read

Aya 38-39: Wanyama Na Ndege Ni Umma

Lugha

Mnyama, ni kila anayetembea katika ardhi wakiwa ni: Watu, wanyama na wadudu.

Maana

Na hakuna mnyama katika ardhi wala ndege arukaye kwa mbawa zake, ila ni umma kama nyinyi.

MwenyeziMungu(s.w.t)anabainishakatikaAyahiikwambabainayetuna wanyama kuna aina ya kufanana, lakini hakufafanua aina yenyewe. Je, tunafanana katika kuwa wao ni viumbe wa Mwenyezi Mungu; au katika kumwamini Mwenyezi Mungu na kumsifu kwa sifa zake njema? Au tunafanana katika kuwa wao ni aina zinazojulikana kwa majina; kama zinavyojulikana koo na kabila? Au ni katika kupanga maisha yao na kufanya mambo kulingana na masilahi?

Kwa hali yoyote iwayo ni kuwa wataalamu wengi wamechunguza tabia na kazi za wanyama, wadudu na ndege na wakafikia kwenye siri za ajabu zinazoshuhudia kuweko mpangaji mwenye hekima. Tutataja baadhi ya mifano.

Ndovu huweka mahakama kwa mhalifu na ndovu aliyekosea huhukumiwa kwa kutengwa na kundi la wengine ili aishi peke yake katika upweke.

Kunguru anapohisi hatari itakayowapata wenzake huwaonya kwa sauti maalum. Ama katika hali ya furaha hutoa sauti iliyo karibu na kicheko.

Utauliza? Kuna faida gani katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu kusema arukaye kwa mbawa zake ambapo kumtaja Ndege kunafahamisha moja kwa mja kuruka kwa mbawa?

Jibu: Hakuna faida, tuijuayo, isipokuwa ufasaha wa maneno.

Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote.

Imesemekana kuwa makusudio ya Kitab hapa ni lawhim-mahfudh (ubao maalum wenye kuhifadhiwa) wenye kukusanya yaliyokuwa na yatakayokuwa.

Kauli ya pili, inasema ni fumbo la ujuzi wa Mwenyezi Mungu kujua makusudio ya mtu, na kauli zake na vitendo vyake.

Kauli ya tatu, inasema ni Qur’an na kwamba Mwenyezi Mungu amebain- isha ndani yake kila yapasayo kubainishiwa watu, miongoni mwa misingi ya dini na matawi yake na yanayofungamana nayo. Nasi tumeichagua kauli hii katika kufasiri Juz. 1 (2:2) kifungu Qur’an na sayansi

Kisha watakusanywa kwa Mola wao.

Dhahiri ya maneno inafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu atawakusanya wanyama na ndege siku ya Kiyama, kama atakavyowakusanya watu. Vilevile Aya isemayo: “Na wanyama mwitu watakapokusanywa.” (82:5)

Maulama wengi wamesema hivyo kwa kutegemea Aya hizo mbili na Hadith isemayo: “Hakika Mwenyezi Mungu atawachukulia kisasi watu kutokana na wenye pembe.”

Sisi tuko pamoja na Ibn Abbas aliyesema kuwa makusudio ya kukusanywa wanyama ni mauti yao; kama ilivyopokewa katika Hadith: “Anayepatwa na kifo ndiyo kiama chake.” Kwa sababu hisabu na adhabu ni baada ya kukalifiwa na sharia na kuzihalifu. Wala hakuna kukalifiwa na sharia ila pamoja na akili; na wanyama na ndege hawana akili, kwa hiyo hawakali- fiwi na sharia.

Kwa sababu hizo basi, hawatakusanya kwa ajili ya hisabu. Lau wanyama wangelichukuliwa hisabu basi ingefaa zaidi watoto wadogo wachukuliwe hisabu. Ama Hadith ya ‘kuchukua kisasi’, ni fumbo la uadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kwamba yeye hataacha kidogo wala kikubwa ila atakidhibiti.
Ikiwa Mwenyezi Mungu atawaadhibu wenye pembe wakimpiga mtu, basi vizuri zaidi ni kutuharimishia sisi kuwachinja wanyama.

Ama kauli ya anayesema kuwa Mwenyezi Mungu atayabadilisha maumivu ya mtu kwa mnyama, hiyo ni kumsemea Mwenyezi Mungu bila ya ujuzi wowote.

Na wale waliokadhibisha ishara zetu ni viziwi na mabubu wako gizani.

Yaani wao ni kama viziwi, kwa sababu wao hawasikii mwito wa haki, na ni kama mabubu kwa sababu wao hawaitamki haki waliyoijua na wako katika giza la kufuata na giza la ushirikina, ukafiri, ufasiki na dhambi.

Amtakaye Mwenyezi Mungu humpoteza na amtakaye humweka kati- ka njia iliyonyooka.

Yametangulia maelezo kuhusu uongofu na upotevu katika Juz.1 (2:26) na Juz.2(4:88).

قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّهِ أَوْ أَتَتْكُمُ السَّاعَةُ أَغَيْرَ اللَّهِ تَدْعُونَ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ {40}

Sema: niambieni, kama ikiwafikia adhabu ya Mwenyezi Mungu au ikiwafikia ile saa, je, mtamuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni wakweli?

بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِنْ شَاءَ وَتَنْسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ {41}

Bali yeye tu ndiye mtakayemuomba. Atawaondolea mnayomuom- ba akitaka. Na mtawasahau mnaowashirikisha.

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِنْ قَبْلِكَ فَأَخَذْنَاهُمْ بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَتَضَرَّعُونَ {42}

Kwa hakika tulipeleka (Mitume) kwa umma zilizokuwa kabla yako; kisha tukawatia katika shida na madhara ili wapate kunyenyekea.

فَلَوْلَا إِذْ جَاءَهُمْ بَأْسُنَا تَضَرَّعُوا وَلَٰكِنْ قَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ {43}

Basi mbona wasinyenyekee ilipowafikia adhabu yetu? Lakini nyoyo zao zilikuwa ngumu na shetani akawapambia waliyokuwa wakiyafanya.

فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّىٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُمْ بَغْتَةً فَإِذَا هُمْ مُبْلِسُونَ {44}

Basi waliposahau yale waliyokumbushwa tuliwafungulia milango ya kila kitu, mpaka walipofurahia yale waliyopewa tuliwakamata kwa ghafla; na mara wakawa wenye kukata tamaa.

فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ {45}

Ikakatwa mizizi ya watu waliodhulumu; na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote.