read

Aya 93: Wenye Takua Na Kuamini

Maana

Wafasiri wameafikiana kwamba iliposhuka Aya ya kuharamisha pombe, baadhi ya Masahaba walimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): Itakuwaje kwa ndugu zetu waliokufa wakiwa wanywaji?

Ndipo ikashuka Aya hii ambayo kwa ujumla inafahamisha kuwa mwenye kunywa pombe kabla ya kubainishwa hukumu yake, hapana vibaya juu yake ikiwa ni katika waumini wanaomcha Mungu. Kuanzia hapa ndipo mafakihi wakaafikiana kwamba kila kitu ni halali mpaka kikatazwe.

Baada ya kuafikiana wafasiri kuwa maana haya ndiyo makusudio katika Aya walihitalifiana katika sababu zinazowajibisha kukaririka takua mara tatu; ambapo mara ya kwanza kumetajwa, pamoja na Imani na amali njema, mara ya pili pamoja na Imani tu na mara ya tatu pamoja na uzuri.

Razi amenukuu, katika hilo, kauli tano. Mwenye Majmaul-bayan akasema: Makusudio ya takua ya kwanza ni kuacha kunywa pombe baada ya kuharamishwa; ya pili ni kudumu juu ya hilo na ya tatu ni kuacha maasi yote pamoja na kufanya mema.

Mmoja wa wafasiri wapya anasema: “Nafsi yangu bado haijatulia na chochote katika tafsir hii; wala Mwenyezi Mungu hajanifungulia chochote.

Tunavyofikiria sisi - Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi - ni kwamba lengo la kukaririka huku ni kubainisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwamba mwenye takua ya kweli ni yule anayemcha Mwenyezi Mungu katika hali zake zote, ujana, uzee na ukongwe, na katika dhiki na faraja.

Na kwamba mwenye kufa juu ya hilo basi yuko katika amani na usalama.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَيَبْلُوَنَّكُمُ اللَّهُ بِشَيْءٍ مِنَ الصَّيْدِ تَنَالُهُ أَيْدِيكُمْ وَرِمَاحُكُمْ لِيَعْلَمَ اللَّهُ مَنْ يَخَافُهُ بِالْغَيْبِ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ {94}


Eny


i


mlioamini


!


Hakika Mwenyez


i



Mung


u


atawa


jaribu kwa baadhi ya mawindo yatakayofikiwa na mikono


yen


u


n


a


mikuk


i


yenu


,


ili


Mwenyezi Mungu amjue ni


nan


i


anayemwogop


a


kwa ghaibu


.


Bas


i


atakayeruka


mipaka baada ya hayo, atapata



adhabu



iumizayo.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنْتُمْ حُرُمٌ ۚ وَمَنْ قَتَلَهُ مِنْكُمْ مُتَعَمِّدًا فَجَزَاءٌ مِثْلُ مَا قَتَلَ مِنَ النَّعَمِ يَحْكُمُ بِهِ ذَوَا عَدْلٍ مِنْكُمْ هَدْيًا بَالِغَ الْكَعْبَةِ أَوْ كَفَّارَةٌ طَعَامُ مَسَاكِينَ أَوْ عَدْلُ ذَٰلِكَ صِيَامًا لِيَذُوقَ وَبَالَ أَمْرِهِ ۗ عَفَا اللَّهُ عَمَّا سَلَفَ ۚ وَمَنْ عَادَ فَيَنْتَقِمُ اللَّهُ مِنْهُ ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ ذُو انْتِقَامٍ {95}


Enyi Mlioamini! Msiue windo na hali mko katika Ihram.



Na miongoni mwenu atakayemuua kwa kusudi, basi malipo (yake) yatakuwa ni mfano wa aliyemuua katika wanyama wa kufugwa, kama watavyohukumu waadilifu wawili



miongoni mwenu, mnyama apelekwe Al-kaaba (kama sadaka); au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini;



au



badala



ya



hayo ni kufunga; ili



aonje ubaya wa jambo lake. Mwenyezi Mungu amekwisha yasamehe yaliyopita; na atakayerudia, Mwenyezi Mungu atampa adhabu;



na



Mwenyezi



Mungu ndiye



mwenye



nguvu



mwenye kuadhibu.

أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ مَتَاعًا لَكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ الْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا ۗ وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ {96}


Mmehalalishiw


a


kuvua


baharini na chakula chake, kwa



manufaa



yenu na kwa wasafiri.



Na mmeharamishiwa kuwinda bara maadamu


mk


o


katik


a


Ihram


.


Na mchen


i


Mwenyez


i


Mungu


ambaye kwake mtakusanywa.