read

Aya 20 – 24: Wanamfahamu Kama Wanavyo Wafahamu Wana Wao

Maana

Wale tuliowapa Kitab wanamjua kama wanavyowajua wana wao.

Waliopewa Kitab ni Mayahudi na Wakristo. Dhamiri ya wanamjua inamrudia Muhammad (s.a.w.). Aya hii inawakabili maulama wa watu wa Kitab kwamba wao wanamjua vizuri Mtume wa mwisho, kama wanavyowajua wana wao, lakini wao wanaficha yale wanayoyajua. Maana haya yamekaririka katika Aya kadhaa, zikiwemo hizi zifuatazo:

\الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِنْدَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيلِ{157}


“Ambao wanamfuata Nabii asiyesoma wala kuandika ambaye wanam- wona



ameandikwa



kwao



katika



T


awrat



na



Injil”



(7:157)

أَوَلَمْ يَكُنْ لَهُمْ آيَةً أَنْ يَعْلَمَهُ عُلَمَاءُ بَنِي إِسْرَائِيلَ {197}


Je,



haikuwa



ishara



kwao



kwamba



wanayajua



haya



maulama



wa



wana



wa Israil? (26:197)

Yamekwishapita maelezo kwa ufafanuzi katika Juz. 2 (2:146) na Juz. 4 (4:164). Si lazima kwa watu wa Kitab, katika kuujua ukweli wa Muhammad (s.a.w.), wakute jina lake limeandikwa kwao katika Tawrat na Injil. Kila mwenye kuusoma Uislamu kwa somo sawa sawa na upekuzi, ataamini kwa imani isiyokuwa na tashwishi yoyote kwamba Uislamu ni haki na ukweli.

Na mawili hayo (haki na ukweli) ndiyo johari za Uislamu, nguzo yake na lengo lake kutokana na neno Lailaha illa Ilah (Hakuna Mungu isipokuwa Allah) ambalo linamaanisha usawa baina ya watu, kumpa mtu msimamo wa misingi ya kufanya amali na ikhlasi na wala sio kwa misingi ya mali, jaha na nasabu. Na vilevile mshikamano na majukumu ya kila kiongozi kwa wachini wake katika mwito wa amani na usalama, maendeleo na utulivu usiokuwa na mwisho.

Wale ambao wamezitia hasarani nafsi zao hawaamini.

Imepita, punde tu Tafsir yake katika Aya 12 ya Sura hii.

Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule amzuliaye Mwenyezi Mungu uwongo.

Makusudio ya dhulma hapa ni Ukafiri. Kwa sababu kila anayemzulia Mwenyezi Mungu uwongo, basi yeye ni kafiri. Hakuna tofauti yoyote baina ya anayemshirikisha na yule mwenye kugeuza hukumu yoyote katika hukumu zake kwa makusudi na kujua; na yule mwenye kudai unaibu wa maasum au kuwaombea viumbe haki, na hali anajua kuwa yeye ni mzushi na mwongo. Wote hawa ni makafiri waovu kwa Ijmai (kongamano), Kitab na Hadith.

Au azikadhibishaye ishara zake? Hakika madhalimu hawatafaulu.

Jumla iliyotangulia imeashiria yule anayeleta yasiyokuwepo; kama mwenye kumfanyia Mwenyezi Mungu washirika au mtoto. Na jumla hii inaashiria yule mwenye kukanusha vilivyopo, kama vile anayemkana Mwenyezi Mungu kabisa. Hukumu ya wote wawili ni moja, kila mmoja wao ni dhalimu:

مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ {18}


“Madhalimu



hawana



rafiki



mpenzi



wala



muombezi



anayetiiwa”



(40:18)

“Na siku tutakapowakusanya wote, kisha tutawaambia wale walioshirikisha: Wako wapi washirikishwa wenu mliokuwa mnadai.”

Wanaomwamini Mwenyezi Mungu wako aina mbili: Kuna wale wanaoamini uungu wake na kuwa ni mmoja tu. Hawa wanaitwa wanaompwekesha Mungu (watu wa Tawhid).

Na kuna wale wanaoamini uungu wake na uungu mwingine. Hawa ndio wale walioharibu imani yao kwa mchanganyiko huu; na wakawa sawa na wale wanaomkana Mwenyezi Mungu. Kwa sababu kumjaalia Mwenyezi Mungu mfano maana yake hasa ni kumkana Mwenyezi Mungu kabisa. Kwani ilivyo nikuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) hana mshabaha wala mfano:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ {11}


“Hakuna



kama



mfano



wake



kitu



chochote.”



(42:


1


1)

Mwenyezi Mungu atawakabili washirikina na swali hili (wako wapi washirikishwa mliokuwa mnadai na mkiwataka msaada, kama mnavyomtaka msaada Mwenyezi Mungu) kwa njia ya kutahayariza na kukarip- ia, na wala sio kwa njia ya kuhakikisha.

Unaweza kuuliza, kwa nini Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema wako wapi washirikishwa wenu na wala hakusema wako wapi washirikishwa wangu, pamoja na kuwa makafiri ndiyo waliosema kuwa Mungu ana washirika na sio wao?

Jibu: Ni kwa kuwa wao ndiyo wako karibu zaidi na mnasaba huo; kwani wao ndio waliozusha ushirikina ambao hauna athari kabisa.

Kisha hautakuwa udhuru wao ila kusema Wallahi, Mola wetu! Hatukuwa washirikina.

Makusudio ya udhuru wao ni udhuru wao wa kushirikisha na kuabudu mizimu. Maana ni kuwa mwisho wa ushirikina waliozusha ni kiapo chao cha uovu kwamba wao hawakuwa washirikina.

Unaweza kuuliza: Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwasimulia watu hao: ‘Wallahi Mola wetu! Hatukuwa washirikina’ inapingana na kauli yake yake.

“Wala hawatamficha Mwenyezi Mungu na mazungumzo (yao)” (4:42) Zaidi ya hayo ni kuwa inajulikana kuwa mtu hawezi kusema uongo Siku ya Kiyama.

Jibu: Katika Kiyama kutakuwa na vituo kadhaa, baadhi yake mtu ataweza kukana na ambapo katika kituo hicho miguu yake na mikono yake haitam- tolea ushahidi wa yale aliyokuwa akiyafanya.

Kwenye kituo hicho ndipo huchukuliwa kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Wallahi Mola wetu! Hatukuwa washirikina.’ Na katika kituo kingine, atakiri ambapo hapatakuwa na nafasi ya kukana. Hapo ndipo huchukuliwa kauli yake Mwenyezi Mungu: “Wala hawataweza kumficha Mwenyei Mungu neno lolote”

Ama kauli ya kuwa mtu atashindwa kabisa kusema uwongo siku ya Kiyama,inakanushwanaAyaisemayo:

يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ اللَّهُ جَمِيعًا فَيَحْلِفُونَ لَهُ كَمَا يَحْلِفُونَ لَكُمْ ۖ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ عَلَىٰ شَيْءٍ ۚ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْكَاذِبُونَ {18}

“Siku atakayowafufua Mwenyezi Mungu wote; wamuapie kama wanavyoapa kwenu, na watadhani kwamba wamepata kitu. Kwa hakika hao ndio waongo hasa.” (58: 18)

Swali la pili linatokana na jibu la swali la kwanza nalo ni kuwa, ikiwa mtu ataweza kusema uwongo kesho, bali hata kuapa, kama ilivyo katika maisha haya ya duniani. Basi kuna wajihi gani kuita akhera nyumba ya ukweli na kuiita nyumba yetu hii (dunia) nyumba ya uwongo?

Jibu: Makusudio ya kutofautisha huku ni kwamba uwongo hapa duniani unaweza ukamletea mtu manufaa au kumkinga na madhara. Ama huko akhera hautafaa chochote. Kwa maneno mengine, kushindwa kusema uwongo, ni kitu kingine na kuweza kusema bila ya manufaa ni kitu kingine.

Angalia jinsi wanavyojisemea uwongo wenyewe.

Msemo unaelekezwa kwa Mtume (s.a.w.) na makusudio yake ni kwa wote, nako ni kusataajabu kutokana na kukana kwao ushirikina na hali wamekufa juu ya ushirikina. Kila mwenye kukana jambo alilonalo au kudai asiyokuwa nayo kwa makusudi, basi amejidaganya mwenyewe, Mwenyezi Mungu na watu:

Na yamepotea waliyokuwa wakiyazua.

Hiyo inaungana na ‘wanavyojisemea uwongo.’ Maana yake ni angalia Ewe Muhammad vipi yamewapotea washirikina yale waliyokuwa wakiyatarajia kuwa yatawasaidia na kuwaombea.

وَمِنْهُمْ مَنْ يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ ۖ وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَنْ يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِنْ يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَا يُؤْمِنُوا بِهَا ۚ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوكَ يُجَادِلُونَكَ يَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ {25}

Na miongoni mwao wako wanaokusikiliza, na tumezitia pazia nyoyo zao wasije kuyafahamu na mna uziwi masikioni mwao. Na wakiona kila Ishara hawaiamini. Hata wakikujia kujadaliana nawe wanasema waliokufuru: Hizi si chochote isipokuwa ni ngano za watu wa kale.

وَهُمْ يَنْهَوْنَ عَنْهُ وَيَنْأَوْنَ عَنْهُ ۖ وَإِنْ يُهْلِكُونَ إِلَّا أَنْفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ {26}

Nao wanamkatazia na wenyewe wanajitenga naye. Na hawaangamizi ila nafsi zao na hawatambui.