read

Aya 89: Viapo Vya Upuuzi

Maana

Mwenyezi Mungu Hawachukuli kwa viapo vyenu vya upuzi.

Viapo vya upuzi ni kuachia ulimi bila ya kukusudia; kama vile kusema: Hapana wallahi, kumjibu aliyeuliza Je umemwona fulani, au kusema: Sivyo wallah, kumjibu aliyesema: Hutaki hii na … Viapo hivi havitiliwi manani wala havina kafara kama mtu akihalifu lile aliloliapia.

Na aliyesema hawezi kuhisabiwa kuwa mwongo, na mtu yeyote hawezi kumwambia umemwapia Mwenyezi Mungu uwongo.

Kwa maneno mengine ni kwamba viapo hivyo havina athari yoyote ya kiapo. Hata hivyo iliyo bora ni kuacha ikiwa mtu hajaghafilika.

Lakini anawachukulia kwa mlivyoapa kwa nia.

Yaani kiapo cha sharia ambacho ni wajibu kukitekeleza na kutiliwa manani, ni kile anachoapa mtu aliyebaleghe mwenye akili timamu, kwa kukusudia, kutaka na kuwa na hiyari.

Wameafikiana kuwa kiapo kinakamilika ikiwa ni kwa kuapa kwa jina la Allah au kwa mojawapo ya majina yake mema, kama vile Khaliq, Razak (Muumbaji na Mruzuku)

Shia na Hanafi wanasema: “Kiapo hakiwi kwa jina la Msahafu na Mtume au Al-Ka'aba, kutokana na Hadith isemayo: Ambaye ataapa, basi na ape kwa jina la Allah au aache."
Shafi, Malik au Hambal wanasema: “Kinakuwa kwa jina la Msahafu. Hambali amekua peke yake katika kusema kuwa kinakuwa kwa Mtume vilevile.

Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa wastani wa mnavyowalisha watu wenu, au kuwavisha au kumwacha huru mtumwa.

Akiapa na akavunja kiapo, yaani akifanya lile aliloliapia kuliacha au kuacha lile aliloapia kulifanya, ni wajibu kwake atoe kafara akihiyarishwa baina ya mambo matatu.

1. Kwanza, kuwalisha masikini kumi mlo moja kila mmoja, kwa pamoja au mbali mbali kwa sharti ya kuwa ni mlo wa chakula ambacho aghalabu yeye hula na famlia yake. Inajuzu kumpa masikini kibaba cha chakula badala ya mlo. Makusudio ya masikini, ni yule ambaye ni halali kumpa Zaka, Kibaba ni zaidi kidogo ya 800 gm.

2. Pili, ni kuwavisha masikini kumi. Inatosha ile inayoitwa nguo ya kawaida. Kwa sababu sharia haikuhusisha. Kwa hiyo yakachukulia maana yaliyozoeleka bila ya kutofautisha mpya na ya zamani; mradi tu isiwe imechakaa au iliyochanika.

3. Tatu, ni kumwacha huru mtumwa; wala hakuna utumwa leo.

Na asiyeweza kupata (hayo), basi afunge siku tatu.

Yaani akishindwa kuyapata hayo matatu yaliyotangulia, atafunga siku tatu. Na akishindwa kufunga, basi ataomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu na kutaraji msamaha wake.

Hayo ndiyo kafara ya viapo vyenu.

Hayo ni ishara ya kulisha, kuvisha, kuacha huru mtumwa na kufunga baada ya kushindwa na mambo matatu. Na vichungeni viapo vyenu. Kuvifanya ni vya kawaida. Kwani kiapo cha Mwenyezi Mungu kina heshima yake na utukufu wake. Mwenyezi Mungu anasema: "Wala msimfanye Mwenyezi Mungu ni pondokeo la viapo vyenu" Juz.2 (2:224)

Kuna Hadith isemayo: "Hakika Nabii wa Mwenyezi Mungu, Musa aliwaamuru waongo wasiape kwa Mwenyezi Mungu. Na mimi ninawaamuru waongo na wa kweli wasimwapie Mwenyezi Mungu."

Namna hii Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya zake ili mpate kushukuru.

Amesema Razi: "Maana yako wazi." Hata hivyo Mwenyezi Mungu (s.w.t) ametaka kutukumbusha neema za kujua hukumu zake, ili tusizitoe mahali pengine.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنْصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ {90}



Eny


i


mlioamini


!


Hakika


pombe na kamari na mizimu na mburuga ni uchafu katika


kaz


i


y


a


Shetani


.


Bas


i


jie


pushen


i


nayo


,


il


i


mpate


kufaulu.

إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنْتُمْ مُنْتَهُونَ {91}


Hakika Shetani anataka kuwaingizia



uadui na


bughudh


a


bain


a



yen


u



kwa


pombe na kamari na kuwazuia kumkumbuka Mwenyezi



Mungu



na



kuswali, basi



je,



mtakoma.

وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَاحْذَرُوا ۚ فَإِنْ تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ {92}


Na



mtiini



Mwenyezi



Mungu na mtiini



Mtume



na tahadharini na mkikengeuka basi jueni kuwa ni juu



ya mtume wetu kufikisha (ujumbe) tu waziwazi.