Aya 169-171: Wako Hai Mbele Ya Mola Wao Wakiruzukiwa
Maana
Na usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa wamekufa, bali wako hai mbele ya Mola wao wanaruzukiwa.
Anayeambiwa 'usiwadhanie' ni kila mwenye akili. Makusudio ya waliouwawa wako katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kila aliyeuawa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; ni sawa awe amekuwa shahidi mbele za Mtume, kabla yake, au baada yake.
Dhahiri ya Aya ni kwamba mashahidi wako hai hivi sasa, na wala sio kuwa watakuwa hai pamoja na wengine siku ya ufufuo. Na wao wako hai kihakika, sio kimajazi, kama kutajwa vizuri n.k.
Hii ndio dhahiri ya Aya, na yapasa kuitegemea. Kwa sababu hakuna la kuwajibisha kutafuta maana nyingine, maadam uhai uko mikononi Mwenyezi Mungu Mtukufu anampa amtakaye wakati wowote autakao.
Wala hatujui dini au Umma uliotukuza mashahidi katika njia ya haki na uadilifu kama uislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) anasema: "Kuchwewa na jua na kupambaukiwa ukiwa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo ndani yake." Na akasema, "Pepo iko kwenye ncha za mikuki." Ambayo ita- maliza dhulma, shari na batili.
Ama wale wanaokufa shahidi katika njia ya haki, wao na haki ni sawa katika mtazamo wa kiislamu, kwa sababu mwenye kuutoa uhai wake kwa ajili ya haki, utakatifu wake ni utakatifu wa haki yenyewe.
Wanafurahia aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake.
Furaha yao ya fadhila hizi iko mara mbili.
1) Kwa kuwa wao wanastarehe kwa fadhila hiyo.
2) Kwamba hili linafahamisha radhi ya Mwenyezi Mungu kwa wale waliojitolea uhai wao kwa ajili yake, sawa na zawadi ya mpenzi inayofa- hamisha upendo wake.
Na wanawashangilia wale ambao hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.
Kila Mumin anampendelea ndugu yake katika imani lile analolipendelea nafsi yake, lakini kwa sababu ya matatizo na kwa sababu fulani huenda mtu asifikie makusudio. Lakini wale waliokufa shahid katika njia ya Mwenyezi Mungu, wanao ndugu katika imani wanaowajua kwa majina wakiwa na iman na ikhlas kama wao, nao wamewaacha bado wako hai. Basi mashahidi watakapoona fadhila za Mwenyezi Mungu kwao, watafurahi na watashangilia kutokana na waliyoyapata, vilevile kwa ajili ndugu zao wanafuata njia yao katika iman, ikhlas na jihadi.
Mashahidi Watashangilia kwa sababu, ndugu zao walio hai watapata kama waliy- oyapata wao miongoni mwa fadhila na karama.
Aya hii ni dalili ya wazi kwamba mashahidi wako hai kabla ya siku ya kiama kwa sababu kushangilia kwao ndugu zao walio hai kumekwishapatikana, na wala sio kuwa kutapatikana kesho.
Wanashangilia fadhila na neema za Mwenyezi Mungu na kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa waumini.
Unaweza kuuliza: kwa nini limerudiwa neno kushangilia na fadhila?
Jibu: Mashahidi wana furaha tatu.
1) Furaha ya kwanza: ni kwa yale waliyoyapata wao, kulikoelezwa na kauli yake Mwenyezi Mungu. Wanafurahia aliyowapa Mwenyezi Mungu kutokana na fadhila zake.
2) Furaha ya pili: ni kwa ajili ya ndugu zao wanaowajua ambao watajiunga nao, kama linavyoonyeshwa hilo na kauli yake Mwenyezi Mungu. "Na wanawashangilia wale ambao hawajajiunga nao."
3) Furaha ya tatu: ni kwa ajili ya kila Mumini wanayemjua na wasiyemjua shahidi na asiye shahidi. Hilo linaelezwa na kauli yake Mwenyezi Mungu: "Wanashangilia neema za fadhila za Mwenyezi Mungu." Linalotilia nguvu kuwa furaha hii ni kwa ajili ya waumini wote, ni kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa waumini."
Swali la pili. Mwenyezi Mungu ameunganisha fadhila na neema: na kuunganisha kunamaanisha tofauti. Tunavyoona sisi ni kwamba hakuna tofauti, sasa tofauti ni ipi hiyo? Razi amejibu kuwa, neema ni thawabu na ujira anaostahiki mtenda amali kuwa ni malipo ya amali yake. Na fadhila ni ziada (Bahashishi) anayoitoa Mwenyezi Mungu kwa ukarimu sio kwa kustahiki.
Jibu hili la Razi halifungamani na chochote, isipokuwa kupendelea tu kuwepo tofauti. Tunavyoona sisi ni kwamba hakuna tofauti yoyote kati ya kusema: "Amenineemesha" na kusema: "Amenifadhili." Ilivyo hasa ni kwamba misamiati inaungana na kutofautiana tamko tu, kunatosha. Kuungana huku kunaitwa ‘muungano wa tafsir’ (Atfu Tafsir)
الَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِلَّهِ وَالرَّسُولِ مِنْ بَعْدِ مَا أَصَابَهُمُ الْقَرْحُ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا مِنْهُمْ وَاتَّقَوْا أَجْرٌ عَظِيمٌ {172}
الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ {173}
فَانْقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِنَ اللَّهِ وَفَضْلٍ لَمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ {174}
إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ {175}