read

Aya 67 – 73: Mwenyezi Mungu Anawaamrisha Mchinje Ng’ombe

Muhtasari Wa Kisa

Aya hizi tukufu haziwezi kufahamika maana yake bila ya kufahamu tukio lililoteremshiwa. Kwa ufupi tukio lenyewe ni hili:

MzeemmojatajirikatikaWaisrailaliuliwanabinamuyake kwatamaaya kurithi mali yake; kisha akadai kuwa ameuliwa na watu wengine, na wakatakiwa walipe fidia. Ukazuka ubishi mkubwa na wakamwendea Musa (a.s.).

Kwa vile hakukuwa na ushahidi wowote wa kugundua mambo walimtaka Musa-kama kawaida yao- kumwomba Mwenyezi Mungu awabainishie muuaji.

Ndipo Mwenyezi Mungu akampa wahyi kuwa wachinje ng’ombe na sehemu ya huyo ng’ombe wampige yule aliyeuliwa atafufuka na ataeleza yule aliyemuua.

Baada ya udadisi mwingi walifanya vile walivyotakiwa kufanya na Yule aliyeuliwa akafufuka na akamtaja aliyemuua.

Maana:

Wakasema: Je unatufanyia mzaha?

Yaani tunakuuliza kuhusu kuuliwa mtu nawe unatuamrisha kuchinja ng’ombe hakika huu ni mzaha.

Akasema: Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kuwa miongoni mwa wajinga.

Yaanimimisifanyimzaha,hatakatikamamboyasiyokuwayakufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu, sembuse hayo ya kufikisha neno la Mungu ambaye umetukuka msemo Wake?

Ilikuwa inatosha tu wamchinje ng’ombe yoyote, kwa sababu waliamrishwa wachinje ng’ombe tu; lakini kwa udadisi wao.

Wakasema: Tuombee Mola wako atupambanulie ni ng’ombe gani?

Wakajibiwa kuwa ni ambaye yuko katikati si mkubwa wala si mdogo, basi fuateni amri wala msingoje, lakini wakarudia tena kuuliza

Wakasema: Tuombee Mola wako atupambanulie rangi yake ni ipi?

Akasema ni wa manjano, lakini tena wakazidi kudadisi na kuuliza swali mara ya tatu, kwa sababu ng’ombe walio katika rangi hii na umri huu ni wengi. Akawaambia kuwa ni yule asiyefanyishwa kazi na asiyekuwa na kasoro yoyote.

Wakamtafuta mpaka wakampata, wakamchinja; kisha wakampiga maiti kwa kipande cha nyama akafufuka na siri ikafichuka baada ya kumtaja aliyemuua.
Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuyisha wafu na anawaonyesha ishara zake ili mpate kufahamu.

Yaani huku kumfufua huyu aliyeuliwa ni ushaidi wazi na dalili wazi ya kufufuliwa watu baada ya kufa, kwa sababu mwenye kuweza kufufua nafsi moja hawezi kushindwa na nyingine. Je, baada ya ushahidi huu wa kuona kwa macho mnaweza mkakanusha na kutia shaka na kuasi? Lakini pamoja na hayo na yasiyokuwa hayo nyoyo zenu zimesusuwaa, bali zimesusuwaa zaidi na zimekuwa ngumu zaidi kuliko jiwe, kama itakavyoeleza Aya inayofuatia.

Baada ya maelezo tuliyoyaeleza kuhusu Mayahudi haiwezekani tena kuuliza swali lolote kuwa, kwa nini Mwenyezi Mungu hakumfufua yule aliyeuliwa tangu mwanzo, na hali Mwenyezi Mungu alikuwa anaweza kufanya hivyo? Vipi anaweza kufufuka mtu kwa kupigwa na nyama ya ng’ombe? Kwa nini ilikuwa lazima ng’ombe huyo? Kisha kuna faida gani ya kumpiga na ng’ombe huyo aliyeuliwa?

Maswali yote haya hayana nafasi baada ya kuthibitisha kuwa Mwenyezi Mungu aliwafanyia Mayahudi mambo maalum wao tu; na kwamba Yeye kwa upande huu ndio amewafadhilisha juu ya watu wote.

ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُمْ مِنْ بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً ۚ وَإِنَّ مِنَ الْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ الْأَنْهَارُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ الْمَاءُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ اللَّهِ ۗ وَمَا اللَّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ {74}

Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, zikawa kama mawe au ngumu zaidi; kwani kuna mawe mengine yanayopasuka yakatoka aji mdani yake; na kuna mengine huanguka kwa sababu ya kumwogopa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu si Mwenye kughafilika na mnayoyafanya.