read

Aya 23-25: Leteni Sura

Kama ambavyo Qur’an imeongoza njia ya kujua kuweko Mwenyezi Mungu Mtukufu vilevile imeongoza njia ya kujua utume wa Muhammad (s.a.w.) miongoni mwazo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyomteremshia mtumwa wetu, yaani Muhammad (s.a.w.).

Basi leteni sura moja iliyo mfano wake.

Makusudio yake ni kushindwa kuleta mazungumzo yaliyo mfano wa Qur’an,wakiwawaondiomabingwakatika fasihinashughuliyaokubwa ni fasihi, lakini si lazima walete yale yanayolingana nayo kwa idadi na umbo. Walipewa hiyari, wakipenda walete yote; Sura kumi au Sura moja.

Vile vile hawakulazimishwa kuleta mfano wa maana yake katika kanuni zatabia,misingiyasharianahabarizaghaibu,baliwalitakiwawalete wanayoyaweza katika maana yoyote na lengo lolote mradi tu ubainifu wake uwe kama wa Qur’an.

Matakwa haya, kama unavyoyaona yasingeliwashinda kama ingelikuwa Qur’an haitoki kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu wao hawakutakiwa wainue jabali au wakaushe bahari, isipokuwa walitakiwa maneno tu. Na wala hakuna kitu rahisi kama hicho kwao. Kwa hivyo kulipothibiti kushindwa kwao, imethibiti kwamba kuna siri Fulani na wala hakuna tafsiri ya siri hii isipokuwa wahyi na Utume.Vilevile kila linaloshinda kutafsiriwa katika elimu halina budi kutafsiriwa na lile lililo juu ya maumbile.

Hakuna kitu chenye nguvu zaidi katika kufahamisha ukweli wa Qur’an kuliko mkatao huu wa kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na hamtafanya ...” mpaka hivi leo hajafanya yeyote baada yao. Na mlango bado umefunguliwa kwa anayetaka kujaribu mpaka mwisho.

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwataja makafiri na adhabu ya moto waliyo nayo, amefuatisha kuwataja waumini, neema na thawabu; kama ilivyo desturi ya Qur’an, kukutanisha mapendekezo na vitisho na ahadi na kiaga kikali, kwa kusisitiza mwongozo na mawaidha.
Wafasiri wengi wamesema kuwa dhamiri katika neno, ‘Mfano wake’ inarudia Qur’an; yaani mfano wa Qur’an, kwa maana ya kuwa leteni sura iliyo na sifa za Qur’an na muundo wake.

Wengine wamesema, bali hiyo dhamiri inarudia mja wetu; yaani mfano wa mja wetu ambaye ni Muhammad (s.a.w.). Kwa maana ya kuwa mleteni Ummiy (mtu asiyesoma), kama Muhammad, aweze kuleta mfano wa Qur’an hii ambayo ameileta mtu huyu Ummiy.

Maana zipo sawasawa kwa kauli zote mbili ingawaje kauli ya kwanza ndiyo mashuhuri na dhahiri zaidi, ambapo Mwenyezi Mungu amesema: Ikiwa mna shaka kwa tuliyomteremshia...Na wala hakusema; ikiwa mna shaka katika Muhammad (s.a.w.). Hata hivyo kauli ya pili ina maana yenye nguvu, kwani lau yakadiriwa kuwa mtu mwenye uwezo analeta mfano wa Qur’an lisingelikuwa hilo ni ushindi. Kwa sababu wajihi wa kushinda unakuja kwa kuletwa na asiyesoma (Ummiy) sio kwa mjuzi mwenye uwezo.

Makusidio ya kuni ni chochote kinachowashiwa moto. Watu ni wale waasi, na mawe ni masanamu waliyokuwa wakiyaabudu washirikina.

Siri Ya Muujiza Wa Qur’an

Utume ni ubalozi kati ya Mwenyezi Mungu na viumbe Wake, anamhusisha nao anayemtaka katika waja wake ili awafikishiye yale wasiyoweza kuyajua; Mwenyezi Mungu amempa nguvu kila Mtume kwa ubainifu ulio wazi juu ya ukweli wa utume wake, ili iwe ni hoja kwa wale waliopelekewa Mtume. Sharti la msingi la ubainifu huo, ni kuwa uwe katika namna maalum inayodhihiri katika mkono wa Mtume na sio mwingine. Hiyo ni kwa kuchukuwa hadhari ya kutatizika kati ya Mtume na asiyekuwa Mtume.

Muhammad (s.a.w.) naye ana ubainifu na dalili juu ya utume wake. Miongoni mwa dalili zake ni hii Qur’an ambayo nakala zake zimeenea kila mahali na Aya zake zinasikika katika vipaaza sauti na katika idhaa za radio mashariki na magharibi, hata Israel.

Njia inayofahamisha kwamba hiyo Qur’an imeshinda, ni kuwa kila mkanushaji alishindwa na anaendelea kushindwa kuleta kitu kama Qur’an au kuleta Sura kama hiyo. Haijanakiliwa habari kuwa kuna mtu aliyeweza kuanzia zamani hadi sasa; ingawaje wapinzani na maadui wa Uislamu na Waislamu ni wengi. Kwa hiyo kimsingi kuthibiti muujiza ndio kuthibiti kwa Utume wa Muhammad (s.a.w.).

Baada ya wanavyuoni kuafikiana kwamba Qur’an ni muujiza wametofatiana katika njia ya muujiza wenyewe na siri yake. Je, ni maajabu na uzuri wa muundo wake? Au ni madhumuni yake mkusanyiko wa elimu, kanuni za sheria na kutolea habari mambo ya ghaibu, n.k.? Au ni mambo yote mawili pamoja?

Wamerefusha maneno katika kubainisha wajihi wa muujiza na kuweka vitabu mahsusi. Sitaki kurefusha yale yaliyosemwa, nafupiliza yale niliyoyaona yana mwelekeo. Kwa ufupi ni kwamba mtu anaweza kumwiga mtu aliye mfano wake kwa kauli na vitendo.

Lakini kumwiga Muumba wake katika athari yoyote miongoni mwa athari Zake, ni muhali. Kwa sababu mtu hawezi kupetuka mpaka wake akiwa kama muumbwa, vyovyote atakavyokuwa na nguvu au mkubwa. Ni vizuri kufafanua kama ifuatavyo:

Kushinda

Tumedokeza kwamba Muhammad aliwashinda wapinzani kwa Qur’an. Hapana shaka kwamba ushindi unatimu na unakubalika ikiwa kitendo chenyewe anakiweza mtu aliyekusudiwa kushindwa; Kama kumtaka mwenye mkono mzima auweke juu ya kichwa chake, au aondoe unyayo ardhini.

Lakini ukimtaka asiyejua kusoma asome na asiyekuwa tabibu atibu au asiyekuwa malenga atunge shairi, haitakuwa ni kushindwa. Muhammad (s.a.w.) amewashinda wapinzani jambo wanaloliweza (maneno) likawashinda, na kushindwa kwao huko kumeongezea Qur’an sifa ya muujiza.

Unaweza kuuliza: Je, muujiza wa Qur’an ni kwa yule fasihi wa lugha ya Kiarabu au asiyejua Kiarabu au mtu dhaifu?

Jibu:Qur’an ni muujiza kwa kuwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu bila ya kumwangalia fasihi na asiyekuwa fasihi, isipokuwa tunajua kwamba ni muujiza kwa kushindwa mwarabu aliye na ufasaha; sawa, na tunapogundua bingwa wa kuogelea anaposhindwa kuogelea kwenye bahari ya mawimbi, kuwa ni kigezo kwamba mwingine asiye bingwa haiwezi bahari hiyo.

Yaani ikiwa fasihi ameshindwa basi mwingine ndio kabisa.
Kwa maelezo yetu sisi mafaqihi ni kwamba kushindwa kwa fasihi ni sababu ya kujua muujiza wa Qur’an na wala sio fungu au sharti lake.

Je, Muhammad Ana Muujiza Mwingine Zaidi Ya Qur’an?

Wengine wanaona kuwa Muhammad (s.a.w.) hana muujiza mwingine isipokuwa Qur’an Ama mimi niko pamoja na wanaoamini kwamba miujiza yake haina ya idadi.

Kwa sababu hekima ya kiungu inapelekea kupatikana namna namna za miujiza kwa kutofautiana hali na watu; kama ilivyofanya hekima yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ya kuapizana Mtume wake na Wakristo wa Najran. Hayo ni ikiwa mwenye kutaka muujiza anautaka kwa kusadikisha.

Ama mwongo mkaidi asiyetoshwa na chochote, anatoshewa na Qur’an tu. Kwa sababu muujiza wa Qur’an ni msingi wa yote, si wa wakati fulani wala na kundi fulani au mtu fulani. Mara nyingine hekima inataka kutoonyeshwa mtu muujiza kabisa; kama vile kutosheka kwa utambuzi na hisia tu, au kwa kuapa Mtume tu.

Imekuja hadith kueleza kwamba mtu mmoja alimwambia Muhammad (s.a.w): “Nina haja gani na muujiza?” Apa tu kwa Mwenyezi Mungu, kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mimi nitakuamini.”

Mtume Akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu mimi ni Mtume wa MwenyeziMungu.Yulemtuakasema:Nashuhudiakwambahapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.”

Ambalo linatufahamisha kwamba miujiza ya Muhammad (s.a.w.) haina idadi, ni kwamba mtu wa dini zamani alikuwa akitoa dalili za Utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.) kutokana na hadith za kusema na mawe, kujiwa na miti na kuchimbuka maji katika vidole vyake na watu walikuwa wakiyakubali wakati huo.

Ama leo ambapo watu wamejitokeza katika maisha bora (na teknolojia), sisi twatoa dalili Utume wake kwamba yeye alisimama pamoja na wanyonge na kuwapiga vita wadhalimu.

Na kwa fadhila zake na fadhila za sheria yake yalivuliwa mataji kutoka katika vichwa vya wastakbari na kutupwa chini ya miguu ya wachunga ngamia na zikagawanywa hazina za wafalme kwa mafukara na maskini.

Kwa vyovyote ilivyo ni kwamba miujiza yote ya Mtume mtukufu ni muhimu na mikubwa, lakini muhimu zaidi katika kukadiria kwangu ni mambo mawili:

1. Kwanza, sheria ya Qur’an ambayo imepanga haki za watu na ufungamano wa watu kati yao juu ya misingi ya uadilifu na kusaidiana. Nitaonyesha kila kitu mahali pake Inshaallah.

2. Pili, maapizano ya Mtume pamoja na ujumbe wa Najran, ambayo ameyataja Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika Sura ya Al-Imran (3).

Hakika maapizano haya ni dalili mkataa na ni mpaka wenye kupambanua, ambao unamweka mpinzani mbele ya adhabu na maangamizo ana kwa ana Maangamizo atakayoyateremsha Muhammad (s.a.w.) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa tamko moja tu linalotoka katika mdomo wake mtakatifu. Hakika ushindi huu hauna mfano wake katika historia ya binadamu. Utakuja ufafanuzi mahali pake Inshaallah.

Tumerefusha maneno katika msingi wa pili (Utume) ili uwe ni uthabiti wenye kuenea wa kila linaloambatana nao katika Aya. Nimetunga kitabu maalum kuhusu Utume nilichokiita Anubuwa wal-Aql (Utume na Akili), kimechapishwa mara nne.

إِنَّ اللَّهَ لَا يَسْتَحْيِي أَنْ يَضْرِبَ مَثَلًا مَا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِنْ رَبِّهِمْ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلًا ۘ يُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ {26}

Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kupiga mfano wowote wa mbu na ulio wa zaidi yake. Ama wale waliomini, wao hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyotoka kwa Mola wao; lakini wale waliokufuru husema: “Nini analotaka Mwenyezi Mungu kwa mfano huu?” Mwenyezi Mungu huwapoteza kwa mfano huo wengi na huwaongoza kwa mfano huo wengi na hawapotezi kwa (mfano) huo isipokuwa wale

الَّذِينَ يَنْقُضُونَ عَهْدَ اللَّهِ مِنْ بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَنْ يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ {27}

Wanavunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha kuifunga na kuyakata aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na kufanya ufisadi katika ardhi. Hao ndio wenye hasara.