Aya 115-117: Na Mashariki Na Magharibi Ni Za Mwenyezi Mungu
Lugha
Mashariki ni mawiyo ya jua na mwezi, na Magharibi ni machweo. Mwenyezi Mungu amehusisha kutaja Mashariki na Magharibi tu bila ya Kusini na Kaskazini kwa sababu zinaingia sehemu zote, maana hakuna mahali kusiko chimbukiwa na jua na mwezi au kuchwea na jua. Kwa hiyo mgawanyo wa ardhi ni Mashariki na Magharibi tu.
Maana
Na Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu, basi mahali popote mnakoelekea ndiko kwenye uelekeo wa Mwenyezi Mungu.
Yaani ardhi na pande zote na vitu vyote ni vya Mwenyezi Mungu. Popote mtakapo-abudu na popote mtakapoelekea kwa kukusudia ibada na radhi ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atawatakabalia. Basi mwenye kuzuiliwa kufanya ibada ndani ya msikiti, na aabudu popote anapopata na popote atakapoelekea, kwani ardhi yote ni msikiti na pande zote ni Qibla.
Mfasiri mmoja amesema kwamba Aya inahusika na upande tu, na sio mahali, yaani ni upande wowote tu, na wala sio mahali popote. Kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema. “Na Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu”. Lakini mfasiri huyu amesahau kauli yake Mwenyezi Mungu:
“Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa (na) Mwenye kujua” kwamba maadamu pande zote na sehemu zote ni za Mwenyezi Mungu, basi inasihi kumwabudu katika mahali popote na kuelekea pande zote kwa kuangalia kuwa kuenea kwa sababu ya kuhukumu ndio kuenea hukumu kwa kufuata sababu na kilichosababisha. Kwa maneno mengine ni kuwa, maadamu pande zote na mahali pote ni pa Mwenyezi Mungu, basi inasihi kuabudu popote na kuelekea upande wowote.
Unaweza kuuliza, hakika dhahiri ya Aya inafahamisha kwamba Mukallaf ana hiyari katika swala yake kuelekea upande wowote, wala hana lazima ya kuelekea Al-Ka’aba, jambo hilo ni kinyume na Waislamu wote?
Jibu: Ni kweli kuwa dhahiri Aya inafahamisha hivyo na inakusanya swala ya faradhi na sunna katika hali zote, lakini imethibiti kutoka kwa Mtume, Maimamu na kwa Ijmai kwamba swala ya faradhi haiswihi kama mtu akielekea pengine ikiwa anaweza kuelekea Al-Ka’aba na swala ya sunna inasihi kwa kuelekea popote katika hali ya kupanda kwenye chombo cha kusafiria na katika hali ya kutembea kwa miguu. Vile vile inaswihi kuswali swala ya faradhi kwa kuelekea upande wowote kwa yule aliyeshindwa kujua Qibla.
Kwa hadith hizi na Ijmai tunaihusisha kauli yake Mwenyezi Mungu: “Popote mnapoelekea huko kuna radhi ya Mungu”, na swala ya sunna katika hali ya kwenda na kupanda na swala ya faradhi kwa mwenye kuchanganyikiwa.
Vile vile kutokana na hadith na Ijmai tunaihusisha Aya 149 ya Sura hii inayosema: “Na popote wendako geuza uso wako kwenye msikiti mtakatifu (Masjidul-Haram)”, na swala ya faradhi katika hali ya hiyari; na tunaihusisha na swala ya sunna katika hali ya kutopanda chombo cha kusafiria.1
Kwa hali hii linabainika kosa na kuchanganyikiwa katika kauli ya mwenye kusema kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu: “Geuza uso wako kwenye msikiti mtakatifu”, imefuta hukumu ya kauli yake Mwenyezi Mungu: “Popote mnapoelekea huko kuna radhi ya Mwenyezi Mungu”. Kwa sababu sharti za kufuta ni kukanusha na kupingana kati ya yenye kufuta na yenye kufutwa; ambapo hali ya kuthibitisha na kukanusha inakuja katika maudhui moja.
Umeshajua kwamba maudhui ‘elekeza uso wako kwenye msikiti mtakatifu’, yanahusika na swala ya faradhi na sunna katika hali ya kutulia. Na maudhui ya ‘popote mnapoelekea huko kuna radhi ya Mwenyezi Mungu’, yanahusika na isivyokuwa hivyo.
Na wanasema: “Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto”
Tumetangulia kueleza katika tafsiri ya Aya ya 113 kwamba Mayahudi, Wakristo na washirikina, kila kundi lilisema kwamba liko kwenye haki na wengine si chochote. Kwa hivyo dhamiri katika kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na wanasema” inarudia kwenye makundi haya matatu. Imeelezwa katika Qur’an kwamba Mayahudi wanasema: “Uzayr ni mtoto wa Mungu” Na Wakristo wanasema: “Masih ni mtoto wa Mungu” na Washirikina wa kiarabu walisema; “Malaika ni watoto wa Mungu.” Kwa hiyo sio kosa kuwa wanazungumziwa wote.
Ameepukana na hilo.
Ni tamko la kutakasa. Katika Aya nyengine ni:
سُبْحَانَهُ أَنْ يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ ۘ{171}
Kwa sababu kupatikana mtoto kwa Mwenyezi (s.w.t.). Kutalazimisha mambo mengi ya kujihadhari kama ifuatavyo:-
• Kwamba ambaye huzaliwa hana budi kuwa katika jinsi ya huyo aliyemzaa ili aweze kuzaa; na Mwenyezi Mungu hana jinsi.
• Kuzaa kunalazimisha udugu, na udugu unahitaji kuwa na mwili; na Mungu sio mwili.
• Sababu inayowajibisha kuzaa ni kumuhitajia mtoto; na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujitosha na viumbe vyote.
• Ambaye anazaa hana budi kuwa amezaliwa; na Mwenyezi Mungu hakuzaliwa.
Amirul Muminin (a.s.) amesema: “Hak-uzaliwa akawa na mshirika katika utukufu”, Yaani kushirikiana na baba yake katika utukufu. “Wala hakuzaa akawa mwenye kurithiwa kwa kufa”. Yaani kuwa na mtoto atakayemrithi baada ya kufa. “Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo kabisa.”
Jambo jengine ni kuwa kila kilicho katika mbingu na katika ardhi ni chenye kuumbwa na kumilikiwa na Mwenyezi Mungu; na chenye kumilikiwa hakiwezi kuwa mtoto wa Muumbaji. Wala Muumbaji hawezi kuwa ni baba wa mwenye kuumbwa mwenye kumilikiwa. Kwa hali hiyo inatudhihirikia njia ya kutoa dalili juu ya kukanusha Mungu kuwa na mtoto katika kauli yake.
Bali ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini. Vyote vinamtii Yeye.
YaanivinamfuataYeye na kumtii. Unaweza kuuliza kwamba herufi ‘Ma’ hutumiwa kwa kisicho na akili na neno qaanituuna hutumiwa kwa aliye na akili. Sasa imekuaje kitu kimoja mara nyingine kuwa katika ibara ya kisicho na akili na mara nyingine kuwa katika ibara ya kilicho na akili?
Jibu:Mbingunaardhiinakusanyakuwanaakilina kutokuwanaakili;na, Aya imekusanya jumla mbili: ya kwanza imethibitisha ufalme wa vilivyokusanywa na mbingu na ardhi, na jumla ya pili imethibitisha kumtii Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo wakati Mwenyezi Mungu alipotaka kuelezea kumiliki, alielezea kwa kisichokuwa na akili, na alipotaka kuelezea twaa ameelezea kwa aliye na akili, kwa sababu twaa huwa ni kwa mwenye akilinamwenye hiyari.
Mbunifu Wa Mbingu Na Ardhi
Neno Badiu (Mbunifu) lina maana ya mtengenezaji ambaye amtengeneza yeye mwenyewe bila ya kuchukuwa kwa mwengine ni kama kauli yake Mwenyezi Mungu:
وَرَهْبَانِيَّةً ابْتَدَعُوهَا{27}
Kwa hivyo maana yanakuwa: Ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye mwanzilishi wa mbingu na ardhi, basi vipi anaweza kunasibishwa aliyemo ndani yake kuwa ni mwanawe?
Na anapotaka jambo, basi, huliambia tu: Kuwa, likawa.
Hili ni fumbo la ukubwa wa Mwenyezi Mungu na uweza wake; kwamba Yeye kwa kutaka tu, basi jambo huwa, ni sawa kuwe hakuna kitu chochote halafu kipatikane kwa kutaka kwake; au kuwe na kitu, lakini akataka kukigeuza.
Tumeeleza katika kufasiri Aya ya 26-27 kwamba Mwenyezi Mungu ana matakwa aina mbili: Matakwa ya utengenezaji na matakwa ya kutoa sharia. Miongoni mwa matakwa ya utengenezaji ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِنْدَ اللَّهِ كَمَثَلِ آدَمَ ۖ خَلَقَهُ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ {59}
وَقَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ لَوْلَا يُكَلِّمُنَا اللَّهُ أَوْ تَأْتِينَا آيَةٌ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ مِثْلَ قَوْلِهِمْ ۘ تَشَابَهَتْ قُلُوبُهُمْ ۗ قَدْ بَيَّنَّا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ {118}
إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا ۖ وَلَا تُسْأَلُ عَنْ أَصْحَابِ الْجَحِيمِ {119}
وَلَنْ تَرْضَىٰ عَنْكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ {120}
- 1. Tazama tafsiri ya Aya inayofuatia 142 inayotimiza tafsiri hii katika kifungu cha kwa nini swala iswaliwe kwenye upande maalum.