Aya 109-111: Mitume Na Siku Ya Kukusanywa
Maana
Siku ambayo Mwenyezi Mungu atawakusanya Mitume awaambie mli- jibiwa nini?
Razi anasema: "Desturi ya Mwenyezi Mungu inayopita katika Kitab chake kitukufu ni kwamba yeye akitaja aina yoyote ya hukumu, huifuatishia ama kwa mambo ya Mwenyezi Mungu, au kufafanua hali za Mitume au hali ya Kiyama, ili kutilia mkazo yaliyotangulia. Na alipotaja hapo hukumu mion- goni mwa hukumu za sharia, amefuatisha kwanza kutaja hali za Kiyama kisha hali ya Isa."
Hadhara aliyoyataja Mwenyezi Mungu (s.w.t) hapa ni hadhara ya kutisha, atakayofufulia viumbe kwa ajili ya hisabu na hukumu, kabla ya kutoka hukumu ya msamaha.
Mwenyezi Mungu Mtukufu atawakusanya Mitume wake aliowatawanya katika nchi zake majimbo yake na mabara yake. Ilivyo ni kwamba majim- bo yake na mabara yake Mwenyezi Mungu Mtukufu sio kama haya majimbo yetu na mabara yetu. Ni umma jinsi na kaumu.
Kisha atauliza kila umma na kila watu kupitia Mtume wao: “Wamekwambia nini hawa?” Anakusudia kwa swali hili kutoa hoja kwa waja wake, na kuwaandaa kwa hukumu yake. Mitume watajibu mbele ya hadhara hii: Hatujui, hakika wewe ndiwe mjuzi wa ghaibu. Na ajuaye ghaibu haifichiki juu yake dhahiri.
Unaweza kuuliza kuwa Mitume wanawajua waliowapinga na kuwapiga vita katika uhai wao; sasa je, kuna wajihi gani wa kusema kwao hatujui?
Jibu: Makusudio ya kusema kwao huku sio kukanusha kujua kabisa, bali makusudio ni kwamba elimu yao si chochote kwa upande wa elimu yake Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa sababu wao wanajua yale yaliyodhihirishwa na umma wao naye anayajua waliyoya dhihirisha na kuyaficha.
Atakaposema Mwenyezi Mungu: “Ewe Isa mwana wa Maryam! Kumbuka neema yangu juu yako na juu ya mama yako.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwauliza Mitume wake kwa neno fupi (Mlijibiwa nini), amemhusisha Isa (a.s.) miongoni mwao kwa maneno marefu akitaja neema yake juu yake na juu ya mama yake.
Nilipokutia nguvu kwa roho mtakatifu (ambaye ni Jibril) ukazungumza na watu utotoni ili kumwepusha mama yako na kila dhana na katika utu uzima yaani maneno ya utotoni yalikuwa kama maneno ya utu uzimani.
Na nilivyokufundisha kitabu
Inasemekana makusudio ya kitab ni kuandika kwa sababu neno Kitabu limechukuliwa kutoka katika neno Kitaba (kuandika) na hekima sharia na Tawrat na Injili
Na ulipotengeneza kwa udongo kama umbo la ndege kwa idhini yangu kisha ukapuliza likawa ndege kwa idhini yangu, na ulipowaponyesha vipofu na wenye mbalanga kwa idhini yangu na ulipowatoa wafu kwa idhini yangu.
Umepita mfano wa tafsiri yake katika Juz.3 (3:49) Mwenyezi Mugu amelikariri neno kwa idhini yangu mara nne kwa kutilia mkazo, kwamba kuumba, kufufua na kuponyesha kunatokana na uwezo wa Mwenyezi Mungu, na hakutokani na yeye Isa.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) amedhihirisha vitendo hivi mikononi mwa Isa ili iwe ni dalili ya ukweli wake na utume wake.
Isa Na Utume Wa Utoto
Inaweza ikadhaniwa au kugeuzwa kwamba Isa ni ni mtume mtoto mdogo kwa sababu yeye alizungumza utotoni, huu ni ujinga au kutia sifa.
Kwa sababu yeye alisema utotoni kwa ajli ya kumuondolea tuhuma mama yake tu, kutokana na kauli ya wakosaji, si kwa kuwa ni mtume.
Ikiwa Mwenyezi Mungu amewaondolea taklifu watoto wadogo je anaweza kuwakalifu na mambo mazito; kama alivyoyataja katika kauli yake:
إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا {5}
Na ni nani atakayemsikia na kumtii na yeye yuko susuni? Je inaweza kuwa hoja ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake kwa mtoto anayenyonya? Ni mafunzo gani atakayoyafikisha kwa watu akiwa ananyonya matiti ya mama yake?
Injili zinazotiliwa maanani na wakristo zinaeleza kuwa Isa alitumwa akiwa katika rika la miaka thelathini (30). Imeelezwa katika Injili, Luka, ninanukuu: “Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikua amepata umri wake kama miaka thelathini.” Luka 3:23
La kushangaza zaidi ni kuwa Injili za wakristo zinasema kuwa mwito wa Isa ulianza akiwa na miaka thelathini, kisha mwingine mtia chumvi anasema kuwa Isa ni mtume mtoto, kinyume na Muhammad aliyetumwa akiwa na miaka arubaini1, akitoa dalili ya uzushi wake huu kwamba Isa alizungumza akiwa utotoni kwa ushahidi wa Qur'an, na kujitia kutojua kuwa Isa alizungumza utotoni ili kumtakasa mama yake, mkweli mtakatifu na wala sio kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake akiwa ananyonya.
Na nilipokukinga na wana wa Israili ulipowajia na hoja zilizo wazi; wakasema wale waliokufuru miongoni mwao: Haya si chochote ila ni uchawi tu.
Yamekuja maelezo katika Nahjul-balagha: "Isa alikuwa akifanya mto wa kulalia ni jiwe , akivaa magwanda, akila chakula kisicho na ladha, taa yake usiku ilikuwa ni mwezi, kimbilio lake wakati wa kusi ni Mashariki na Magharibi (hakuwa na kimbilio), matunda na manukato yake ni mimea inayoliwa na wanyama, hakuwa na mke wa kumtia msukosuko wala mtoto wa kumhuzunisha wala mali ya kumsumbua wala tamaa ya kumdhalilisha, kipando chake (usafiri) ni miguu yake na mtumishi wake ni mikono yake"
Pamoja na hayo yote hakusalimika na mayahudi. Walijaribu kumuua wakamwita muongo na mchawi, mama yake wakamwita malaya, si kwa lolote ila ni kwa kuwa ametamka haki akiwalingania kwenye hiyo haki na kuwaamrisha. Haya hayahusiki na mayahudi tu kwani watu wengi humfanyia uadui anayewaongoza kwenye haki.
Na nilipowapa wahyi wanafunzi kwamba, niaminini mimi na mtume wangu, wakasema: “Tumeamini na ushuhudie kuwa sisi ni Waislamu.”
Neno wahyi linatumika kwa maana nyingi, ikiwemo ilham (ufahamisho): kama katika kauli yake Mwenyezi Mungu:
وَأَوْحَىٰ رَبُّكَ إِلَى النَّحْلِ أَنِ اتَّخِذِي مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا {68}
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّ مُوسَىٰ أَنْ أَرْضِعِيهِ ۖ فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ فَأَلْقِيهِ فِي الْيَمِّ {7}
Maana ya wahyi kwenye Aya zote hizo ni ufahamisho na ndiyo maana yaliyotumika hapa.
Unaweza kuuliza: kwa nini Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemkumbusha Isa neema kinyume na mitume wengine pamoja na kwamba fadhila zake na neema zake hazina idadi.
Jibu: Mwenyezi Mungu amejumlisha msemo pamoja na Mitume na akafafanua pamoja na Isa kwa sababu wafuasi wake walizama sana kwa Isa. Ama wafuasi wengine hawakuwahi kudai uungu kwa mitume wao, ndipo ukaja ufafanuzi kwa kuweka hoja.
إِذْ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ هَلْ يَسْتَطِيعُ رَبُّكَ أَنْ يُنَزِّلَ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِنَ السَّمَاءِ ۖ قَالَ اتَّقُوا اللَّهَ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ {112}
قَالُوا نُرِيدُ أَنْ نَأْكُلَ مِنْهَا وَتَطْمَئِنَّ قُلُوبُنَا وَنَعْلَمَ أَنْ قَدْ صَدَقْتَنَا وَنَكُونَ عَلَيْهَا مِنَ الشَّاهِدِينَ {113}
قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا أَنْزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِنْكَ ۖ وَارْزُقْنَا وَأَنْتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ {114}
قَالَ اللَّهُ إِنِّي مُنَزِّلُهَا عَلَيْكُمْ ۖ فَمَنْ يَكْفُرْ بَعْدُ مِنْكُمْ فَإِنِّي أُعَذِّبُهُ عَذَابًا لَا أُعَذِّبُهُ أَحَدًا مِنَ الْعَالَمِينَ {115}
- 1. Mtia chumvi huyu alitaka kumboresha Isa kuliko Muhammad kwa siri, lakini waliomshuhudia Muhammad wanajua ni nani. Angalia tafsiri ya Aya 113 Sura hii