapenzi, hisia, mawazo, siri, huzuni, majibizano, makumbusho na simanzi .." Na sifa nyinginezo zilizopangwa.

Mungu awarehemu! Tafsiri nzuri ya maana ya kuingiliana ni ile aliyoisema Sheikh Muhammad Abduh aliposema: "Ni ishara ya kwamba kila mmoja kati ya mume na mke ni sehemu inayotimiza sehemu nyengine; ni kama kwamba ilikuwa sehemu moja imetenganishwa na sehemu nyingine halafu ikaunganishwa kwa mwingiliano huu na kuwa moja."

Lakini ni bora zaidi tufasiri maingiliano kwa maana ya kufanyiana hisani, kwa kufu- ata kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala msisahau hisani baina yenu." (2:237)

Yaani hisani ya kila mmoja kwa mwengine, mke na mume. Mwenyezi Mungu anamkubusha mume yale yaliyokuwepo kati yake na mkewe.

Ndoa Ni Kubadilishana Roho Kwa Roho

Na hali wao wamechukua kwenu agano madhubuti.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekupangia kufunga ndoa kwa matamko aliyoyataja katika kitabu chake kitukufu na kuwajibisha kuyatumia hayo tu; sawa na matamko ya ibada, na akakuongezea huko kufunga ndoa, utukufu ambao hauko katika mapatano mengine; kama vile bei, ajira n.k.

Kwa sababu bei ni kubadilishana mali kwa mali. Ama ndoa ni kubadilishana roho kwa roho na akayafanya ni mapatano ya rehema na mapenzi sio mapatano ya kumiliki mwili badala ya mali.

Mafakihi wamesema: "Kufunga ndoa ni karibu zaidi na ibada kuliko mapatano mengine; na ni kwa sababu hii, ndipo wakaitegemeza kwenye jina la Mwenyezi Mungu Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kwa sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu."

Sheikh Muhammad Shaltut anasema: "Kama tukijua kuwa neno Mithaq' (agano) limekuja katika Qur'an kwenye ibara za mambo yaliyo baina ya Mwenyezi Mungu na waja wake katika wajibu wa Tawhid, na kulazimiana na hukumu, vile vile katika mambo hatari ya dola moja na nyengine tu, basi hapa tutajua cheo cha kutaja hilo neno katika kufunga ndoa.

Vile vile kama tukijua kuwa kulisifu neno Mithaq kwa neno Ghalidh (madhubuti) hakuna katika Qur'an isipokuwa katika maudhui ya ndoa tu, basi utazidi utukufu wa jambo hili ambao umeletwa na Qur'an."

وَلَا تَنْكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُمْ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۚ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَمَقْتًا وَسَاءَ سَبِيلًا {22}

Wala msiwaoe walioolewa na baba zenu, ila waliokwisha pita. Hakika hilo ni ovu na chukizo na njia mbaya.

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ مِنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُمْ مِنْ نِسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُمْ بِهِنَّ فَإِنْ لَمْ تَكُونُوا دَخَلْتُمْ بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَنْ تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَحِيمًا {23}

Mmeharamishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu na shangazi zenu na khalat zenu, na binti wa kaka na binti wa dada, na mama zenu waliowanyonyesha na dada zenu wa kunyoyonya, na mama wa wake zenu na binti zenu wa kambo walio katika ulinzi wenu, waliozaliwa na wake zenu mliowaingilia-hapana vibaya juu yenu ikiwa hamkuwaingiliana wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu, na kukusanya kati ya dada wawili, ila waliokwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusameh Mwenye kurehemu.
  • 1. Kutoka mke kwenye twaa ya mume