read

Aya 106-108: Kuthibitisha Wasia

Maana

Aya hizi tatu ni katika Aya za hukumu, na zinaingia katika mlango wa wasia na ushahidi. Ndani yake mna hukumu zifuatazo:

1. Enyi mlioamini! yanapomfikia mauti mmoja wenu, wakati wa kuusia ushahidi kati yenu ni wa waadilifu wawili miongoni mwenu, Mwenyezi Mungu anakusudia kuwa atakayehisi kuwa ajali yake imekurubia na akataka kuusia anayoyataka, awalete waadilifu wawili katika Waislamu na awashuhudishe juu ya wasia wake.

Ilivyo ni kuwa wasia ni sunna na wala si wajibu ila kwa ambaye ana haki za watu au za Mwenyezi Mungu na zikamdhihirikia dalili za mauti na akahofia kupotea baada yake

2. Au Wengine wawili wasiokuwa katika nyinyi mnapokuwa safari- ni na msiba wa mauti ukawafikia. Mtawazuia wawili hao baada ya Swala, na waape kwa Mwenyezi Mungu mkiwa na shaka: Hatupokei thamani yoyote kwa haya hata kama ni jamaa wala hatufichi ushahidi wa Mwenyezi Mungu, hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye dhambi.

Shia na Hambal wamesema kuwa Mwislamu akiusia safarini na asipate Mwislamu, basi anaweza kuwashuhudiza watu wawili katika Ahlul-Kitab (watu wa kitab) kuwa waape baada ya Swala mbele ya watu kuwa wao hawakuhini watu kuficha wala hawakupokea chochote kwa ushahidi au kiapo. Hapo ushahidi wao utakubaliwa kama utakavyokubaliwa wa Waislamu wote. Na itapasa juu ya hao mashahidi kuapa ikiwa kuna shaka katika ukweli wao. Ama mwaminifu hana kiapo, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Mkiwa na shaka."

Hivi ndivyo walivyofutu Shia Imamiya na Hanbal kwa kutegemea Aya hii. Ama Abu Hanifu, Malik na Shafi, wamesema kuwa haukubaliwi ushahidi wa asiyekuwa Mwislamu kwa hali yoyote ile, na wameifanyia taawili Aya kwa maana nyingine. Ameongezea Malik na Shafi kuwa haukubaliwi ushahidi wa asiyekuwa Mwislamu kwa hali yoyote hata kama ni kwa wao kwa wao. Hayo yamo katika Kitab Al-Mughni.

3. Ikigundulika kuwa wawili hao wamestahiki dhambi, basi wengine wawili watasimama mahali pao katika wale ambao wamestahiki (kudai). Washike nafasi ya wa mwanzo waape kwa Mwenyezi Mungu: Ushahidi wetu ni haki zaidi kuliko wa wale; na sisi hatukupita kiasi; hakika hapo tutakuwa miongoni mwa madhal- imu.”

Imeelezwa katika sahih za Shia na Sunni kwamba Aya hii ilishuka kwa sababu ya watu watatu waliosafiri kibiashara, mmoja wao akiwa Mwislamu na wawili Wakristo. Njiani yule Mwislamu akaugua na akahisi kuwa ajali yake imekurubia, akaandika wasia wake, akitaja vitu vyote alivyo navyo na akauficha katika baadhi ya mizigo yake bila ya kuwafahamisha wale wenzake; kisha akawausia kuwa mizigo yake waifikishe kwa watu wake.
Alipokufa, wale wawili walichukua kitu kutoka katika bidhaa zile za maiti na wakapeleka zilizobaki kwa watu wake. Walipogundua watu wa marehemu wasia wake, waliona kuwa kuna kitu fulani kilichotajwa hakimo. Hivyo wakawauliza wale wawili, wakakanusha na wakasema wakiapa: "Alichotupa ndicho tulichowapa".

Watu wa marehemu wakakiona kile kitu kwa mtu mwengine. Walipomuuliza umekipata wapi, akajibu kutoka kwa fulani na fulani (wale watuhumiwa wawili). Kesi ikapelekwa kwa Mtume (s.a.w.w.). Inasemekana kuwa wale wawili walipoonyeshwa, walisema tulikinunua kwake (yule marehemu). Ndipo ikashuka Aya hii.

Maana yake yakiwa kama alama za kuleta shaka zikidhihiri kwa watuhumiwa basi wajibu wakati huo ni kusimama watu wawili katika warithi wa marehemu na waape kwa Mwenyezi Mungu kwamba wao ni wa kweli kuliko watuhumiwa na waseme katika kiapo chao: “Sisi hatukupita kiasi; hakika hapo tutakuwa miongoni mwa madhalimu.” Baada ya kiapo watahukumiwa watuhumiwa.

Unaweza kuuliza: Maneno ya wafasiri yamekuwa marefu na kugongana kuhusu kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Katika wale ambao wamestahiki."

Mpaka ikanukuliwa kutoka kwa mmoja wa wakale akisema: “Hii ndiyo jumla yenye mushkeli zaidi kwa muundo katika kitab cha Mwenyezi Mungu.” Sasa je tafsir sahihi ni ipi?

Jibu: Lililowatia wafasiri kwenye shaka ni kuwa dhamir ya wanaostahiki inawarudia nani? Tujuwavyo sisi ni kuwa inawarudia warithi wa marehemu kwa sababu madeni na mambo mengine, yaliyokuwa yakimstahiki marehemu yanawastahiki warithi baada ya kufa kwake.

Kwa hiyo maana yatakuwa. Wataapa wawili katika wale ambao ni wajibu juu yao yale yaliyo wajibu kwa wanayemrithi. Mfumo wa Aya unalitilia mkazo hili.

Kwa sababu wengine wawili watakaosimama mahali pa watuhumiwa katika kuapa, hapana budi wawe ni katika warithi wa marehemu kwa maafikiano ya wafasiri, na haiwezekani kwa hali yoyote kuwa ni wengineo. Kwa hiyo inakuwa dhamiri ya wanaostahiki inawarudia wao hasa.

Hiyo inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi ulio sawa au watao- gopa visije vikaletwa viapo vingine baada ya viapo vyao.

Hiyo ni ishara ya hukumu iliyotangulia na kuelekea zaidi ni ubainifu wa sababu ya hukumu. Yaani makusudio ya sharia tuliyoiweka ni kutogeuza mashahidi ushahidi wao wakaapa uwongo au kujizuia kuapa kwa kuhofiwa kupingwa viapo vyao na viapo vya warithi.

Unaweza kuuliza kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alipobainisha hukumu aliweka wawili wawili, akasema: Ushahidi wao wawili, watasimama wawili. Lakini aliposihiria sababu ya hukumu amebainisha kwa wengi akasema: Ya kwamba watatoa ushahidi. Je kuna wajihi gani?

Jibu mashahidi ni wane: wawili wanashuhudia mwanzo, na wawili watasimama mahali pao ikiwa litadhihiri kosa kwa ushahidi wa kwanza. Zaidi ya haya ni kwamba sababu katika hukumu ni kuenea kwenye maudhui yaliyo tajwa na mengineyo.

يَوْمَ يَجْمَعُ اللَّهُ الرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَا أُجِبْتُمْ ۖ قَالُوا لَا عِلْمَ لَنَا ۖ إِنَّكَ أَنْتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ {109}


Siku ambayo Mwenyezi Mungu atawakusanya Mitume awaambie mlijibiwa nini?”


W


atasema: “Hatujui, hakika wewe ndiwe mjuzi sana wa ghaibu.

إِذْ قَالَ اللَّهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ اذْكُرْ نِعْمَتِي عَلَيْكَ وَعَلَىٰ وَالِدَتِكَ إِذْ أَيَّدْتُكَ بِرُوحِ الْقُدُسِ تُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا ۖ وَإِذْ عَلَّمْتُكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنْجِيلَ ۖ وَإِذْ تَخْلُقُ مِنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ بِإِذْنِي فَتَنْفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِي ۖ وَتُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ تُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ كَفَفْتُ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَنْكَ إِذْ جِئْتَهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ إِنْ هَٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُبِينٌ {110}


Atakaposema Mwenyezi Mungu: Ewe Isa mwana wa Maryam! Kumbuka neema yangu juu yako na juu ya mama yako. Nilipokutia nguvu kwa


r


oho mtakatifu, ukazungumza na watu utotoni na katika utu uzima. Na



nilivyokufundisha kitab


n


a


hekim


a


n


a


T


awra


t


na


Injil. Na ulipotengeneza kwa udongo



kama umbo la ndege



kwa idhini yangu, kisha ukapuliza likawa ndege kwa idhini yangu, na ulipowaponyesha vipofu na wenye mbalaga kwa idhini yangu na ulipowatoa wafu kwa



idhini yangu, na nilipokukinga na wana wa Israil ulipowafikia na hoja zilizowazi; wakasema wale waliokufuru miongoni mwao.



Haya



si



chochote



ila ni uchawi tu.

وَإِذْ أَوْحَيْتُ إِلَى الْحَوَارِيِّينَ أَنْ آمِنُوا بِي وَبِرَسُولِي قَالُوا آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ {111}


Na nilipowafahamisha wanafunzi kwamba Niaminini



mimi



na



Mtume wangu, wakasema


T


umeamini



na ushuhudie kuwa sisi ni wanyenyekevu.