Aya 112-115: Chakula Kutoka Mbinguni
Maana
Maneno yamekuwa mengi kuhusu chakula na waliokitaka kuwa je, walikuwa waumini au watiaji shaka? Na kwamba je, kilishuka chakula au hakikushuka kwa sababu wanafunzi waligeuza maombi yao baada ya kutishiwa na Mwenyezi Mungu aliposema: “Lakini atakayekufuru baada ya hapo basi nitamwadhibu adhabu ambayo sijamwadhibu yeyote katika ulimwengu.”
Kama tukikadiria kuwa kilikuja je kilikuwa ni cha aina gani na rangi gani? Kisha je, waligeuzwa manyani au nguruwe baadaye kwa sababu waliiba? Sisi tutaelekea kwenye mazungumzo yetu na tunayofahamishwa na matamko ya Aya na yanayoambatana nayo.
Waliposema Wanafunzi: Ewe Isa bin Mariyam, Je Mola wako anaweza kututeremshia chakula kutoka mbinguni; akasema Mcheni Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni waumini.
Aya hii inaashiria kuwa wanafunzi hawakuwa wakimwamini Isa walipomtaka chakula kwa sababu wao hawahitajii chakula ndipo waamini, linalotil- ia nguvu hilo ni kusema kwao: Je anaweza Mola wako." Huku ni kutambulisha kutia shaka katika uweza wa Mwenyezi Mungu. Hata hivyo Aya iliyotangulia imeshuhudia kuamini kwao. "wakasema tumeamimi…" Zaidi ya hayo neno wanafunzi lenyewe linafahamisha kumwamini Isa na sasa je kuna wajihi gani wa kuchanganya Aya mbili hizi?
Wafasiri wengi wamejibu kuwa swali lao hili halipingi imani yao. Kwa sababu makusudio yake ni kuamini kwa njia za hisia na macho, baada ya kuamini kwa njia ya akili na dalili. Kwa maneno mengine ni kuitia nguvu imani na kuithibitisha; sawa na alivyosema Ibrahim (as):
وَلَٰكِنْ لِيَطْمَئِنَّ قَلْبِي ۖ {260}
Na wanafunzi wamelifafanua kusudio lao hili kwa kusema kwao katika Aya inayofuatia: Na ili zitulie nyoyo zetu ikiwa ni jibu la walivyoambi- wa na Isa "mcheni Mola wenu ikiwa nyinyi ni waumini." Ama kusema kwao, “Je aweza Mola wako" maana yake je, atakubali Mola wako tukimuuliza kututeremshia chakula kutoka mbinguni?
Wakasema: Tunataka kula katika hicho na ili zitulie nyoyo zetu na tujue ya kuwa umetuambia kweli na tuwe miongoni mwa wanaoshuhudia.
Wanataka wale ili waamini na wajue au wanataka wale ili waitie nguvu imani katika nyoyo zao na elimu katika akili zao; kama tulivyotangulia kueleza, kisha wampe habari asiyehudhuria chakula katika watu wao aami- ni mpinzani na utulie moyo wa muumini hata kama hatakula.
Wanafunzi Wa Muhammad (Saw) Na Wa Isa (As)
Mtume Muhammad naye alikuwa na wanafunzi kama alivyokuwa nao Isa (as) na Mtume wowote katika Mitume. Lakini wanafunzi wa Muhammad hawakumwomba kuwashibisha kutokana na njaa kwa kutumia miujiza yake, kama walivyofanya wanafunzi wa Isa ambao walisema"Tunataka kula katika hicho", wala hawakutaka awasalimishe na hofu , kama walivyofanya sahaba wa Musa (as) bali walimwambia katika baadhi ya vita kupitia mdomoni mwa Mikidadi bin Al-Aswadi "Endelea ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa lile alilokutakia Mwenyezi Mungu na sisi tuko pamoja nawe wala hatutakwambia yale waliyosema wana wa Israil kwa
Musa: Nenda wewe na Mola wako mpigane na sisi tuko hapa tumekaa. Lakini sisi tunakwambia: Nenda wewe na Mola wako mkapigane na sisi tuko pamoja nanyi. Walikuwa wakifa mashahidi mbele yake na huku wakisema: “Tumefuzu, naapa kwa Mola wa Al-Kaaba.” Masimulizi ya historia yao utafikiri ni vigano tu.
Ammara bin Yazid alipigana siku ya Uhud mpaka majeraha yakamzidia. Alipoona sasa anakufa alijitupa miguuni mwa Mtume (s.a.w), hakuinua kichwa chake hapo mpaka alipomaliza uhai wake kwa muishilio huu mwema.
Alipoanguka Sa'ad bin Rabi, siku ya Uhud, alimwambia mmoja wa wenzake: "Mwambie Mtume wa Mwenyezi Mungu, Saad Bin Rabi anasema umetupa kitu bora cha Mtume alichowapa umma wake na wafikishie salam zangu watu wako uwaambie mwana wa Rabi anawaambia hamtakuwa na udhuru wowote kwa Mwenyezi Mungu kama mkimwacha Mtume wetu hata kidogo."
Amra bin Jumuh alikuwa mlemavu na akataka kutoka pamoja na Mtume kwenda vita vya Uhud. Watoto wake walipojaribu kumzuia akaondoka kumshtakia Mtume (saw): "Mimi nataraji kuchechemea usiku kwenda peponi." Mtume (saw) akamruhusu. Akauliwa yeye, watoto wake wane na shemeji yake. Baada ya vita mjane wake akaja, akachukua maiti ya mumewe, nduguye na wanawe wane kwenye ngamia na kwenda nao Madina.
Wanawake wakamkabili kumuuliza habari, akasema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko salama, ama msiba mwingine zaidi ya Mtume ni mwepesi."
Wakamuuliza: "Na hizi maiti ni za nani?" Akawajibu: “Wanangu, mume wangu na ndugu yangu. Mwenyezi Mungu amewakir- imu kwa kufa mashahidi ninawachukua nikawazike"
Mifano hii tumeileta kutofautisha baina ya sahaba wa Muhammad na wa mitume wengineo. Wala hatutakuwa tumeongeza chumvi, kama tukisema kuwa hakuna mtume yeyote aliyekuwa na masahaba kama Mtume Muhammad (saw). Ama siri ya hilo inakuwa katika utu wake utukufu wake na risala yake.
Akasema Isa bin Maryam: Ewe Mwenyezi Mungu Mola wetu! Tuteremshie chakula kutoka mbinguni ili kiwe sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ishara itokayo kwako na uturuzuku kwani wewe ni mbora wa wanaoruzuku.
Alipoona kuwa wao wanang'ang’ania, aliomba kwa unyenyekevu: Ewe Mola wetu! Kuondoa shub-ha na kumkadhibisha kila atakayedai kuwa Isa ana uwezo katika hilo. Makusudio ya ishara ni mujiza. Na sikukuu ni furaha.
Mwenyewzi Mungu akasema: Hakika mimi nitakuteremshia lakini atakayekufuru baada ya hapo basi nitamwadhibu adhabu ambayo sijamwadhibu yeyote katika walimwengu.
Mwenyezi Mungu aliitikia maombi ya Isa ili sahaba zake wazidi kumwamini na kuamini utume wake na awe na hoja nao, kama watahalifu na watastahiki adhabu kali ambayo hajamwadhibu yeyote katika waliokanusha na waliokufuru. Kwa sababu wao ndio waliotoa maombi ya chakula na kukitaka; na mwenye kuitikiwa maombi yake amesimamiwa na hoja na hana udhuru wowote wakuhalifu.
وَإِذْ قَالَ اللَّهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنْتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَٰهَيْنِ مِنْ دُونِ اللَّهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِنْ كُنْتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنْتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ {116}
مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۚ وَكُنْتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنْتَ أَنْتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنْتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ {117}
إِنْ تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِنْ تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنْتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ {118}