read

Aya 187: Kazi Ya Wanavyuoni

Maana

Na Mwenyezi Mungu alipochukua ahadi na wale waliopewa Kitab, lazima mtakibainisha kwa watu wala hamtakificha.

Serikali huanzisha vituo na kumpangia kila mtu kazi yake na pia huchukua ahadi kwa kila mfanya kazi kwamba ataitekeleza kwa uaminifu na kuwa ataadhibiwa yule atakayevunja miiko.

Mwenyezi Mungu ameumba binadamu, akamwamrisha lile lililo na kheri naye na akamkataza lile lililo baya kwake na linalomdhuru. Na amewachagua Mitume ili wafikishe hukumu zake kwa waja wake, akawaamuru wachukue ahadi ya Mwenyezi Mungu na kila wanayemfikishia hukumu hizi kwamba nao wazifikishe kwa watu.

Kwa hivyo, mwanachuoni wa dini ni mfanyikazi wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) wa kubainisha yaliyoteremshiwa Mitume. Yeyote atakayeficha kitu, basi yeye atakuwa na jukumu la kuulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, sawa na mfanyikazi wa serikali anavyoulizwa kama hakutekeleza wajibu wake.

Hayo yameelezwa katika Aya kadhaa walizozitaja wanavyuoni katika mlango wa kuamrisha mema na kukataza mabaya. Kama vile: Hakika wale wanaoficha tuliyoyateremsha, katika hoja na uwongofu; baada ya Sisi kuyabainisha kwa watu Kitabuni, hao anawalaani Mwenyezi Mungu na wanawalaani wanaolaani ( 2:159)

Na Mtume (s.a.w.) amesema: "Mwenye kuinyamazia haki ni shetani bubu." Sikwambii mwenye kuisaidia batili. Vilevile aliulizwa kuhusu jihadi ipendezayo zaidi kwa Mwenyezi Mungu, akasema: "Neno la kumpa ukweli kiongozi dhalimu." Imam Ali (a.s.) naye akasema: "Mwenyezi Mungu hatawaadhibu wajinga kwa kutojifundisha mpaka awaadhibu wenye elimu kwa kutoelimisha."

Haya yanaenea kwa wote, sio kwa wenye elimu tu, au watu wa dini au wasio na dini, au kwa mashinani au matawii, la! Ni kazi ya kila mtu.

Kauli ya Mwenyezi Mungu: "Na Mwenyezi Mungu alipochukua ahadi…" inaenea kwa wote. Kwa sababu waliopewa Kitabu wanaingia mayahudi,manasara na waislamu. Bali Qur'an ndicho Kitabu Kitukufu, kama ambavyo wajibu wa kubain- isha na uharamu wa kuficha unaingia katika Utume wa Muhammad (s.a.w.). na mengineyo katika misingi ya dini na matawi yake.

Wengine wakasema inawakusanya mayahudi na manasara tu, kwa sababu wao walificha dalili za Utume wa Muhammad (s.a.w.) zilizo katika Tawrat na Injil. Lakini ilivyo ni kuwa inaonyesha kuenea kwa kukosekana dalili ya kuhusika.

Wakaitupa nyuma ya migongo yao.

Kutupa kitu nyuma ya mgongo ni fumbo la kuacha kukitilia manani, kama ambavyo kukikodolea macho ni fumbo la kukitilia maanani.

Na wakakiuza kwa thamani ndogo basi ni mabaya waliyoyauza.

Kila anayeificha haki kwa kuathirika na mambo ya kidunia bila ya kuangalia ya akhera, basi atakuwa amemuuzia shetani dini yake kwa thamani ndogo. Wengine hawatosheki na kuificha haki tu, bali wanakigeuza kitabu na Hadith kwa tamaa ya ukubwa na utajiri, na hawa ndio wanaolaaniwa na Mwenyezi Mungu na pia wenye kulaani.

لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوْا وَيُحِبُّونَ أَنْ يُحْمَدُوا بِمَا لَمْ يَفْعَلُوا فَلَا تَحْسَبَنَّهُمْ بِمَفَازَةٍ مِنَ الْعَذَابِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ {188}

Usiwadhanie kabisa wale ambao wanafurahia mambo waliyoyafanya na wakapenda kusifiwa kwa wasiyoyafanya - usiwadhanie kabisa kuwa wataokoka na adhabu, na wana wao adhabu iumizayo.

وَلِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَاللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ {189}

Na ufalme wa mbinguni na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni mwenye uwezo juu ya kila kitu.