read

Aya 17 – 19: Hakuna Mwondoaji Madhara Ila Mwenyezi Mungu

Maana

Na kama Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hakuna wa kuyaondoa ila yeye.

Aya hii inafahamisha kuwa madhara kama vile ufukara, maradhi n.k. ni kazi ya Mwenyezi Mungu sio ya mtu. Vilevile kuyaondoa na kuepukana nayo ni kazi yake. Kwa hiyo kuna haja gani ya kufanya juhudi na kufanya kazi ?

Jibu: Kwanza, kufanya juhudi na kujitafutia riziki ni wajibu kiakili na kinakili (nukuu). Ama kiakili ni kwamba uhai haukamiliki ila kwa kazi. Na kinukuu zimepituka kiwango cha mutawatir. Miongoni mwazo ni:

فَانْتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِنْ فَضْلِ اللَّهِ{10}



T


awanyikeni



katika



ardhi



mtafute



fadhila



ya



Mwenyezi



Mungu”



(62:10)

هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِنْ رِزْقِهِ ۖ {15}



Y


eye ndiye aliyeidhalilisha ardhi kwa ajili yenu; basi tembeeni katika pande



zake



na



mle



katika



rizki



zake.”



(67:15).

Katika Hadith ni “Safirini mtapata faida.” Nyingine ni: “Fanyianeni dawa enyi waja wa Mwenyezi Mungu, kwani yule ambaye ameteremsha ugonjwa, ameuteremshia na dawa.”

Kwa hiyo basi atakayezembea akaacha kuhangaika na akapatwa na madhara, yeye mwenyewe ndiye atakayekuwa na jukumu. Mwenye kuhangaika bila ya kuzembea na akaguswa na madhara, basi jamii yake iliyo mbovu katika hali na hukumu zake ndiyo itakayokuwa na jukumu.

Ikiwa jamii yake pia ni nzuri basi atakuwa amedhurika kwa kudura ya Mwenyezi Mungu na majaaliwa yake.

Pili, Hakika Mwenyezi Mungu hamtakii madhara mja wake yeyote. Vipi iwe hivyo, na hali yeye ndiye aliyesema:

وَمَا أَنَا بِظَلَّامٍ لِلْعَبِيدِ {29}




Na



mimi



siwadhulumu



waja.”



(50:29)

Na ndiye mwenye kusema:

وَاللَّهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ {207}


“Na



Mwenyezi



Mungu



ni



mpole



kwa



waja”



(2:207)

Na katika Hadith imeelezwa: “Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwahurumia zaidi waja wake kuliko mama anavyomhurumia mwanawe.”

Kwa hiyo basi makusudio ya madhara katika Aya hii ni yale anayolipwa mja kutokana na amali yake; au ni mtihani kwa ajili ya masilahi yake na mengineyo ambayo hayapingani na uadilifu wake Mwenyezi Mungu na rehema yake. Tumeyafafanua hayo tulipofasiri (5:100).

Na akikugusisha kheri, basi yeye ndiye mwenye uweza juu ya kila kitu.

Yaani hakuna wa kuzuia heri na fadhila zake. Arrazi anasema: “Mwenyezi Mungu katika kheri ametaja kuwa yeye ndiye mwenye uweza juu ya kila kitu na katika madhara ametaja kuwa hakuna wa kuyaondoa ila yeye, ametaja hivyo kwa kufahamisha kuwa matakwa ya Mwenyezi Mungu kufikisha kheri yanashinda yale matakwa yake ya kufikisha madhara.”

Naye ndiye mwenye kuwatenza nguvu waja wake; naye ndiye mwenye hekima mwenye habari.

Kutenza nguvu ni ishara ya uweza wa Mwenyezi Mungu na kuwa na habari ni ujuzi wake. Amewatenza nguvu Mwenyezi Mungu waja wake kwa kuwafanya waweko bila ya kutaka kwao; na amewatenza nguvu vilevile kwa mauti.

Ibnul-Arabi katika Futuhatil-makkiyya anasema: “Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewatenza nguvu waja wake kwa sababu wao wamempin- ga na wakagombana naye katika kuhalifu hukumu zake na mwenye kugombana na Mwenyezi Mungu basi yeye ni mwenye kutenzwa nguvu na hapana budi kushindwa,.’

Sema: Ni kitu gani kikubwa zaidi kwa kutoa ushahidi?

Yako maelezo katika baadhi ya Hadith kuwa Washirikina wa Makka walimwambia Mtume: Mayahudi na Wakristo hawashuhudii Utume wako hebu tuonyeshe anayekushuhudia. Ndipo akateremsha Mwenyezi Mungu (s.w.t) Aya hii.Yaani waulize Ewe Muhammad ni nani ambaye ushahidi wake uko juu ya ushahidi wote? Kisha akamwamrisha kuwajibu: Sema:

Mwenyezi Mungu ndiye shahidi baina yangu na baina yenu.

Hakuna jawabu halisi kama hili, nalo ni kuwa shahidi baina yetu ni Mwenyezi Mungu.

Na nimepewa wahyi Qur’an hii ili niwaonye kwayo na kila imfikiayo.

Qur’an ni ushahidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya Mtume Muhammad, ambayo imewashinda kuleta hata Sura moja mfano wake, wakajaribu wakashindwa. Kushindwa huku ni ushahidi mkubwa wa ukweli wa Mtume katika risala yake.

Kauli yake: ‘Ili niwaonye kwayo na kila imfikiayo,’ Maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemteremshia hii Qur’an ili imuonye kila itakayemfikia mpaka siku ya ufufuo. Sahaba mmoja alikuwa akisema: “Atakeyefikiwa na Qur’an ni kama kwamba amemwona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.)”

Vilevile Aya hii inafahamisha kuwa ambaye haukumfikia mwito wa Muhammad (s.a.w.), basi anasamehewa katika kuacha Uislamu. Hayo nimeyazungumza kwa ufafanuzi katika Juz. 4 (3:115).

Je, kweli nyinyi mnashuhudia kwamba wako waungu wengine pamo- ja na Mwenyezi Mungu?

Swali hapa ni la kukanusha na kuyaweka mbali hayo. Maana ni vipi mtam- fanya Mwenyezi Mungu pamoja na waungu wengine baada ya kuwa wazi dalili za umoja wake Mwenyezi Mungu Mtukufu! Kisha Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kujibu kuwa yeye hashuhudii kama wanavyoshuhudia.

Sema: Mimi sishuhudii. Kisha akamwamrisha jambo jingine: Sema: Yeye ni Mungu mmoja tu, na hakika mimi ni mbali na hayo mnayoyashirikisha ya kuabudu masanamu na mengineyo.

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمُ ۘ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنْفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ {20}


W


al


e


tuliowap


a



Kitab


wanamjua



kama



wanavyowajua



wana



wao.


W


ale



ambao wamezitia hasarani nafsi zao hawaamini.

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ {21}


Na



ni



nani



dhalimu



zaidi kuliko yule amzuliaye Mwenyezi Mungu uwongo. Au azikadhibishaye ishara zake? Hakika madhalimu hawatafaulu.

وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا أَيْنَ شُرَكَاؤُكُمُ الَّذِينَ كُنْتُمْ تَزْعُمُونَ {22}


Na



siku



tutakapowakusanya


wote


,


kish


a


tutawaaambia


wale



walioshirikisha:


W


ako


wap


i


washirikishw


a


wenu


mliokuwa



mnadai?

ثُمَّ لَمْ تَكُنْ فِتْنَتُهُمْ إِلَّا أَنْ قَالُوا وَاللَّهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ {23}


Kish


a


hautakuw


a



udhuru


wao



ila



kusema



W


allahi,



Mola wetu! Hatukuwa



washirikina.

انْظُرْ كَيْفَ كَذَبُوا عَلَىٰ أَنْفُسِهِمْ ۚ وَضَلَّ عَنْهُمْ مَا كَانُوا يَفْتَرُونَ {24}


Angalia



jinsi



wanavyojisemea uwongo wenyewe. Na yamepotea



waliyokuwa



wakiyazua.