Aya 87 – 88: Msiharamishe Vizuri
Maana
Enyi mlioamini! Msiharamishe vizuri alivyowahalalishia Mwenyezi Mungu.
Wamesema kuwa Aya hii imeshuka kwa Masahaba waliokuwa na hofu sana na Mwenyezi Mungu wakajiharamishia wanawake, vyakula vizuri na mavazi. Wakawa wanaswali usiku na kufunga mchana. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akawaita na kuwasomea Aya hii, akasema: Ama mimi ninaswali usiku na ninalala, ninafunga na ninafungua na ninawaendea wanawake. Basi atakayejiepusha na mwenendo wangu si katika mimi."
Na kauli yake Mwenyezi Mungu. Wala msipetuke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wapetukao mipaka, inafahamisha kuwa kuharamisha halali ni sawa na kuhalalisha haramu, yote mawili ni dhulma na ukiukaji mipaka.
Na kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu vilivyo halali na vizuri. Imetangulia tafsir yake katika Juz.2 (2:168)
لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَٰكِنْ يُؤَاخِذُكُمْ بِمَا عَقَّدْتُمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ {89}