Aya 92-96: Musa Aliwajia Na Hoja
Maelezo
Aya hizi ziko wazi na zinayakariri yaliyotangulia. Kwa hiyo tutaeleza maana kwa ujumla. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwamrisha Mtume wake kujadiliana kwa uzuri na wapinzani. Maana ya kujadiliana kwa uzuri ni kuzungumza na moyo na akili. Hoja zote za Qur’an ziko namna hiyo; imewataka wakanushaji wajifikiriie wao wenyewe na kuumbwa mbingu na ardhi; akamwambia mwenye kumnasibisha Bwana Masih uungu, kuwa yeye Masih na mama yake walikuwa wakila chakula.
Na inazungumza na nyoyo za Mayahudi kwa Aya hizi kwa kuwakumbusha neema ya Mwenyezi Mungu ya kuwapelekea Tawrat ambayo ndani yake mna uongofu na nuru; kama zilivyowakumbusha Aya zilizotangulia kukombolewa kwao kutoka kwenye minyororo ya Firaun, n.k.
Kisha Mwenyezi Mungu akawakemea kwa kuabudu kwao ndama wakaikufuru na kuipinga neema Yake, amekariri kutaja kuinuliwa jabali juu yao kutokana na uasi wao na mantiki ya kiakili ikayakadhibisha madai yao ya kuwa wao ni watoto na wapenzi wa Mwenyezi Mungu, na kwamba pepo inawahusu wao tu hataingia mwengine zaidi yao. Vilevile amewaamrisha kutamani mauti ikiwa wao ni wakweli.
Kwa sababu mwenye kuitakidi kwamba pepo ni yake, basi atachagua mauti yenye raha kuliko kuwa na maisha ya balaa na mashaka.
Kisha Qur’an ikatoa habari kwamba wanapupia sana dunia na wana pupa zaidi kuliko wale wasioamini pepo wala moto. Bali hata mtu katika wao anaweza kutamani lau angeliishi miaka elfu. Lakini kurefusha kwake umri hakutamfaa kitu wala hakutamwokoa na adhabu.
Lengo la majadiliano haya ya kimantiki ya akili yaliyo salama ni kuwathibitishia Mayahudi hoja kwamba wao ni waongo wanavyodai kuwa wanaamini Tawrat, na kudai kwao kuwa wao ni taifa teule la MwenyeziMungu.
SheikhMaraghikatikatafsiryakeanasema:“Imekuja Hadith kwamba Abdalla bin Rawaha alipokuwa akipigana na Warumi alikuwa akiimba:
• Kwa hamu naitamani, Pepo ilokaribia
• Yenyevinywajilaini, Vilobaridijamia
• Na Ammarbin YasirkatikavitavyaSiffinalisema:
• Hapo kesho twaazimu, Kukutana na wapenzi
• Muhammad muadhamu, Na swahabaze wa enzi
IkiwaMayahudihawatatamanimautibasiwaosiwakweliwaimani.Hoja hii inawahusu watu wote.KwahivyoniwajibukwaWaislamukuifanya hoja hiyo ni mizani watakayopimia madai yao ya imani na kusimamia haki za Mwenyezi Mungu. Wakiwa wanaona raha kujitolea roho zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, watakuwa ni waumini wa kweli, vinginevyo watakuwa kinyume na madai yao.
Maslahi Ndio Sababu
Hatuna shaka kabisa kwamba suala la kumkadhibisha Muhammad (s.a.w.) sio suala la kuhusiana na ubaguzi tu. Isipokuwa sababu hasa ni maslahi yao ya kiutu na manufaa yao ya kimaada. Kwani wao wanaishi kwa utapeli, riba, na uasherati; na Muhammad (s.a.w.) anayaharamisha hayo.
Vipi wataamwamini? Ushahidi wa hayo ni kwamba wao hawana sababu nyingine isipokuwa pupa ya manufaa ya kibinafsi. Na kila mwenye kupupia manufaa yake, haumfai mjadala mzuri. Na kaui yake Mwenyezi Mungu: “Na utawaona wanapupia zaidi maisha,” inafahamisha hilo.
قُلْ مَنْ كَانَ عَدُوًّا لِجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّهِ مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ {97}
مَنْ كَانَ عَدُوًّا لِلَّهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّهَ عَدُوٌّ لِلْكَافِرِينَ {98}
وَلَقَدْ أَنْزَلْنَا إِلَيْكَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ وَمَا يَكْفُرُ بِهَا إِلَّا الْفَاسِقُونَ {99}
أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْدًا نَبَذَهُ فَرِيقٌ مِنْهُمْ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ {100}