Aya 11 – 17: Umetufisha Mara Mbili Na Umetuhuisha Mara Mbili
Maana:
Watasema: Mola wetu! Umetufisha mara mbili, na umetuhuisha mara mbili! Basi tunakiri madhambi yetu. Basi je, ipo njia ya kutoka?
Watakaosema hivyo ni watu wa motoni. Mauti ya kwanza ni kabla ya kuto- ka matumboni mwa mama zao na ya pili ni haya mauti yaliyozoeleka. Uhai wao wa kwanza ni uhai wa duniani na wa pili ni wa ufufuo baada ya mauti.
Maana ni kuwa watu wa Jahannam, wakiwa katikati ya moto wakiadhibi- wa, watamnyenyekea Mwenyezi Mungu huku wakisema: Ewe Mola wetu! Wewe ni muweza wa kila kitu. Ulituleta duniani, ukatutoa kwenye mauti, kisha ukatufufua baada yake.
Hivi sasa tuko mbele yako tukijuta na kukiri makosa na dhambi zetu. Je, kuna njia yoyote, kutokana na karama yako, kutuwezesha kutoka motoni, tukikuahidi utiifu na kufuata amri?
Hayo ni kwa sababu alipoombwa Mwenyezi Mungu peke yake mlikataa. Na akishirikishwa mnaamini.
Hili ni jawabu la kauli yao ‘Je, ipo njia ya kutokea?’ Ufupisho wa jawabu ni kuwa mlinganiaji haki aliwapa mwito wa haki, duniani, mkaukataa. Na mlinganiaji shetani aliwapa mwito mkaukubali. Hivi sasa mnaita hamtajibiwa.
Kauli yake Mwenyezi Mungu: Basi hukumu ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Mkubwa, inaashiria kuwa kesho hukumu ni ya Mwenyezi Mungu tu peke yake, hakuna mkubwa isipokuwa Yeye tu:
وَعَنَتِ الْوُجُوهُ لِلْحَيِّ الْقَيُّومِ ۖ وَقَدْ خَابَ مَنْ حَمَلَ ظُلْمًا {111}
Yeye ndiye ambaye anawaonyesha Ishara zake, na anawateremshia riziki kutoka mbinguni. Na hapana anayekumbuka ila anayerejea.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametuonyesha ushahidi mwingi juu ya kuweko kwake, utukufu wake, dalili za upangiliaji wake na hekima yake katika mbingu, ardhi, watu, wanyama na hata katika mvua na mimea na mengingineyo yasiyokuwa na ukomo.
Ilivyo ni kuwa dalili hizi, pamoja na wingi wake, hazijitokezi ila kwa mwenye busara na kufikiria, lakini mpofu wa moyo hayaoni hayo. Anasema Tagore:
“Hakika Mwenyezi Mungu anadhihirisha kuweko kwake katika mfumo hai wa sura mbali mbali za maumbile. Ameudhihirisha kwenye mfumo ulioko baina ya nguvu za maumbile zinazopambana katika umoja wao kwenye kanuni iliyopangiliwa isiyoepukika, wakati huo huo zikielekea kuhakikisha malengo. Kila kitu katika maumbile kina wadhifa wake maalum na malengo maulumu yaliyopangiliwa. Mbegu inafanya kazi kwa bidii ili itoe mti, mti nao unajitihidi ili utoe mau na maua nayo yana kazi ya kutoa tunda. Haya hawezi kuyatambua isipokuwa mwenye moyo ulio salama.”
Makusudio ya mwenye moyo salama ndio yale hasa yaliyokusudiwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na hapana anayekumbuka ila anayerejea.’
Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye, wajapochukia makafiri.
Wanaambiwa waumini. Makusudio ya kuomba hapa ni ibada na dini ni utiifu. Maana ni kuwa mwabuduni Mwenyezi Mungu peke yake na mumtii katika amri zake na makatazo yake, wala msijali lawama. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewasahilishia waja wake njia ya kumtii, pale alipowaongoza akiwahadharisha, akawakalifisha kwa wepesi; na hakumwachia udhuru mwenye kutafuta visababu.
Ndiye Mwenye daraja za juu.
Hiki ni kinaya cha utukufu wake. Imesemekana kuwa Makusudio ya daraja hapa ni tofauti ya wanaomojua Mungu katika maarifa yao.
Kuanzia maarifa ya mtu wa kawaida hadi maarifa ya wanafilosofia na manabii.
Mwenye Arshi.
Ni kinaya cha umiliki na utawala.
Hupeleka Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake, ili kuonya Siku ya kukutana.
Makusdio ya roho hapa ni wahyi. Siku ya kukutana ni Siku ya Kiyama ambapo kila mtu atakutana na malipo ya amali yake. Na makusudio ya kuonya siku hii ni kuonya adhabu. Imekuja ibara ya kuwa Yeye Mwenyezi Mungu ndiye muonyaji, kutokana na ukali na vituko vya siku hiyo.
Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamteremshia wahyi anayemtaka katika waja wake, ili awaonye watu, kwamba wao watafufuliwa baada ya mauti, katika siku ambayo itakuwa mbaya kwa wenye kuvuka mipaka na waasi na kuulizwa yale waliyokuwa wakiyafanya.
Siku watakayodhihiri wao.
Yaani itadhihiri hakika yao.
Hapana kitachofichikana chochote chao kwa Mwenyezi Mungu.
Huu ni ubainfu wa kauli ya: ‘Siku watakayodhihiri.’
Ufalme ni wa nani leo?
Wataulizwa siku ya kiyama, wakiwa wametokeza kwa ajili ya hukumu: amri na hukumu ni ya nani? Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atawajibia, kwa sababu jawabu liko wazi.
Au wao wenyewe watajibu kihali na kimaneno kuwa: Ni wa Mwenyezi Mungu Mmoja Mtenza nguvu waja.
Leo kila nafsi italipwa kwa iliyoyachuma. Hapana dhulma leo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
Ayahiiikowazi,naimetanguliakatikaJuz.13(14:51).
وَأَنْذِرْهُمْ يَوْمَ الْآزِفَةِ إِذِ الْقُلُوبُ لَدَى الْحَنَاجِرِ كَاظِمِينَ ۚ مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ {18}
يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ {19}
وَاللَّهُ يَقْضِي بِالْحَقِّ ۖ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِنْ دُونِهِ لَا يَقْضُونَ بِشَيْءٍ ۗ إِنَّ اللَّهَ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ {20}
أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ كَانُوا مِنْ قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا هُمْ أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَآثَارًا فِي الْأَرْضِ فَأَخَذَهُمُ اللَّهُ بِذُنُوبِهِمْ وَمَا كَانَ لَهُمْ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَاقٍ {21}
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانَتْ تَأْتِيهِمْ رُسُلُهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ فَكَفَرُوا فَأَخَذَهُمُ اللَّهُ ۚ إِنَّهُ قَوِيٌّ شَدِيدُ الْعِقَابِ {22}