read

Aya 139-141: Je Mnahojiana Nasi Juu Ya Mwenyezi Mungu?

Maana

YamekwishatanguliamaelezokatikaAyaya92-96kwenyekifunguche ‘Maslahi ndio sababu’, kwamba Mayahudi walimpinga Mtume kwa ajili ya masilahi yao na mali waliyokuwa wakiichuma kwa njia ya riba na utapeli. Vile vile pombe, kamari na mengineyo yaliyoharamishwa na Uislamu. Na walimwambia Mtume: “Wewe siye Mtume kwa sababu Mwen-yezi Mungu hapeleki Mtume asiyekuwa Myahudi”. Yaani wanadai kwamba Mwenyezi Mungu ni wao peke yao na kwamba yeye ni Mungu wa kabila na sio Mungu wa Ulimwengu.

Vile vile viongozi wa kikristo na mamwinyi wa kiquraishi walimpinga Mtume kwa kuhofia vyeo vyao na masilahi yao. Wakatoa sababu za uongo, kama walivyotoa Mayahudi. Wakristo walisema kama ilivyoelezwa katika tafsiri mbali mbali: “Lau Mwenyezi Mungu angelituma Mtume, basi angelikuwa katika kabila letu sio mwarabu.”

Ama mamwinyi wa kikuraish, nao walisema: “Lau Mwenyezi Mungu angelipeleka Mtume kutoka katika kabila la Waarabu basi angelimtuma kutoka katika tabaka la kitajiri lenye nguvu; kama ilivyoonyesha Aya hii:

وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ هَٰذَا الْقُرْآنُ عَلَىٰ رَجُلٍ مِنَ الْقَرْيَتَيْنِ عَظِيمٍ {31}

“Na walisema: Kwa nini hii Quran haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii?”. 36 (43:31)

أَوْ يُلْقَىٰ إِلَيْهِ كَنْزٌ أَوْ تَكُونُ لَهُ جَنَّةٌ يَأْكُلُ مِنْهَا {8}

Au (mbona) hakuangushiwa hazina (ya mali); au (kwa nini) asiwe na bustani ale katika hiyo?
(25:8)

Kila kitu kinaweza kuwa na mjadala na hoja; hata kuweko Mwenyezi Mungu pia; isipokuwa kitu kimoja tu, hakiwezi kuwa na ubishani milele kwa wale wanaomjua Mwenyezi Mungu, nacho ni kuihusisha rehema ya Mwenyezi Mungu na neema Yake kwa watu fulani tu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ ۚ {32}

“Je wao wanaigawa rehema ya Mola wako?...” (43:32)

Kwa hivyo ndio Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake Muhammad (s.a.w.) kuwaambia wale waliokanusha.

“Je mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu?” Na hali nyinyi mnajua kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua zaidi anayestahiki Utume na asiyestahiki! Basi msimwingilie Mola wenu, ni juu yetu sisi na nyinyi kuikubali hukumu Yake sio kufanya mjadala katika matakwa Yake na hiyari Yake. Hayo ndio maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na hali Yeye ni Mola wetu na Mola wenu.”

Na sisi tuna vitendo vyetu; na nyinyi mna vitendo vyenu.

Kauli hii ni sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu:

لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ {6}

“Mna dini yenu nami nina dini yangu”. (109:6)

Yaani athari yaugomvi wenukatikakhiyari yaMwenyeziMunguya kunineemesha mimi, itawarudia nyinyi peke yenu; kama vile ambavyo madhara ya ukafiri yanamrudia kafiri na manufaa ya imani yanamrudia mumin.
Na sisi tunamfanyia Ikhlasi Yeye tu. Sio nyinyi kwa sababu mnamhukumu Mwenyezi Mungu na mnataka afanye vile mtakavyo nyinyi. Ama sisi mambo yote tunamwachia Yeye na tunakubali hukumu Yake.

Je mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Ishaq na Yaqub na wajukuu (zake) walikuwa Mayahudi au Wakristo.

Hayo yanaungana na “Mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu?” Maana yake ni jambo gani kati ya mawili mnaloling’ang’ania? Je ni kusema kwenu kwamba Mwenyezi Mungu hamtumi Mtume mwarabu au ni kuwa mko kwenye dini ya Ibrahim na watoto wake na wajukuu zake?

Mking’ang’ania jambo la kwanza basi Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi anapouweka ujumbe wake. Na kama mking’ang’ania jambo la pili, basi Ibrahim aliachana na dini zote za upotofu akashikamana na dini ya haki. Hakuwa Myahudi wala Mkristo.

Kwani dini hizo zilizotokea baada yake na baada ya watoto wake na wajukuu zake. Kwa hiyo kauli yenu ni batili haina hoja.

Qur’an inatuongoza katika ubishani huu kwenye mfumo ambao unatakikana tuufuate kwa kutegemea mantiki ya kiakili yatakayowakinaisha wote wenye akili.

Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu?

Tumetangulia kueleza kuwa Mayahudi na Wakristo, kila kundi lilisema ndilo linalostahiki utume; ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume Wake Mtukufu kuwajibu kwa kauli Yake: Je nyinyi mnajua zaidi mahali alipouweka ujumbe Wake au ni Yeye? Ujumbe ni wa Mwenyezi Mungu na unatoka kwa Mwenyezi Mungu, vipi mnataka kumchagua nyinyi? Je, nyinyi ni mawasii wa Mungu? Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo kabisa. Je, kuna mjinga zaidi ya asiyejua kitu amwambie mgunduzi wa chombo cha anga za juu kuwa mimi ninajua zaidi kuliko wewe?

Sijaona kauli iliyo fasaha zaidi ya kumfanya mtu kuwa mjinga kuliko kauli hii ya Mwenyezi Mungu (Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu?). Tunamtaka maghufira Mwenyezi Mungu na kumtaka hifadhi kutokana na wanayoyasema na wanavyofanya wabatilifu:

Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule afichae ushahidi alionao utokao kwa Mwenyezi Mungu?

Yaani enyi Mayahudi na Wakristo, ushahidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu mmeusoma katika Tawrat. Nao ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atatuma Mtume mwarabu kutoka katika kizazi cha Ismail (a.s.), lakini pamoja na hayo mmeuficha ushahidi mkamkosea Mwenyezi Mungu kwa kukigeuza Kitabu chake kwa batili na kuipinga haki. Kwa hiyo mnapasa laana na adhabu.

Huo ni umma uliokwishapita. utapata uliyoyachuma nanyi mtapata mtakayoyachuma.

Aya hii imekwishatangulia katika Aya ya 134 herufi kwa herufi. Huko imebainisha kwamba Ikhlas ya Ibrahim (s.a.w.) na utukufu wake hauwezi kuwafaa nyinyi na kitu chochote. Hapa imekuja kwa kubainisha kwamba amali ya Mayahudi na Wakristo haiafikiani na itikadi ya Ibrahim na amali yake. Kwa hiyo madai yao kwamba wao wako kwenye mila ya Ibrahim ni uwongo na uzushi. Hayo tumeyazungumza katika tafsir ya Aya ya 48.

Ushahidi

Ni wajibu kwa kila mtu aliyebalehe mwenye akili kuitikia mwito wa kutoa ushahidi; wala haifai kwake kukataa bila ya udhuru. Mwenyezi Mungu anasema:

وَلَا يَأْبَ الشُّهَدَاءُ إِذَا مَا دُعُوا ۚ {282}

“Na mashahidi wasikatae wanapoitwa.(2:282)

Imam Jaafar Assadiq amesema: “Anapokuita mtu ili ushuhudie juu ya deni au haki yoyote usichelewe.”

Jukumu la kuchukua ushahidi linawajibisha kuutoa na ni haramu kuuficha. Mwenyezi Mungu anasema:

وَلَا تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ ۚ وَمَنْ يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ ۗ {283}

Wala msifiche ushahidi na atakayeuficha basi hakika moyo wake ni wenye kuingia dhambini...”(2:283)

Amesema Imam Assadiq (a.s.) “Mwenye ushahidi asikatae kuutoa atakapotakiwa na atoe nasaha wala asilaumiwe”.

Ndio, inawezekana kuacha kutoa ushahidi kwa kuhofia madhara au kumhofia mwingine asiyekuwa na hatia. Kwa sababu hakuna kudhuriana katika Uislamu kutokana na Ijmai na Hadith mahsus.

Wenye Kufanya Ikhlas

Uislamu unawahoji wabatilifu, unawalaumu kwa kiakili na dhamiri. Vile vile unawanasihi kwa uzuri na kuwaamrisha mema, lakini hauwachukulii hatua nyingine zaidi ya mawaidha mazuri isipokuwa kama wakipetuka mpaka, wakafanya uadui kuwapoteza watu wema na kuipoteza haki kwa uzushi na propaganda za uongo. Wakifanya kitu katika hivi itapasa kuwatia adabu. Ameyabainisha Mwenyezi Mungu hayo katika Aya nyingi, kwa mfano:

فَإِنِ انْتَهَوْا فَلَا عُدْوَانَ إِلَّا عَلَى الظَّالِمِينَ {193}

...“Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa madhalimu.” (2:193)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنْفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُمْ مَنْ ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ {105}

“Enyi mlioamini lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu. Hawawadhuru waliopotoka ikiwa mmeongoka. Marejeo yenu yote ni kwa Mwenyezi Mungu; basi atawaambia mliyokuwa mkiyatenda.” (5:105)

Na Aya nyingine ni hii tuliyonayo: “Na sisi tuna vitendo vyetu nanyi mna vitendo vyenu na sisi tunamfanyia Ikhlasi Yeye”