read

Aya 7 – 11: Lau Tungelikuteremshia Karatasi

Maana

Na lau tungelikuteremshia maandishi katika karatasi.

Mtume (s.a.w.) alikaa Makka miaka kumi na tatu tangu kuteremshiwa Wahyi mpaka alipohama kwenda Madina. Katika muda wote huu alikuwa akiwalingania watu hapo kwenye Tawhid na uadilifu, na kuwakataza ushirikina na ukandamizaji.

Mfumo wake katika kutoa mwito ulikuwa ni hekima na mawaidha mazuri. Wakamwitikia wachache wao na wengi wao hawakumwitikia.

Isitoshe hawakutosheka kutomwitikia, bali walimpiga vita na kumuudhi kwa mikono yao na mara nyingine kwa ndimi zao. Akawa anavumilia maudhi yao na akijitahidi ili waamini, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamwambia:

وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ {103}


“Na wengi katika watu hawatakuwa wenye kuamini hata ukijitahidi vipi.” (12:103)

Na akasema: Na lau tungelikueremshia maandishi katika karatasi na wakayagusa kwa mikono yao, bila shaka wale waliokufuru wangelisema: Haya si chochote ila ni uchawi dhahiri.”

Yaani lau tungelikuteremshia maandishi katika ukurasa mmoja, wakayaona na wakayagusa na kuyashuhudia na macho yao wangeliyatia ila na kusema ni uchawi.

Aina hii ya watu iko katika kila kizazi na kila mahali. Wakati wetu huu kuna kundi kubwa la watu wasiotosheka na upinzani wa kuhisiwa na kuguswa, mpaka wakaviita vitu kwa vinyume vyake; mbwa mwitu wakamwita punda na nyoka wakamwita njiwa wa amani.

Hii Amerika inapigana vita vya kuangamiza watu katika Vietnam na huku inasema sisi tunajenga na kutumikia uhai. Na hiyo Israil inachokoza, kisha inasema sisi ndio tuliochokozwa.

Wanasema: Mbona hakuteremshiwa Malaika.

Dhamir ya ‘wanasema’ inawarudia washirikina wa Kiquraish. Walimtaka Mtume (s.a.w.) awateremshie Malaika ashuhudie anayoyalingania, na awe na msaada wa kutekeleza risala yake. Mfano wa Aya hii ni kama Aya ile isemayo:

وَقَالُوا مَالِ هَٰذَا الرَّسُولِ يَأْكُلُ الطَّعَامَ وَيَمْشِي فِي الْأَسْوَاقِ ۙ لَوْلَا أُنْزِلَ إِلَيْهِ مَلَكٌ فَيَكُونَ مَعَهُ نَذِيرًا {7}


“Na



wakasema: Ana



nini



Mtume



huyu



anakula



chakula



na



anakwenda sokoni. Mbona



hakuteremshiwa



Malaika



awe



muonyaji



pamoja



naye.” (25:7)

Na kama tungeliteremsha Malaika, hakika amri ingekwishahukumi- wa kisha wasingelipewa nafasi.

Yaani lau kama Mwenyezi Mungu angeliwateremshia Malaika wangelikufa mara moja bila kungojea. Sasa hapa utauliza, kuna uhusiano gani kufa kwao mara moja na kuteremshiwa Malaika?

Baadhi ya wafasiri wamejibu kuwa watu wakimwona Malaika roho zao zitatoweka kabisa kutokana na vitisho wanavyoviona. Lakin kauli hii si ya kutegemewa kabisa. Wengine wakasema: Imetangulia katika hekima ya Mwenyezi Mungu kumwangamiza kila anayehalifu Malaika.

Kauli hii nayo ndiyo haifai kabisa kuliko ile iliyotangulia. Kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t) hawaangamizi wanaomhalifu katika maisha haya, wala Malaika hawana utukufu zaidi ya Mwenyezi Mungu ambaye umetukuka sana utukufu wake.

Jibu sahihi ni kuwa uhusiano uliopo kwenye kufa na kuteremshwa Malaika ni siri ambayo Mwenyezi Mungu hakuidhihirisha kwa waja wake wala siri hii haiwezi kujulikana na akili. Kwa hiyo ni wajibu kunyamaza aliyoy- anyamazia Mwenyezi Mungu.

Na kama tungelimfanya Malaika, bila shaka tungelimfanya mtu.

Lau Mwenyezi Mungu angelimtuma Malaika kwa watu, angekuwa na hali mbili tu: Ama abakie na Sura yake au awe katika Sura ya mtu. Na kubakia katika Sura yake na wakati huo huo kuwa mjumbe kwa watu, ni jambo lisilowezekana. Kwa sababu tabia ya Malaika si kama tabia ya mtu.

Na kufikisha ujumbe kunahitajia kutangamana na hao watu, nako hakupatikani ikiwa maumbile na tabia hazilingani. Zaidi ya haya ni kwamba Malaika hawakuumbwa kuishi katika sayari hii.

Na lau angelikuwa katika mfano wa binadamu wangelisema tunataka Mtume wa kimalaika. Kwa hiyo Malaika kwa Sura yake ya kimalaika hawezi kufikisha ujumbe na kwa sura ya mtu hawezi kuaminiwa na washirikina wa Makka. Kwa hiyo tatizo litabakia hivyo hivyo bila ya ufumbuzi. Kwa hakika ni kwamba Aya hii inaelezea wazi kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwajadili wakadhibishaji kwa mfumo wa mantiki ambao wenye akili wanautumia kuwanyamazisha wabishani wao.

Na tungeliwavisha yale wanayoyavaa.

Yaani lau Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwajaalia Malaika katika Sura ya mtu, watu wangelidhani kwamba yeye ni mtu hasa.

Na hakika walifanyiwa stihzai Mitume kabla yake, lakini yakawazunguka wale waliofanya mzaha miongoni mwao, yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.

Yaani tulia ewe Muhammad kutokana na dharau unazozipata kwa watu wako.! Kwani kudharauliwa Mitume sio jambo lililoanza sasa, bali lilikuwako tangu zamani. Na Mwenyezi Mungu aliwaangamiza waliowafanyia mizaha Mitume wao; na yatawapitia wanaokufanyia mzaha yale yaliyowapitia waliokuwa kabla yao. Hayo yalikuwa, kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwaangamiza waliomdharau Muhammad (s.a.w.); alipomwambia:

إِنَّا كَفَيْنَاكَ الْمُسْتَهْزِئِينَ {95}


“Hakika



sisi



tumekutoshea



(dhidi



ya)



wanaofanya



mzaha.



(15:95)

Sema: Tembeeni katika ardhi, kisha muone ulikuwaje mwisho wa wa wale waliokadhibisha?

Tafsir yake imekwishatangulia katika Juz. 4 (3:137)

قُلْ لِمَنْ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ قُلْ لِلَّهِ ۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنْفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ {12}


Sema:



Ni



vya nani vilivyomo ardhini na mbinguni? Useme


n


i


vy


a


Mwenyez


i


Mungu. Amejilazimishi


a r


ehema.


Hakik


a


atawakusany


a


Siku


ya Kiyama.



Isiyo na shaka.


W


al


e


amba


o


wamezitia


hasarani nafsi zao,



basi wao hawaamini.

وَلَهُ مَا سَكَنَ فِي اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ {13}


Ni



vyake



vilivyotulia



katika usiku



na mchana; naye ndiye asikiaye



na



ajuaye.

قُلْ أَغَيْرَ اللَّهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ ۗ قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ {14}


Sema: Je nimfanye mlinzi


asiyekuw


a


Mwenyezi


Mungu; naye



ndiye



anayel


isha


,


wal


a


halishwi


.


Sema:


Hakika mimi nimeamrishwa


niw


e


w


a


mwanz


o


katika


weny


e


kusilimu


.


N


a


wala


kabis


a


usiw


e


katika


washirikina.

قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ {15}


Sema:



Hakika



mimi



ninaogopa adhabu ya siku kubwa


ikiw


a


nitamwas


i


Mola


wangu.

مَنْ يُصْرَفْ عَنْهُ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمَهُ ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ {16}


Atakayeepushw


a


nay


o


siku


hiyo


,


hakik


a


(Mwenyezi


Mungu


)


amem


r


ehem


u


na


huk


o


ndik


o


kufuz


u


kuliko


wazi.