read

Aya 116-118: Issa Na Watu

Lugha:

Neno nafsi linatumika kwa maana nyingi, mingoni mwazo ni:

• Uhai wa binadamu na wanyama. Maana haya ndiyo aliyoyakusudia Mwenyezi Mungu aliposema: "Kila nafsi itaonja mauti"

• Dhati ya kitu, mfano: ndicho nafsi yake.

• Ghaibu, mfano: Siijui nafsi ya fulani, yaani ghaibu yake. Haya ndiyo maana yaliyokusudiwa katika: Unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu na wala siyajui yaliyo katika nafsi yako.

Maana

Na pale Mwenyezi Mungu atakaposema: Ewe Isa bin Maryam! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu hamkusudii Isa hasa kwa swali hili, kwa sababu yeye anajua kuwa Issa hakuwaambia watu hivyo. Isipokuwa anakusudia kuweka hoja kwa yule anayedai madai haya ya kikafiri kwa Isa na mama yake.

Atasema: Wewe umetakasika! Na ushirika. Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu.

Kwa sababu yeye ni Mtume na Mtume ni maasum, mwenye kuhifadhiwa na makosa, na yeye ametumwa kupiga vita ushirikina na kuleta mwito wa Tawhid (umoja wa Mungu), vipi tena yeye mwenyewe adai uungu na awatake watu wamwabudu?

Ikiwa niliyasema basi bila shaka umekwishayajua.Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu wala mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika wewe ndiye mjuzi zaidi wa yaliyofichikana.

Anatoa ushuhuda wa usafi wake wa shirki yao kutokana na ilimu ya Mwenyezi Mungu. Huo ni ushahidi tosha.

Sikuwaambia ila uliyoniamrisha, ya kwamba, Mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa nao na uliponifisha ukawa wewe ndiye mwangalizi juu yao.

Imelezwa katika matayo: “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Iblisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.” (Mathayo: 4:1-2) , “....Nenda zako shetani, kwa maana imeandikwa , msujudie Bwana Mungu wako, umuabudu yeye pekee.” (Mathayo 4:10 )

Je Mungu anafunga? Basi anamfungia nani? Je anakuwa na njaa na yeye ndiye mtoaji riziki? Vipi ajaribiwe na Iblis na hali yeye ni mjuzi wa ghaib? Vipi aweze kuchukuliwa kutoka mlima mmoja hadi mwingine na yeye ndiye aliyeiumba na kuumba ulimwengu wote.

Ukiwaadhibu basi hao ni waja wako. Na ukiwasamehe basi wewe ndiye mwenye nguvu mwenye hekima.

Baadhi ya malezo ya tafsir yanasema kuwa kauli ya Isa (as): “Ukiwaadhibu basi hao ni waja wako, ni kuwaaombea msamaha kwa adabu na matarajio, na neno: "Basi ni waja wako" Inadhamini hilo. lakni baadhi wamekataa isipokuwa huchukulia kusamehewa kwa kutubia; yaani wakitubia uwasamehe.

Tunawajibu wenye kusema hivi kwamba msamaha pamoja na toba hauhi- taji uombezi; kwa sababu mwenyewe Mwenyezi Mungu amejiwekea kum- samehe anayetubia. Kisha kuna kizuizi gani kwa Issa kuwaombea watu wake maghufira na rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu? Nabii Ibrahim alikwishawaombea watu wake kwa kusema:

فَمَنْ تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي ۖ وَمَنْ عَصَانِي فَإِنَّكَ غَفُورٌ رَحِيمٌ {36}


"Basi



aliyenifuata



huyo



ni



wangu



mimi



na



aliyeniasi



hakika



wewe



ni mwingi



wa



maghufira



mwenye



kurehemu"



(14:36).

Zaidi ya hayo ni kwamba kumsamehe mkosaji ni jambo zuri kwa hali yoyote,

أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ ۚ {32}


"Je,



wao



wanaigawa



rehema



ya



Mola



wako?"



(43:32)

قَالَ اللَّهُ هَٰذَا يَوْمُ يَنْفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ ۚ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ {119}


Mwenyezi



Mungu



atasema:


Hi


i


ndiy


o


sik


u


ambayo wasema


o


kwel


i


utawafaa


ukweli



wao.


W


ao



watapata bustani zipitazo



mito



chini


yake


.


Hum


o


watadumu milele


.


A


w


e



radh


i



nao


Mwenyezi Mungu na wao


waw


e


radh


i


naye


.


Huko


ndiko



kufuzu



kukubwa


.

لِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ {120}


Mwenyez


i


Mung


u


ndiye


mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo, naye ni



Muweza



wa



kila



kitu.