Aya 2: Mali Ya Mayatima
Na wapeni mayatima mali zao.
Hapana budi yatima awe na mtu mwenye akili na mwaminifu atakayemlea na kuangalia mali yake kwa masilahi yake mpaka aweze kujitegemea na kujua baya na zuri. Aya hii inafungamana na mali za mayatima; inawaamrisha mawasii waichunge hiyo mali na wasiifuje; waitumie vizuri kwa ajili ya kuwalisha na wawape wenyewe watakapokuwa wakubwa.
Wala msibadilishe kibaya kwa kizuri.
Makusudio ya kibaya hapo ni mali ya haramu na kizuri ni mali ya halali. Maana yake msile na kustarehe kwa mali ya yatima na mali zenu mkazibania. Ikiwa mtafanya hivyo, basi mtakuwa mmebadilisha lile ambalo ameliharamisha Mwenyezi Mungu (mali ya yatima) kwa zuri, lile alilolihalalisha (mali yenu). Aya hii iko katika mwelekeo wa Aya isemayo: "Je, mnabadili vilivyo duni kwa vile vilivyo bora?"(2:61)
Wala msile mali zao kwa mali zenu; hakika hilo ni dhambi kubwa.
Makusudio ya msile hapo ni msitumie maana yake, msinufaike na mali za yatima kama mnavyofanya kwa mali zenu. Kwa sababu umuhimu wenu ni kuzichunga tu, na kuzitumia kwa masilahi ya mayatima. Na mkiligeuka hilo basi mtakuwa wakosaji wenye dhambi.
وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانْكِحُوا مَا طَابَ لَكُمْ مِنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا {3}
وَآتُوا النِّسَاءَ صَدُقَاتِهِنَّ نِحْلَةً ۚ فَإِنْ طِبْنَ لَكُمْ عَنْ شَيْءٍ مِنْهُ نَفْسًا فَكُلُوهُ هَنِيئًا مَرِيئًا {4}