read

Aya 82 – 86: Uadui Wa Mayahudi Na Urafiki Wa Wakristo

Maelezo yanaanzia na Aya 82 iliyokuwa mwisho wa juzuu ya sita, kwa vile inaungana hapa.

Maana

Hakika utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu wengine kwa walioamini ni mayahudi na washirikina.

Yaani mayahudi na washirikina ndio waliokuwa maadui zaidi kwa Waislamu. Mara nyingi watu wameitolea ushahidi Aya hii, kuwa dini ya kikristo iko karibu zaidi na Uislam kuliko dini ya kiyahudi. Hilo ni kosa ikiwa inakusudiwa dini ya kiyahudi na ya kikristo kabla ya kugeuzwa. Kwa sababu dini kwa Mwenyezi Mungu na Mitume wake ni moja tu kwa upande wa itikadi na msingi yake. Na kama ikikusudia baada ya kubadilishwa, basi zote mbili ni sawa (Ukristo na Uyahudi) hakuna yenye afad- hali.

Usahihi ni kuwa uhasama wa mayahudi na washirikina katika Uislam una- tokana na mgongano baina ya mwito wa kiislam na tabia iliyokuwa imeshi- ka kasi katika Bara arabu mwanzo wa utume. Tabia hiyo ilikua ni mashindano ya kupora mali na watumwa. Vilevile riba, ghushi na mengineyo ya kutumia nguvu na utapeli. Tabia hii iliambukiza wafanyibiashara wa kigeni, kama walivyoambukizwa viongozi wa kiyahudi waliokuwa wakimiliki viwanda na biashara ya ndani.

Ukaja mwito wa Muhammad (saw) unaohimiza uadilifu na kukataa dhuluma na unyonyaji wa aina zote, na kuzuia unyonyaji wa mayahudi na washirikina. Kutokana na hali hiyo ndipo pande zote mbili zikakutana na kukubaliana kwa pamoja kujiepusha na dini na itikadi na kuungana mkono kupigana na Muhammad (saw), adui wa wote wawili.

Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa uadui wa mayahudi na washirikina kwa waislam, ulikuwa ni kwa msukumo wa kidunia na wala sio wa kidini, lakini mayahudi walijificha nyuma ya pazia la dini kwa kujionyesha na unafiki; sawa na wafanyavyo leo watu wanaotafuta chumo la haramu. Zaidi ya hayo ni kuwa mayahudi na washirikina wanashirikiana katika ubaguzi. Lakini washirikina pamoja na ujahili wao walikuwa na moyo usiokuwa mgumu, wakarimu na wenye fikra huru zaidi ya mayahudi. Ndio maana wengi wao wakamwamini Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na ni mayahudi wachache tu ndio waliomwamini Muhammad.

Ni Nani Walio Karibu Na Waislamu Kimapenzi.

Na utawakuta walio karibu zaidi kwa mapenzi na waumini ni wale waliosema sisi ni wanaswara.

Baadhi wanaichukulia Aya hii na iliyo baada yake ni chombo cha kukoroga mambo, kwamba Uislamu unaelemea mojawapo ya majeshi mawili hivi sasa. Jambo hili ndilo lililotufanya tufafanue Aya hizi nne kwa namna ambayo haitaacha nafasi kwa wale wanaobadilisha mambo.

Hakika mwenye kuziangalia vizuri Aya hizi, hawezi kuwa na hata chembe ya shaka kuwa zinakamilishana na kwamba haifai kabisa kuifasiri moja pekee yake bila ya kuichanganya na wenzake.
Nazo ziko wazi kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) hakuwafanya bora manaswara, kwa ujumla, kuliko makundi mengine katika kuwa karibu kiurafiki, si kwa umbali wala karibu. Isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) alikusudia kikundi maalum kutoka manaswara (wakristo) kwa dalili ya kuwa yeye hakuishia hapo tu bali aliendelea kusema: “Hayo ni kwa sababu wako miongoni mwao makasisi na watawa, na kwamba wao hawafanyi kiburi.”

Tena akaendelea kusema: Na wanaposikia yaliyoteremshwa kwa mtume, utaona macho yao yanamiminika machozi kwa sababu ya haki waliyoitambua; wanasema: "Mola wetu! Tumeamini basi tuandikie pamoja na wanaoshuhudia."

Maana yake ni kuwa miongoni mwa manaswara (wakristo) wako waliou- jua Uislamu,wakaukubali kwa kutii, kukinai na kwa imani. Historia inathibitisha hivyo; kama ambavyo inathibitisha chuki ya manaswara kwa Uislam na Waislam. Kwa mfano: Fedheha ya Wataliano huko Tripoli ya Magharibi, na Wafaransa katika Algeria, Tunisia, Morocco na Syria. Vile vile fedheha ya Waingereza katika Misr, Iraq, Sudan n.k.

Na leo hii1 Marekani wanaaungana na mayahudi katika kulingamiza taifa la Palestina. Wanawapa silaha za kisasa maharamia hawa, kisha wanafanya uchokozi na kudai kuwa wao ndio waliochokozwa na kuungwa mkono na Marekani katika Baraza la Usalama na Umoja wa mataifa. Hapo Marekani husema: Huu ndio ukweli uadilifu na demokrasia.

Je, baada ya hayo na mengi yasiyokuwa haya, itasemwa kuwa wakristo wote wako karibu kwa urafiki na waislam? Haya hayasemwi ila na mjinga au mwenye kutaka kuwapoteza watu. Kisha mpotezaji huyu atasema nini kuhusu kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na kwa nini tusimwamini Mwenyezi Mungu na haki iliyotujia, na hali tunatumai Mola atuingize pamoja na watu wema?”

Hakiiliyowajianakuiamini,niilewaliyobashiriwanaIsa:

وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِنْ بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ ۖ {6}


"Na kutoa Bishara ya Mjumbe atakayekuja baada yangu aitwaye Ahmad” (61:6)

Hayo, bila shaka, yanatiliwa mkazo na kukanushwa na kauli yake Mwenyezi Mungu aliyoifuatilia bila ya upambanuzi wowote isemayo:

Basi Mwenyezi Mungu atawalipa, kwa yale waliyosema, Bustani zipi- tazo chini yake mito, humo watakaa milele na hayo ndiyo malipo ya wafanyao mema.

Ushahidi wa wema na kulipwa pepo kwa kundi hili la wakristo ni dalili ya mkato ya kusilimu, na kwamba ndilo pekee lililokusudiwa baada ya kusifiwa wema na thawabu.

Ama wakristo ambao wameikana haki baada ya kuijua au wakaipinga bila ya kuangalia dalili zake na ubadhirifu wake, hawa wamekemewa na Mwenyezi Mungu na kuwapa kiaga kwa kusema:

Na wale waliokufuru na kuzikadhibisha Aya zetu hao ndio watu wa Motoni.

Unaweza kuuliza kuwa kauli ya waliokufuru na kuzikadhibisha Aya zetu, inamhusu kila mwenye kukufuru na kukadhibisha. Sasa je, kuna wajihi gani wa kuhusisha wakristo?

Jibu: Mfumo wa maneno unafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) baada ya kuahidi pepo wenye kuamini katika wakristo, amewaahidi moto wenye kung'ang'ania ukafiri miongoni mwao. Ameleta neno la jumla, ili kujumuisha kemeo kwa kila mwenye kuihalifu haki na kuipinga, jambo ambao halipingani na yale tuliyoyasema.
Kwa ufupi ni kuwa Aya hii iko wazi kuwa makusduio ni kundi mahsusi katika wakristo - wale waliojua haki na kuiamini. Na kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawaingiza peponi kwa sababu ya imani yao na amali yao njema.

Tukikadiria kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na utawakuta walio karibu kwa mapenzi na waumin ni wale waliosema sisi ni manaswara," inawakusanya wakristo wote, basi itawajibika tuiache dhahiri ya Aya na tuihusishe na wale walioamini katika wao kwa sababu mbili:

Kwanza, kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaja katika Aya kadhaa kuwa manswara wamemfanyia Mungu washirika, wakaficha jina la Muhammad (saw) na wakawafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu. Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) akakataza kuwafanya mayahudi na manswara kuwa marafiki. Na akasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ {51}


"Enyi Mlioamini msiwafanye marafiki mayahudi na manswara." (5:51)

Tukiunganisha Aya hii, na zilizo mfano wa Aya hii, juu ya kauli yake Mwenyezi Mungu na utawakuta walio karibu zaidi kwa mapenzi na wauminni wale waliosema sisi ni manswara," maana yanakuwa.

مِنْهُمْ أُمَّةٌ مُقْتَصِدَةٌ ۖ وَكَثِيرٌ مِنْهُمْ سَاءَ مَا يَعْمَلُونَ {66}


"Miongoni mwao wako watu washikao njia ya wastani, na wengi wao wanayoyafanya



ni



mambo



mbaya"



(5:66)

Pili, ni kuwa wafasiri wanasema, Aya hii tunayoizungumzia ilishuka kwa sababu ya Najashi, mfalme wa Uhabeshi2 aliyekuwa mnaswara (Mkiristo). Kwani Mtume (saw) alipoona adhabu inayowapata sahaba zake kutoka kwa washirikina, mwanzo mwanzo wa mwito wa Uislam, aliwaamuru kuhamia Uhabeshi na kuwaambia: "Huko kuna mfalme ambaye hadhulumiwi mbele yake yeyote." Wakaenda huko, miongoni mwao akiwemo Jafar bin Abu Talib. Wakapata amani kwa Najashi na ujirani mwema. Hilo lilikuwa mnamo mwaka wa tano wa kutangazwa Utume.

Zimekuja Hadith Mutawatir kuwa Najashi na Baraza lake, la Mambo ya dini na mambo ya kidunia, walisilimu mikononi mwa Jafar bin Abu Talib baada ya kuwasomea Aya za Qur'an Tukufu na kutaja mazuri ya Uislam. Na kwamba walibubujikwa na machozi waliposikia Aya za Mwenyezi Mungu.

Baada ya hayo tunasema kwamba yule anayetolea ushahidi kauli ya Mwenyezi Mungu (Na utawakuta walio karibu zaidi kwa mapenzi na waumin ni wale waliosema sisi ni manswara) kwamba ukristo na wakristo kwa ujumla wote wako karibu zaidi na Uislamu na waislamu kuliko wengine, na kunyamazia Aya zinazokamilisha Aya hii, anayefanya hivyo huyo hakijui Kitabu cha Mwenyezi Mungu au ni mwenye kujionyesha tu kwa kutaka kuongeza chumvi kwa kuutumia Uislamu na Qur'an au anaweza kuwa ni mhaini anayezitia sumu fikra dhaifu katika Uislamu ili zikubali madai ya maadui wa dini, wanaowasaidia Israil na kuwapongeza kwa uchokozi wao kwa Waarabu na Waislam.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ {87}


Enyi mlioamini!


Msiharamish


e


vizur


i


alivy


owahalalishia Mwenyezi Mungu.


W


ala msipetuke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaopetuka



mipaka.

وَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّهُ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي أَنْتُمْ بِهِ مُؤْمِنُونَ {88}


Na kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu vilivyo halali na vizuri, na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye



nyinyi



mnamwamini.

  • 1. Huo ni mwaka 1967
  • 2. Sasa ni Ethipia