Aya 100-107: Wamemfanyia Mwenyezi Mungu Washirika
Maana
Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika majini.
Washirikina wako aina nyingi, kuna waliofanya masanamu ni miungu, kuna walioabudu nyota, walioabudu Iblisi na waliofanya giza kuwa ni Mungu. Kundi jingine wamefanya majini kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ameeleza kuwapo Malaika na kwamba amewaumba kutokana na moto.
Katika Aya tuliyo nayo Mwenyezi mungu ameeleza tu kikundi ambacho kimewafanya majini ni washirika wa Mwenyezi Mungu, lakini hakubainisha aina ya majini hawa walioabudiwa na washirikina, je ni majini wa kuwazia tu au ni wengineo?
Kwa ajili hii ndipo wafasiri wakatofautiana. Kuna waliosema ni Ibilisi wengine wakasema ni giza na mengineyo ambayo hayana msingi wowote wa kielimu kabisa.
Kwa maana yoyote itakavyokuwa ni kwamba Mwenyezi Mungu amewajibu washirikina hawa kwa kifupitu Hali yeye amewaumba, na dhamir ya Amewaumba inawarudia majini. kwani wao ndio walio karibu na hiyo dhamir.
Inawezekana kuwa inawarudia wshirikina au wote, kwa sababu Mwenyezi Mungu ameumba majini na watu; kwa maana yakuwa ni vipi Mwenyezi Mungu awe na washirika naye ni Muumba wa kila kitu?
Na wamemsingizia kuwa na wana wa kike na wa kiume bila ujuzi.
Washirikina wa kiarabu walisema kuwa malaika ni mabinti wa Mungu, Mayahudi wakasema Uzair ni mwana wa Mungu na wakristo wakasema Masih ni mwana wa Mungu Maneno yote hayo ni dhana na madai bila ya ujuzi.
Ametakasika na ametukuka juu ya wanayombandikiza nayo
Ametakata Mwenyezi Mungu na upungufu na yuko juu kuliko wanavyomsifu nayo,
Mbunifu wa mbingu na ardhi.
Yaani ameziumba bila ya mfano uliotangulia.
Inawezekanaje awe na mwana hali hana mke wa jinsia yake wala wa jinsia nyingine, kwa sababu hana mfano na kitu kingine naye ni mwenye kujitosha na kila kitu. Umetangulia ufafanuzi katika kufasiri Juz.5 (4:50)
Na ameumba kila kitu.
Na muumbwa hawezi kuwa mshirika na Muumba.
Naye ni Mjuzi wa kila kitu.
Pamoja na hayo ati hajui kama ana mtoto; lau angekuwa naye angelimjua. Kwa hivyo kuacha kujua jambo hakumaanishi kutokuwepo kulingana na asiyekiuwa Mwenyezi Mungu. Ama kulingana na Mwenyezi Mungu ni kuwa ujuzi wake hauepukani na kupatikana yanayojulikana.
Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu hakuna Mola (mwingine) isipokuwa Yeye; Muumba wa kila kitu. Kwa hivyo mwabuduni yeye.
Msemo unaelekezwa kwa washirikina maana ni kuwa Mwenyezi Mungu amekusanya sifa zote za upweke, akaumba ulimwengu na vilivyomo na kupanga mambo yote basi yeye ndiye mwenye haki ya kumpwekesha kwa ibada wala msimshirikishe na yeyote pia msimnasibishie mke na mwana.
Hayamfikii macho.
Tumezungumzia kwa ufafanuzi kuhusu kumwona Mungu katika kufasiri Juz.1 (2:55)
Bali yeye huyafikia macho na mengineyo kwa sababu Yeye amekizunguka kila kitu.
Naye ni Mpole, Mwenye habari.
Mpole kwa waja wake, mwenye habari ya matendo yao na makusudio yao.
Hakika zimewajia busara kutoka kwa Mola wenu.
Makusudio ya busara hapa ni dalili na hoja za kuwepo Mwenyezi Mungu na kuwa Yeye ni mmoja, zikiwamo zile zilizotangulia kupasua mbegu na kokwa (konde), kuumba usiku na mchana, kuumba watu kutokana na nafsi moja na kuteremsha maji ambayo ni uhai wa kila kitu. Kutumia busara kuwa ni dalili ni katika hali ya kutumia kisababishi kuwa ni sababu. Kwani busara ni kujua kunakotokana na na moyo; na kujua huku kunatokana na dalili na hoja.
Basi atakayefungua macho ni faida yake mwenyewe; na atakayeyapo- fua ni hasara yake mwenyewe.
Baada ya kutoa dalili za mkato juu ya haki, hapa Mwenyezi Mungu anase- ma kuwa atakayefuata basi ameifanyia nafsi yake na atakayehalifu basi ameifanyia ubaya nafsi yake mwenyewe.
إِنْ أَحْسَنْتُمْ أَحْسَنْتُمْ لِأَنْفُسِكُمْ ۖ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا ۚ {7}
Na namna hii tunazifafanua ishara na waseme umesoma. Na ili tuyabainishe kwa watu wanaojua.
Wakati wa Ujahiliyya Waarabu walikuwa hawajui kusoma, hawana elimu yoyote. Waliposikia Qur’an na wakaona fani za fasihi, aina kwa aina za hoja zinazowazima wao na yale wanayoyatukuza. Lakini bado waliendelea kukataa. Hali yao ilipokuwa hivyo walitafuta vijisababu wakasema: “Ewe Muhammad, Qur’an hii uliyokuja nayo umejifundisha tu wala sio Wahyi kutoka kwa Mungu”.
Kwa maelekezo haya inatubainikia kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Na namna hii tunazifafanua ishara,’ maana yake ni, tumetermsha katika Qur’an aina na dalili na ubainifu kwa makusudio ya kuongoka kwazo washirikina na waache kumwambia Mtume kuwa wewe umesoma.
Ama kauli yake: ‘Ili tuyabainishe kwa watu wanaojua’ maana yake ni tunazifanua Aya za Qur’an ili wanufaike nazo wale wanaojua maana yake uwaongoze kwenye imani na haki. Ama wajinga na wapotevu hakuna matarajio ya kuongoka kwao. mwisho wa mambo ni kuwa Aya hizi zinakata nyudhuru zao na kuwa ni hoja juu yao.
Fuata uliyopewa wahyi kutoka kwa Mola wako. Hakuna Mola (mwingine) isipokuwa Yeye; na jitenge na washirikina.
Hii ni amri ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake ya kuonya na kutoa bishara kwa Qur’an na kudumu juu ya hilo wala asijali ukanushaji wa washirikina na kukadhibisha na istihzai zao.
La kushangaza ni kauli ya asemaye kuwa Aya hii ni mansukh (imefutwa hukumu yake) na Aya ya kupigana. Mwenyezi Mungu hakumwamrisha Mtume kuacha kupigana na washirikina katika Aya hii mpaka isemwe kuwa ni mansukh ila amemwamrisha kufuatilila kuilingania haki na kutojali ukadhibishaji wa washirikina.
Kimsingi ni kuwa kulingania haki bila ya kujali ni jambo jingine na kupi- gana ni jambo jingine. Sharti ya kwanza ya naskh na mansukh (yenye kufuta na yenye kufutwa hukmu) ni kuwa maudhui yawe mamoja
Na kama Mwenyezi Mungu angetaka wasingeshirikisha.
Yaani Yeye Mwenyezi Mungu mtukufu hakutaka kuwasukuma kwenye imani au kuwalazimisha kuacha ushirikina kwa neno ’kuwa ikawa’ amba- lo ameliumbia ulimwengu. Lau angelitaka waamini kwa matakwa haya basi wasingeshirikisha. Angalia tafsiri ya Juz.1 ( 2:26)
Na hatukukufanya uwe mtunzaji wao wala wewe si mlinzi juu yao.
Jumla ya kwanza na ya pili zina maana moja au maana yanayokurubiana wala hatufahamu lengo lolote la hilo isipokuwa kutilia mkazo; bali mkazo huu vilevile ni mkazo wa kauli yake: ‘Na jitenge na washirikina.’ Kwa sababu lau angelikuwa ni mtunzaji na mlinzi wao, basi isingelijuza kujitenga nao.
إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ {25}
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُمْ {26}
وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ فَيَسُبُّوا اللَّهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمْ مَرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُمْ بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ {108}
وَأَقْسَمُوا بِاللَّهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِنْ جَاءَتْهُمْ آيَةٌ لَيُؤْمِنُنَّ بِهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِنْدَ اللَّهِ ۖ وَمَا يُشْعِرُكُمْ أَنَّهَا إِذَا جَاءَتْ لَا يُؤْمِنُونَ {109}
وَنُقَلِّبُ أَفْئِدَتَهُمْ وَأَبْصَارَهُمْ كَمَا لَمْ يُؤْمِنُوا بِهِ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَنَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ {110}