read

Sura Ya Arubaini Na Mmoja: Fussilat

Imeshuka Makka, ina Aya 54

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

حم {1}

Haa Mim.

تَنْزِيلٌ مِنَ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ {2}

Ni uteremsho kutoka kwa Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

كِتَابٌ فُصِّلَتْ آيَاتُهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ {3}

Ni Kitabu kilichopambanuliwa Aya zake. Qur’an ya Kiarabu kwa watu wanaojua.

بَشِيرًا وَنَذِيرًا فَأَعْرَضَ أَكْثَرُهُمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ {4}

Inayotoa bishara, na inayoonya. Lakini wengi wao wamepuuza; kwa hiyo hawasikii.

وَقَالُوا قُلُوبُنَا فِي أَكِنَّةٍ مِمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ وَفِي آذَانِنَا وَقْرٌ وَمِنْ بَيْنِنَا وَبَيْنِكَ حِجَابٌ فَاعْمَلْ إِنَّنَا عَامِلُونَ {5}

Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayotuitia, na masikio yetu yana uziwi, na baina yetu na wewe kuna pazia. Basi wewe tenda, nasi tunatenda.

قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ فَاسْتَقِيمُوا إِلَيْهِ وَاسْتَغْفِرُوهُ ۗ وَوَيْلٌ لِلْمُشْرِكِينَ {6}

Sema: Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; ninapewa wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na mumtake maghufira. Na ole wao wanaomshirikisha.

الَّذِينَ لَا يُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ {7}

Ambao hawatoi Zaka nao ndio wanaoikataa Akhera

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ {8}

Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema watakuwa na ujira usiosimbuliwa.