Je, Mwenyezi Mungu Si Wa Kumtoshea Mja Wake? Aya 32 – 37
Maana
Basi ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uwongo Mwenyezi Mungu, akamfanyia washirika au mtoto?
Kauli mbaya zaidi ni uwongo na uwongo mbaya zaidi ni kumzulia Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Na kuikadhibisha kweli imfikiapo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia ulimi wa Mtume wake.
Hivi ndivyo walivyo watu wa masilahi na manufaa, mahali popote na wakati wowote, wanaukana ukweli na kuusadikisha uwongo. Kwa sababu masilahi yao yanakuwa kwa uzushi na ubatilifu. Miongoni mwa niliyoyasoma kuhusiana na haya ni kuwa uwongo mkubwa zaidi ni kusema mwongo: “Mwenyezi Mungu anajua kuwa mimi ni mkweli.”
Je! Siyo katika Jahannamu makazi ya makafiri? Bila shaka ndio makazi yao na makazi ya kila taghuti muovu.
Na aliyeleta ukweli na aliyeusadikisha, hao ndio wenye takua.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikuja na ukweli kutoka kwa Mwenyezi Mungu na waislamu wakausadikihsa. Hao mbele ya Mwenyezi Mungu ndio watu wema ikiwa watayaogopa aliyoyakataza; vinginevyo kusadikisha bila matendo hakuna maana yoyote.
Watapata watakachotaka kwa Mola wao. Hayo ndiyo malipo ya watendao mema.
Yaani wale wanaogopa aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu. Kwa sababu bado mazungumzo yanawahusu wao. Mwenyezi Mungu hakuanisha malipo, bali amewaachia vile watakavyo.
Ili Mwenyezi Mungu awafutie uovu zaidi walioufanya na awalipe ujira wao kwa wema zaidi ya waliokuwa wakiufanya.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasamehe madhambi yote, makubwa na madogo, kwa yule mwenye kutubia, akaamini na akatenda mema; na atawalipa wale wanaomtii na kushukuru neema zake kwa wema mkubwa kuliko vile walivyokuwa wakitii na kushukuru.
Je! Mwenyezi Mungu si wa kumtoshea mja wake? Na wanakutishia kwa wasio kuwa Yeye!
Makusudio ya mja wake hapa ni Muhammad (s.a.w.). Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamkinga na shari ya anayemkusudia shari. Makusudio ya wale wasiokuwa yeye ni masanamu. Kundi la wafasiri wamesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alipoyataja masanamu kwa ubaya, makuraishi walisema: Muhammad asipokoma kuwataja vibaya miungu wetu, basi tutamshtakia kwao apatwe na majanga.”
Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii. Hili haliko mbali na akili za wajinga na wapumbavu. Hakuna mwenye shaka kuwa Mwenyezi Mungu anamtoshea na kumkinga mja wake na mtume wake.
Na anayepotezwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumwongoza. Na anayeongozwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumpoteza.
Wakati tukifasiri Aya ya 23 ya Sura hii tuliyo nayo, kwenye Juz. 23, na kwengineko, tulisema kuwa Mwenyezi Mungu, anampoteza yule mwenye kufuata njia ya upotevu kwa hiyari yake, na anamwongoza mwenye kuchagua uongofu kwa hiyari yake na akafuata njia yake.
Je! Mwenyezi Mungu si Mwenye nguvu anayeweza kulipiza anayekufuru na akadhukumu kwa hiyari yake tena baada ya kupewa hoja?
وَلَئِنْ سَأَلْتَهُمْ مَنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّهُ ۚ قُلْ أَفَرَأَيْتُمْ مَا تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ إِنْ أَرَادَنِيَ اللَّهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ أَوْ أَرَادَنِي بِرَحْمَةٍ هَلْ هُنَّ مُمْسِكَاتُ رَحْمَتِهِ ۚ قُلْ حَسْبِيَ اللَّهُ ۖ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ الْمُتَوَكِّلُونَ {38}
قُلْ يَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ {39}
مَنْ يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ مُقِيمٌ {40}
إِنَّا أَنْزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ لِلنَّاسِ بِالْحَقِّ ۖ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا ۖ وَمَا أَنْتَ عَلَيْهِمْ بِوَكِيلٍ {41}
اللَّهُ يَتَوَفَّى الْأَنْفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا ۖ فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَىٰ عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَىٰ إِلَىٰ أَجَلٍ مُسَمًّى ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ {42}
أَمِ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ شُفَعَاءَ ۚ قُلْ أَوَلَوْ كَانُوا لَا يَمْلِكُونَ شَيْئًا وَلَا يَعْقِلُونَ {43}
قُلْ لِلَّهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا ۖ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ {44}
وَإِذَا ذُكِرَ اللَّهُ وَحْدَهُ اشْمَأَزَّتْ قُلُوبُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ ۖ وَإِذَا ذُكِرَ الَّذِينَ مِنْ دُونِهِ إِذَا هُمْ يَسْتَبْشِرُونَ {45}