read

Aya 114: Kuzuia Misikiti Ya Mwenyezi Mungu

Maelezo

Aya hii ni katika Aya ambazo kauli za kuifasiri zimekuwa nyingi. Dhahiri yake inafahamisha makemeo na kiaga kwa asiyeiheshimu misikiti au sehemu yoyote ya kufanyia ibada na kuzuia kujengwa au kufanyiwa ibada ndani yake.

Vile vile kuivunja au kuipuuza. Na kwamba wajibu wa kimungu na wa kibinadamu unafaradhishia kila mtu kuzitakasa sehemu za kufanyia ibada na kuziingia kwa heshima na unyenyekevu, na hali ya kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu na kutaraji thawabu zake, sio kuzivunjia heshima na kuzidharau. Kwa sababu ziliwekwa kwa lengo la ibada.

Kisha Mwenyezi Mungu amebainisha kwamba mwenye kuziingilia sehemu za ibada kwa nia mbaya atamdhalilisha katika maisha ya dunia na kesho atamwadhibu adhabu kubwa.

Kwa ufupi Ayainabainisha kwamba mwenye kufanya jambo kadha atafanyiwa kadha. Na hilo ni suala la kijumla sio lililopita wala la wakati wa kushuka Aya au kungoja kutokea.

Lakini wafasiri wamesema kuwa ni suala maalum; kisha wakahitalifiana kwamba je suala lenyewe lilitokea kabla ya Utume wa Muhammad (s.a.w.) au baada yake?Wale waliosema kuwa lilitokea kabla nao pia wamehitalifiana katika kulielezea tukio lenyewe.

Kuna baadhi yao waliosema kwamba Aya inaelezea tukio la Titus wa Roma alipoingia Baytul-Maqdis baada ya kufa Masih kwa kiasi cha miaka sabini; akaiharibu kiasi ambacho halikubaki jiwe juu ya jiwe jengine; akavunja hekalu la Suleiman na akachoma baadhi ya nakala za Tawrat.

Masih alikuwa amewehadharisha Mayahudi kuhusu hilo. Inasemekana kwamba Titus aliiharibu Baytul Maqdis, kwa kuhimizwa na MayahudiiliawateseWakristo.

Miongoni mwa wale wanaosema kuwa Aya inaelezea matukio yaliyopita kuna wanaosema kwamba inaelezea yale aliyofanya Nebukadnezzar katikakuiharibu BaitulMaqdis.

Katika Tafsir Al-Manar anasema ninamnukuu: “Jambo la ku-shangaza ni kwamba Ibn Jarir amesema katika Tafsir yake kwamba Aya inaonyesha kuungana Wakristo pamoja na Nebukadnezzar wa Babilon kuiharibu BaitulMaqdis,ambapotukiolaNebukadnezzarlilikuwakablayakujaMasih na Ukristokwamiakamia sitana thalathininatatu(633)”.1

Vile vile kuna wengine wanaosema kuwa Aya inatoa habari ya jambo lililokwisha tokea, kwamba imeshuka kwa ajili ya washirikina wa Kiquraish waliomzuia Mtume na sahaba zake kuingia Makka katika kisa cha Hudaybiya.
Ama wale wanaosema kuwa Aya inatolea habari jambo linalongojewa kutokea, pia nao wamehitilafiana. Kuna wale waliosema kwamba Aya inaonyesha uvamizi wa Wakristo juu ya Baitul-Maqdis na miji mingine katika miji ya Waislamu. Wengine wanasema kuwa inatolea habari tukio la Wakaramet (Karmathians) la kuivunja Al-Ka’aba na kuwazuia watu kuhiji. Kisha kundi linalosema hivi likasema: “Hii ni katika miujiza ya Qur’an,kwa sababu ilitoleahabarimamboyatakayotokea.

Hayo ndiyo kwa ufupi waliyoyasema wafasiri. Na sisi hatutegemei chochote katika kauli hiyo; kwani hakuna dalili ya kiakili au kauli itakayoweza kuituliza akili. Sisi tunategemea dhahiri ya Aya ambayo haipingani na akili wala hakuna kauli ya Hadith inayoeleza jengine. Dhahiri hiyo ni: Wajibu wa kuheshimu sehemu za kuabudu na kuharamishakuziingilianakwambamwenyekukusudiauovu,atapata malipo yake.

Hukumu Za Misikiti

Ni Sunna kujenga misikiti, kuiamirisha kwa sababu ya kutajwa Mwenyezi Mungu, kui-safisha na kuing’arisha, Ni haramu kuivunja, kuingia mwenye janaba na mwenye hedhi.

Ni Suna kuswali raka mbili za kuuamkia (kuusalimia) wakati wa kuingia. Ni makuruhu kujenga mahali palipo juu; kwa sababu Ali (a.s.) aliuona msikiti katika mahali palipo juu akasema: “Kama Sinagogi” yaani Hekalu la Kiyahudi. Kuna hadith inayosema: “Nyumba hujengwa mahali palipo juu na msikiti hujengwa mahali tambarare.” Vile vile ni makruhu kutengeneza mihrabu ndani yake; kwa sababu Amiril-Muminin alipokuwa akiiona husema: “Kama kwamba ni madhabahu ya Mayahudi.” Makusudio ya ya Mihrabu hii iliyo makuruhu, ni ile inayotokeza ndani ambayo huwadhikisha wenye kuswali, bali jamaa wamesema kuwa ni haramu. Ama mihrabu inayojitokeza nje haina ubaya wowote.2

وَلِلَّهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ {115}

Na Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu, basi mahala popote mnakoelekea ndiko kwenye uelekeo wa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua.

وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ بَلْ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَهُ قَانِتُونَ {116}

Na wanasema: Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto. Ameepukana na hilo. Bali ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini. Vyote vinamtii Yeye.

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ {117}

Mbunifu wa mbingu na ardhi; na anapotaka jambo basi huliambia tu kuwa, likiwa.
  • 1. Ilitokea sadfa siku niliyosoma kosa hili la Tabariy, nikasoma makala ndefu katika gazeti la Al-jumhuriya la Misr la tarehe 5 May 1967, inayosema “...Tabariy bila shaka ni nguzo ya wanahistoria wa Kiislamu na kitabu chake ndio kiongozi cha tafsir....” Tabari alikufa mwaka 310 AH yaani karibu miaka 1050 iliyopita. Ikiwa hali ya wanahistoria waliotangulia na wanaotegemewa ni hii, je, ategemewe nani?
  • 2. Amenakili mwenye Miftahul-Karama kutokana na wanachuoni umakaruhu wa kuiinua misikiti na wamesema, bali hujengwa kwa wastani; kama ambavyo imenukuliwa kutoka vitabu saba vya kifiqhi umakaruhu wa mihrabu yenye kutokeza. Mimi ninadhani kwamba W aislamu wanavyojihimu kujenga misikiti mikubwa ni kwa ajili ya kushindana na makanisa tu na kauli ya Amirul Miminin (kama sinagogi) inaashiria hilo